jamani mi si mchaga lakini muache chuki binafsi na wachaga
viongozi wao wengi wako commited wa CCM na vyama vingine
Tukubali tukatae sie makabila mengine mengi hatuna asili ya kupendezesha kwetu
Mi nimepita mikoa mingi kidogo tz jamani mingi inafanana DODOM pazuri pale mjini tu kungine majangana wanaoendeleza mji pale%kubwa ni wachaga,wasukuma nk
Wagogi wachache tu wamekalia kulinda.
Shinyanga,kahama pa kwaida sana km hakuna
Kigoma,SINGIDA,RUKWA,MTWARA,TABORA,LINDI NK huwezi fananisha na KLM japo sijafika ila ninaambiwa na watu ninaowaamini
Ushauri makabila mengine tuwe na asili ya kupenda kwetu unless tutaendelea kuwapinga majungu wao wanasongea mbela
asante mkuu, nchi yetu hii inatofautiana sana.
my friend, its very unfortunate kwamba haujui unayeongea naye, mimi unayeongea na mimi ni mchaga wa rombo mashati, lakini sikai kilimanjaro na baba yetu hajatulelea kilimanjaro pamoja na kwamba at least kila mwaka lazima twende kusalimia ndugu. kwa jinsi nilivyokua mikoa mingine, nikahisi namna wachaga wanavyochukiwa kwasababu ya majivuno kama ya kwako, inaniwia shida sana kusapoti point zako kwasababu naona zitasababisha wachaga waendelee kuchukiwa zaidi mikoa mingine, na watapendwa kilimanjaro na arusha tu. ukabila hauna dili.
Pamoja mkuu. Japo uzi ni wa mkoa mzima ila undani wake ni mule mule tu kujustfy maendeleo ya wachagga. Hivi ni lazima kujisifu? Besides, inasaidia nini watu kuzungumzia huo uchagga sooooo muuuuuch.... wanasababisha watu kuwaona wajivuni. In fact, it looks a fact maanake uzi unaohusu huko utaona wanavyojiona ufahari kuwa wachagga as if it was there making. Mbaya sana. Cha msingi ni kupiga kazi kwa kwenda mbele. Acha wengine wakusifu kwa kazi zako.
Mababu zao wangeanza na ujivuni walipokuwa wanaingia mijini hakuna ambae angewapokea. Kila kitabu kizuri kinahimizi watu kujinyenyekesha kwa mafanikio yao. Ndipo wengine watafurahi kuwa jirani nawe. Ona wamarekani wanavyosakamwa.... Ni hayo hayo kujivuna. Nachojua hao wanaojivuna hawana lolote walilochangia uchaggani. Aibu na iwe juu yao 🙁
hahaha, unauliza wana nyumba ngapi wakati nimekutajia hadi idadi mzee? na huo ni mfano tu wa watu wa karibu yangu ambao sio wachaga pamoja na kwamba mimi ni mchaga...mbona mgumu kuelewa mzee we mchaga gani wewe?...umejenga kwenu kwanza wewe au ndo waleee .......
sasa hao ndugu zako watatu ndo wananyumba nyingi kuliko wachagga? we unajua idadi ya wachagga?,
inaonekana haujui ku compare, relevant must be compared with relevant. nahisi unahitaji tuition
Unajua mleta uzi anajibu uzi ulioanzishwa huko nyuma kwamba kwa nini Moshi inakua polepole!!! Sasa mtoa uzi ndo anajibu mapigo kwa hicho alichoeleza. Fine, inaweza kuwa ni kweli lakini uwingi wa shule ni jambo la muda mrefu na siyo indicator ya maendeleo halisi ya eneo. Bado tunapaswa tukubali kwamba speed ya kukua kwa miji miwili maarufu hairidhishi. Na hapa lazima tuseme miji miwili ya Moshi na Tanga kama ingekuwa kwa kasi ile ya zamani hakuna cha Mwanza, Arusha au Mbeya zingetia mguu. Kwa watu wa zamani inasemekana jiji la Tanga lingeendelezwa lingeipita hata Dar na kwa kweli kuna viashiria kuwa Tanga ilijengwa na kupangwa vema halafu baadae ikatoswa au kusahauliwa. Mara nyingi utashi fulani( hasa wa kisiasa) inaweza kuwa chanzo cha yote haya!
Baada ya Uhuru na Serikali zote zilizofuatia zili Stagnise Mikoa ya Tanga na Kilimanjaro...kuna Wakati unaweza kufikiri haya maeneo yalisuswa..,Huwa nashangaa Sana watu kusema Mikoa imependelewa ..Wakati Mikoa ya Ukanda huu iliona ustaarabu hata kabla ya Uhuru .
Kufa kwa Zao la Mkonge,,kudumaa kwa chai ,kufa kwa viwanda tanga ...na Bandari ya Tanga nayo Ika yumba .....Reli ya Tanga- Moshi- voi - Arusha ..Ina miaka 5 Reli haiajapita Juu yake ...hata Baada ya baadhi ya juhudi Za baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wazawa wa Huko kuomba Kama Serikali haitaki Hiyo Reli iwaachie waongee na wadau ili kubeba mzigo toka Bandari ya Tanga hadi Kenya au Mombasa hadi Tanzania ...Kuleta ushindanii..
Kuna Wakati kwa makusudi kabisa Zao la kahawa liliuwawaa ili tu vijana wakimbie waache kuchagua upinzani ...Sasa Matokeo yake Hao Hao Ndio wamepeleka sumu maeneo mengine....kufa kwa Uchumi kumesababisha vijana wa tanga ,Moshi ..kukimbilia mjini na waliobaki wanakunywa viroba ...hakuna Nguvu kazi
Maendeleo mengi yanayoonekana Sasa Kama Shule ,Barabara Za vijijini zilijengwa na Kodi ya WAKAZI kupitia chagga council ie shule,vyuo,hoteli ,scholarships abroad ..,bunge ,palces etc na Tanga kupitia makampuni makubwa ya mikonge,chai etc
Haya maneno ya upendeleo imefikia mahala yaishe ...Kama Mikoa Hii ingeachiwa iende kwa kasi basi mji uliokuwa ukishindana na Tanga au Noshi ni Nairobi na Mombasa .....kwa Taarifa tu Wakati wa Uhuru Tanga ilikuwa nzuri na imeendelea kuliko DAR