Kilimanjaro: Madiwani Siha wagoma Bei ya Maji kupanda kutoka Tsh. 700 hadi 850 kwa Uniti moja

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,622
Baraza la Madiwani Halmshauri Siha Mkoani Kilimanjaro, limesema halipo tayari kuona bei ya maji ikipanda katika Wilaya hiyo na kusababisha usumbufu kwa Wananchi.

Msimamo huo umewekwa wazi, kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichofanyika ukumbi wa Halmshauri hiyo, ambalo katika maswali ya hapo kwa papo Diwani wa Kata ya Kirua Samweli Mmar alihoji uamuzi wa bodi ya maji Lawate Fuka, kupandisha bei ya maji.

Akizungumza kwenye kikao hicho May 17 mwaka huu, Diwani Mmar amesema kuwa amepata malalamiko, Wananchi juu ya kupandishwa kwa bei ya maji kutoka shilingi 700 hadi shilingi 850 kwa uniti moja hali ambayo imeleta mtafaruka kwa Wananchi.

"Ni kweli jambo hili limeleta mtafaruku kwa Wananchi kupandisha bei mara kwa mara mwaka jana uniti moja ilikuwa inauzwa shilingi 700, lakini mwaka huu tena wanapandisha na kufika uniti shilingi 850 kwa kweli Wananchi wangu wameniletea hili jambo, " amehoji.

Diwani huyo haoni sababu za msingi zilizosababisha bodi hiyo kupandisha bei, na hasa ikizingatiwa kuwa miundombinu iliishajengwa na kwamba inatumia mfumo wa maji maji tiririka na hivyo kutokuwa na gharama kubwa za uendeshaji kiasi cha kupandisha bei bila ushirikishwaji wa wananchi.

Juma Jani Diwani wa Kata ya Sanya juu, amesema hao wanapandisha bei, wana mpango wa kuwachafua madiwani, na kwamba asingependa kuona wananchi wanaitisha mgomo kama ulioendeshwa na wafanyabiashara wa Kariakoo.

“Hatutaki kilichotokea Soko la Kariakoo, ambacho ndiyo kama hiki, kabla ya kwenda kwa Wananchi sisi tumekataa na hatupo Tayari, hatuwezi kuruhusu hili jambo,” amehoji Diwani huyo.

Kwa upande mwingine, Diwani wa kata ya Gararagua Zakaria Lukumay, amesema kama bodi imeshindwa kazi, ni vema wakaachia ngazi na siyo kuwasumbua Wananchi, Serikali inatuma fedha nyingi kwenye miradi hii na kwamba ankara wanazolipa wananchi, zinatosha kukarabati miundombinu kama imeharibika

Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Dancan Urasa, Amesema Baraza hilo halipo tayari kuona gharama za maji zinaongezeka na pia halihitaji Wananchi wapate usumbufu kwani mradi ni wakwao na wangeshirikishwa

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, ni Bodi ya Lawate Fuka ndiyo wanapandisha bei ya maji wakati wnzao wa Magadini na Makiwaru wao wameendelea kutoza bei ya zaman ya Sh700 kwa uniti.

Meneja wa Maji Safi na usafi wa Mazingira (Ruwasa), wilayani humo Emmy George, amesema utaratibu wa kupandisha bei upo, japo busara inatuma kuketi na jamii inayohudumiwa na mradi huu ili kukubaliana na bei pendekezwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa hapo labda waombe Serikali itoe ruzuku Kwa hiyo mamlaka yaaji vinginevyo itashindwa kujiendesha na hata hayo maji ya Sasa wataacha kupata.
 
Ila Watz kwa kulalamika hatujambo kweli ndoo 50 kwa 850 ambayo ni sawa na Tsh 17 kwa ndoo wanaona kubwa?
 
Attachments

  • 720EFFE4-D23D-4DD9-AB4B-FAC40F4C727E.jpeg
    720EFFE4-D23D-4DD9-AB4B-FAC40F4C727E.jpeg
    104.7 KB · Views: 4
Waachane nayo wakachote chemchem na mto Karanga, na mto rau na Siha na mto weruweru
 
Ila Watz kwa kulalamika hatujambo kweli ndoo 50 kwa 850 ambayo ni sawa na Tsh 17 kwa ndoo wanaona kubwa?
Kwako unaona ndogo ila ni kubwa.

Kwa jografi ya mkoa wa Kilimanjaro hata hiyo 700 kwa unit ilikuwa kubwa kwa sababu kule maji bado yanatokana na vyanzo halisi vya maji pia sehemu nyingi ufugaji wao hufanyia indoors so hakuna gharama za kusema maji yanawekwa dawa yatakate tofauti na mji kama Dar tunaotumia maji ya Ruvu
 
Back
Top Bottom