Kilimanjaro Express

Kilimanjaro Express

Tulishasema hapa mara nyingi hapa kwamba Kilimanjaro na Dar Express ni moja ya mabasi yenye ubabaishaji mkubwa lakini watu bado wanakuwa vichwa vigumu hawaelewi, badala yake wanakuja hapa kulialia.

Acha wawapigeni tu maana hakuna namna sasa,...
nilishakuonesha bus la kupanda
 
Fujo zilikuwa kubwa sana nikasahau kufanya hivyo. Ila nikiliona tena nitazileta hapa namba za gari kwa sababu nawakumbuka dereva na konda wake pia.
Ukiweka bandiko tu si rahisi kuaminika maana unaweza ukawa unawachafua kwa manufaa yako au ya kampuni yako kibiashara
 
Mimi ninasafiri sana kati ya Dar - Moshi - Arusha kwa basi tajwa hapo juu. Leo tarehe 20 December 2016, mimekuta mfumo mpya kwenye ofisi yao ya Moshi, unalipa Tshs 3,000 na kukatiwa tiketi ya Arusha (Hakuna kulipa ndani ya basi kwa konda). Mfumo huu ni mziri (tena sana).

Kitu kilichonifanya kuandika uzi huu, ni pale basi ilipofika. Kondakta na dereva wa basi lilipofika wakasema "Hakuna nafasi!!! Nafasi zimejaa!!!". Hilo jambo likasababisha abiria kuanza kusukumana tukiwa hatuamini kinachoendelea. Dereva alipoona hilo na yeye akaja kuanza kusukuma abiria ili wasiingie. Nikajiuliza maswali kadhaa:
1 - Kilimanjaro Express ninayoijua mimi ndio kuna utaratibu mbovu hivi? Je ni kwa kuwa ni kipindi cha sikukuu wakiwa wanaamini kuwa watapata tu abiria?
2 - Kwanini ofisi ilikatisha tiketi kuzidi nafasi zilizopo kwenye gari husika?
3 - Haki ya abiria iko wapi hapa?

It's very [HASHTAG]#sad[/HASHTAG], Kilimanjaro Express badilikeni
just report to Sumatra
 
UMETOZWA NAULI KUBWA KWENYE BASI KULIKO UMBALI UNAOKWENDA?
Ni rahisi tu, fanya yafuatayo:
1. Bishia nauli uliyotozwa kuwa si halali. mfano kama unakokwenda ni Dar-Mafinga, nauli inapaswa kuwa 20,000 wewe ukatozwa Dar-Njombe 25,000, bishia. Kondakta akikataa lipa, ingia kwenye gari.
2. Atakupa tiketi imeandikwa Dar-Mafinga 25,000 au atakupa tiketi imeandikwa Dar-Njombe 30,000. Pokea
3. Ipige picha hiyo tiketi, au iscan kisha itume kwenda nambari 0682 887722(kwa whatsapp,telegram au wechat) ukielezea kuwa umetozwa nauli kubwa kuliko umbali wa safari au umepandishwa bus ordinary wakati wewe ulitozwa nauli ya luxury. Na kwamba kondakta amekataa kukuandikia tiketi ya unakokwenda badala yake akakuandikia tiketi inayoonesha kituo ambacho basi linaishia. Au Tuma ujumbe au piga simu kwenda 0800 110 019 au 0800 110 020 (bure). Namba hizi tumia hata pale gari inapokatisha ruti au kuwatelekeza njiani baada ya kuharibika.
4. Basi litasimamishwa kituo cha mbele, utarudishiwa nauli yako. Kama limekamatwa na askari polisi basi dereva au kondakta atarudisha nauli na 30,000 itamhusu. Akikamatwa na SUMATRA basi atarudisha nauli na faini ya sh.250,000 itamhusu.
5. SAMBAZA UJUMBE HUU KADIRI UWEZAVYO, MUELIMISHE MWENZIO
KWA HISANI YA RSA TANZANIA,
USALAMA BARABARANI JUKUMU LETU SOTE
 
Mimi ninasafiri sana kati ya Dar - Moshi - Arusha kwa basi tajwa hapo juu. Leo tarehe 20 December 2016, mimekuta mfumo mpya kwenye ofisi yao ya Moshi, unalipa Tshs 3,000 na kukatiwa tiketi ya Arusha (Hakuna kulipa ndani ya basi kwa konda). Mfumo huu ni mziri (tena sana).

Kitu kilichonifanya kuandika uzi huu, ni pale basi ilipofika. Kondakta na dereva wa basi lilipofika wakasema "Hakuna nafasi!!! Nafasi zimejaa!!!". Hilo jambo likasababisha abiria kuanza kusukumana tukiwa hatuamini kinachoendelea. Dereva alipoona hilo na yeye akaja kuanza kusukuma abiria ili wasiingie. Nikajiuliza maswali kadhaa:
1 - Kilimanjaro Express ninayoijua mimi ndio kuna utaratibu mbovu hivi? Je ni kwa kuwa ni kipindi cha sikukuu wakiwa wanaamini kuwa watapata tu abiria?
2 - Kwanini ofisi ilikatisha tiketi kuzidi nafasi zilizopo kwenye gari husika?
3 - Haki ya abiria iko wapi hapa?
It's very [HASHTAG]#sad[/HASHTAG], Kilimanjaro Express badilikeni

Wewe nae ni walewale tu! Utakataje tiketi hujaona basi unalosafiri nalo!? Kizazi kama chenu sijui kitaisha lini!.
 
Mbona kuna tetesi kwamba jamu ya ARUSHAK ILIMANJARO sio kubwa na had wanasema mabasi yamewekwa packing hakuna abiria
 
Ukiweka bandiko tu si rahisi kuaminika maana unaweza ukawa unawachafua kwa manufaa yako au ya kampuni yako kibiashara

Ningeweza kutaja namba yeyote ya basi lao (kama nina nia ya kuwaharibia biashara). Ila nimesema ukweli kuwa sikuzinakili.
 
Umesahau dar express wana huduma mbovu kweli. Leo nmewahi ili nikakate tiketi, nmekaa kwenye foleni kuanzia saa moja inafika saa tatu kasoro wanasema nafasi zimejaa gari za tar 21 na 22. Tukawaomba watukatie za tar 23 wakagoma kabisa. Kilichonisikitita wakati tupo kwenye foleni kuna madalali waliokua wanaingia ndani wanareserve nafasi za wateja wao. Pia majibu ya wahudumu hayakua ya kuridhisha kabisa......
 
Fujo zilikuwa kubwa sana nikasahau kufanya hivyo. Ila nikiliona tena nitazileta hapa namba za gari kwa sababu nawakumbuka dereva na konda wake pia.
Acha ubabaishaji, kwani kwenye ticket uliyokata si inaandikwa namba ya gari!!?
 
Tulishasema hapa mara nyingi hapa kwamba Kilimanjaro na Dar Express ni moja ya mabasi yenye ubabaishaji mkubwa lakini watu bado wanakuwa vichwa vigumu hawaelewi, badala yake wanakuja hapa kulialia.

Acha wawapigeni tu maana hakuna namna sasa,...
Mimi sijawahi Panda gari nyingine zaidi ya dar express.. Wana madereva makini sana...so nikiwa na Safari huwa siumizi kichwa hata kidogo.... Ni magari ya uhakika na madereva wao wanajielewa
 
Acha ubabaishaji, kwani kwenye ticket uliyokata si inaandikwa namba ya gari!!?

Hizi tiketi za Moshi - Aruaha hawaandiki, na hiko kitu ndio kinatia dosari kwenye mfumo huu. Wangeandika namba ya basi ingetusaidia abiria kujua lipi ndio gari langu.
 
Back
Top Bottom