Kilimanjaro Express mnakera sana kurudia filamu

Kilimanjaro Express mnakera sana kurudia filamu

Tony Yeyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
733
Reaction score
570
Hawa jamaa ukipanda basi zao zile za DAR-ARUSHA, utakoma yani wanakuwekea muvi zile zile.

Yan ata upande mara buku muvi zao ni zile zile.

Kwani mnashindwa nunua CD zingine?
 
😂😂😂😂Basi nyingi sana sizani kama wanabadilishaga Moviee.

Halafu hua zinafanana, sijui wanarushiana kwenye Grp zao za WhatsApp.

Shida inakuja ukiitilia maanani au kushughulisha ubongo.
 
Ulipandaa ukaangalie movie

Unatv kwenuu usiniaibishe bana

#PANDANDEGE UONE MARUDIO YA KAIZERCHIEF NA SIMBA SSC
 
Movie za kina Mkojani na Tin White bila Shaka.😂😂😂

Hawa jamaaa inabidi siku wafanye ukaguzi wa ghafla ili wapate angalau tu'malipo kwa mabasi yanayosafiri mikoa mbali mbali
 
Scandinavia ndiyo kampuni pekee iliyomudu biashara ya usafirishaji abiria mikoani, kwa bahati mbaya sana kampuni ilikufa
 
Nadhani inabidi waboreshe waweke screen kwenye kila siti pamoja na earphones ili kama mtu anahitaji kuangalia movies basi aangalie tena kwa sauti inayomtosha yeye msikilizaji, hapo hatowabughuzi abiria wengine!
 
Mabasi yanayo usb charging port. Nini kinakuzia kutazama movies ulizo download awali kwenye simu/device yako badala ya kutazama movie zile zile za mabasi.? Safari maandalizi -snacks,movies,muziki tulivu,novel pdf format. Bon voyage
 
Mkuu kuna mabasi ukipanda unakuta wameweka series za Kijapan na Kichina zile watu wanapaa angani, halafu kuna mikelele ya mtu anayejiita mtafsiri. Inaboa
 
Ilimudu vipi,,, Kama ilipata hasara na kujifia tu
Haikupata hasara. Waliokuwa wamiliki walijiwekea malengo ya kuiendesha kampuni kwa muda wa miaka kadhaa kisha wanaachana nayo na ndivyo walivofanya.
 
Umelipia Nauli ili ufike tu kule uendako au utizame ' Series ' mpya mpya ndani ya Basi? Miswahili bhana taabu tupu tu kila Uchao.
 
Mkuu kuwa na movies nyingi za kuonyesha sehemu kama ile ni kazi kwani wanapanda watu wa umri,dini, makabila,mataifa tofauti tofauti. Unaweza kuweka movie katikati jamaa wanakula kitimoto,wametukana nk
 
Mabasi yanayo usb charging port. Nini kinakuzia kutazama movies ulizo download awali kwenye simu/device yako badala ya kutazama movie zile zile za mabasi.? Safari maandalizi -snacks,movies,muziki tulivu,novel pdf format. Bon voyage
Kila mtu anamiliki smart phone?
 
Ni mabasi yote mzee!!
Wanaweka movie za hivyo hovyo.
Na kama ni safari za masafa marefu, 950+ km ndio kero zaidi.
 
Back
Top Bottom