Mwl Razaq Mtele Malilo
Member
- Sep 29, 2016
- 34
- 83
KILICHOTOKEA UCHAGUZI WA DARUSO-MLIMANI (UDSM) NI ISHARA KUWA CCM IMECHAKAA
Na Mwl Razaq Mtele Malilo
Tarehe 20/4/2017 kulikuwa na uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Rais wa serikali ya wanafunzi CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (CKD) maarufu kama UDSM, uzinduzi uliofanyika katika viunga vya YOMBO 4 moja ya kumbi kubwa za mihadhara katika chuo hiki kikongwe Tanzania.
Katika uzinduzi huo uliojumuisha wagombea watatu wa nafasi ya urais ambao ni JOHN JEREMIAH, EMMANUEL PAUL na RICHARD AUGUSTINO.
Katika uzinduzi huo ndugu JOHN JEREMIAH alionekana kuwa na mvuto mkubwa huku akishangiliwa kwa mbwembwe mno ndani ya ukumbi akifuatiwa na EMMANUEL PAUL ambaye alishangiliwa kwa mbwembwe wenda kwa sababu tu anatokea ndaki yenye wanafunzi wengi katika chuo ambayo ni ndaki ya Insia yaani College of Humanity (COHU) na kelele hizo kuhusishwa na siasa za undaki.
Ndugu RICHARD AUGUSTINO alionekana kuwa na hoja nzuri lakini Sera yake ya kuirudisha UDSM kwenye Shirikisho la Vyuo vikuu nchini (TAHILISO) ambapo udsm ilijitoa chini ya utawala wa KITAPONDA AHADI ,Sera hii ilipelekea ndugu Richard kupingwa na wanaharakati wa Siasa za DARUSO kwa nguvu zote kwani hawaoni umuhimu wa kuwa na shirikisho hilo ambalo limeshindwa kupigania maslahi ya wanavyuo nchini.
Hii ilipelekea ndugu Richard kuonekana kupoteza ushawishi na hata tafiti iliyofanyika na Taasisi ya MALILO TRUTH GROUP (MTG) kumweka katika nafasi ya mwisho kwa asilimia ya ushindi kwa mujibu wa tafiti walioufanya.
Ndugu EMMANUEL PAUL alionekana ndiye mshindani mkubwa wa JOHN JEREMIAH lakini kadri ya siku zilivyokwenda ndugu PAUL alikuwa anapoteza ushawishi wa kisiasa na hii baada tu ya kusambaa kwa picha ikimuonesha ndugu EMMANUEL PAUL akiwa kwenye sare za CCM akiwa na makada mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye sare na kuelezwa kuwa alikuwa anagombea uongozi ndani ya chama hiko kupitia UVCCM lakini alishindwa kwenye uchaguzi huo.
Zipo taarifa za ndani zinazosema picha hiyo ilisambazwa na moja ya kada mkongwe wa CCM hapa UDSM ambaye alikuwa akimuunga mkono ndugu JOHN JEREMIAH na lengo la kusambaza kwake ni kumkatia upepo ndugu EMMANUEL PAUL ambaye alikuwa anampa homa ndugu JEREMIAH.
Baada tu ya kusambaa picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii hasa makundi ya whatsapp ya wanaudsm, Instagram na Facebook ilikata kabisa upepo wa ushawishi wa ndugu EMMANUEL PAUL na kumpoteza kumtoa kabisa kwenye ushindani.
Na hii ikamfanya ndugu Paul kuanguka vibaya hata kupoteza kura kwenye ndaki yake ya nyumbani ndaki ya insia na kuwa mtu wa mwisho kwenye matokeoa ya uchaguzi.
Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa za UDSM wanahusisha tukio hili la kutumia picha ya CCM ili kumpotezea mtu ushindi na kumchafua na hadi kupelekea kuanguka kabisa na kuwa wa mwisho ni ishara tosha kuwa CCM imechokwa hususani na wanavyuo.
Ni jambo ambalo si zuri kwa CCM kwamba mgombea yeyote ambaye atabainika ni CCM kwa dhahiri basi hawezi kushinda katika chaguzi za vyuo vikuu maslani CHUO KIKUU CHA DSM kwakuwa tu ya UCCM wake hata kama ana uwezo.
Hii inamaanisha kuwa CCM imepoteza ushawishi miungoni mwa wanajamii hususani wasomi wa vyuo vikuu.
CCM UDSM inatakiwa ikae ijiulize kuanguka kwa kifo cha mende kwa ndugu PAUL kwa sababu tu ya picha iliyosambazwa ya mgombea akiwa na makada wa CCM ikapelekea kupoteza kwa mgombea.
CCM ijiulize ni kwa nini iwe hivi ? Kisha ijitathmini imewafanyia nini wanaudsm hadi wawe na hasira na mgombea kwakuwa tu ameonekana akiwa kwenye sare za CCM na watu wakamchukia moja kwa moja hadi kupoteza kura hadi kwenye College yake ya COHU ambayo mara nyingi mgombea anayetokea college yao lazima wampe kura za kutosha.
Hili ni jambo ambalo CCM inatakiwa ijiulize na kujifunza.
Katika uchaguzi huo wa DARUSO ndugu JOHN JEREMIAH aliibuka mshindi akifuatiliwa na ndugu RICHARD AUGUSTINO na mwisho kabisa ni ndugu EMMANUEL PAUL
DEMOKRASIA NA HAKI NDIO MISINGI YA AMANI
By Mwl Razaq Mtele Malilo
BAED-UDSM