Kilichotokea kwa Mzee Mkapa kisitokee kwa kiongozi mwingine

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
87
1,595
KILICHOTOKEA KWA MKAPA KISITOKEE KWA KIONGOZI MWINGINE.

Na Bashir Yakub, Wakili.
+255 714 047 241.

Haikuwa sawa kuupeleka mwili wake kila asubuh uwanjani, kuuanika pale masaa 12, na kisha kuurudisha tena kila jion,kwa siku tatu mfululizo.

Mzee Mkapa ni kiongozi wa kitaifa na hivyo ilikuwa lazima aagwe kitaifa na viongozi pamoja na wananchi.

Hata hivyo, maoni yangu ingetengwa tu siku moja ambayo mwili wake ungebebwa siku hiyo hiyo moja na kupelekwa uwanjani kwa ajili ya viongozi na wananchi kuaga, na kisha kwenda kuzikwa kwao moja kwa moja.

Au kama kungekuwa na ulazima wa kumuaga kwa siku tatu mfululizo basi mwili ungebakizwa palepale uwanjan, kuliko kuzunguka nao asubuh na jion barabarani.

Na kama hakukuwa na vifaa vya kuutunza palepale uwanjan, basi ni wakati muafaka sasa wa kuwa na vifaa hivyo "mobile morgue equipments" ili jambo kama hili lisitokee tena kwa kiongozi mwingine.

Sijui, lakini nadhan angekuwa na uwezo wa kuzungumza angesema inatosha.

Sina kumbukumbu nzuri kwa Mwalimu ilikuwaje, ila sidhan kama ilikuwa hivi.

Na hata kama ilikuwa hivi swali kwetu ni je, tunaonaje, jambo hili bado ni zuri kwa viongoz wetu wanaotutangulia??

Ninachojua kumsitiri mfu sio tu kumzika chini ya udongo, bali ni pamoja na kumuepusha na mizunguko ya aina hii.

Nikiuliza hapa nani angependa akifa awe anapelekwa uwanjan asubuh, anakaa huko masaa 12, na kisha jioni anarejeshwa nyumban kwake, kwa siku tatu mfululizo, nadhan hatapatikana.

Hakuna atayekubali kwake au kwa mtu wake.

Haikuwa sawa kuuzungusha barabarani kwa kiwango hicho mwili wa mzee wetu, basi tusifanye hivyo tena.
 
Ninachojua kumsitiri mfu sio tu kumzika chini ya udongo, bali ni pamoja na kumuepusha na mizunguko ya aina hii.

Nikiuliza hapa nani angependa akifa awe anapelekwa uwanjan asubuh, anakaa huko masaa 12, na kisha jioni anarejeshwa nyumban kwake, kwa siku tatu mfululizo, nadhan hatapatikana.

Jr
 
Mimi hapa kaka... Asubuhi wanipeleke kijiweni kwangu napopata kahawa, mchana nipitishwe nilipozoea kupata ugali samaki, saa tisa nipitishwe kiwanja nilichokuwa napiga kilaji, jioni nipitishwe kwa mchepuko wangu Eva kisha wanirudishe kwa mama Bhoke nikalale kwa ratiba za kesho yake.
 
Na kama hakukuwa na vifaa vya kuutunza palepale uwanjan, basi ni wakati muafaka sasa wa kuwa na vifaa hivyo "mobile morgue equipments" ili jambo kama hili lisitokee tena kwa kiongozi mwingine.
Naam matumizi mengine muafaka ya Kodi zetu...., ila..., why not badala ya kununua hizo mobile morgue equipment tusiongeze ukubwa wa mortuaries ili kina kabwela wengi zaidi wapate hii huduma..., au all animals are equal but some are more equal than others ?
 
Back
Top Bottom