Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,102
- 4,960
Kuna kelele zinaendelea mitandaoni kuhusu mtoto wa Rais aitwaye Abdul. Kelele hizi japo hazina ukweli wala uthibitisho ila zina kila dalili ya kuwa na uhalisia kwa kiasi flani
Kelele zilianza Abdul alipokwenda Uganda Uganda na kupokelewa kama kiongozi wa kitaifa. Watu walihoji.
Kwa sasa anatajwa si kwa afya bali kwa matukio ya ufisadi. Kwa mtoto wa Rais kutajwa kwa rushwa ni doa kubwa linalohitaji kukemewa. Lisipokemewa hata wasio watoto na ndugu wa marais wanaokamatwa na kufungwa kwa rushwa wanapaswa kuachwa.
Hali kama hii tumeona kwa familia ya mzee Mwinyi lakini pia tumeiona kwenye familia ya JK ambapo mke wake na mwanaye wapo bungeni. Lakini mbaya zaidi ni kwamba watoto wa JK pia walitajwa kwenye skendo kama hizi na alipoingia JPM alipambana na familia hii jambo lililomkera sana JK.
Japo JPM alimteua mwanaye lakini hakuna connection iliyokuwepo kati ya familia yake na mfumo wa serikali. Hakuna siku mtoto wa JPM alituhumiwa kutoa amri au kuwa mstari wa mbele kwenye taasisi ya urais.
Mzee Mkapa hadi sasa hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa watoto wake na familia yake kwenye siasa za Urais. Mkapa alitenganisha kabisa majukumu ya serikali na majukumu ya familia.
Mwalimu Nyerere sina sababu ya kumjadili sana. Alifanya kwa vitengo tena kipindi ambapo nchi ipo gizani.
Kutokana na tuhuma zinazosmbazwa zikihusisha hadi taasisi kubwa duniani cha uchunguzi tunaamini mtoto wa rais anapaswa kutajwa vikali hivi? Nini kifanyike kutenganisha familia na kiti cha uongozi?