Kilichosababisha umeme kukatika alfajiri

Kilichosababisha umeme kukatika alfajiri

Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mbeya , Iringa na baadhi ya maeneo ya Mkoanwa Dar es Salaam huduma ya umeme imerejea
Mmerejesha ndio, lkn cha moto tumekiona tangu hiyo saa nane
 
Tanesco mnatakiwa kujitathmini aisee. Hii imekuwa ni aibu ya taifa kila siku mnakata umeme. Nadhani kuna shida ambayo huwa hamuisemi.
Hivi hamuwezi kujifunza hata kwa majirani zetu wakenya mjue wanatumia mbinu gani. Mbona wataalamu wako wengi tatizo nini.
Jirekebisheni aisee tunawezaje sasa kuwa na Tanzania ya viwanda kwa mtindo huu
 
Kitengo cha Mahusiano kwa wateja TANESCO. Hongera. Tulikosa viti hivi kipindi fulani.
 
Mmetuharibia "game" la asubuhi!! hahahah
Ila naona usharejea
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKATIKA KWA UMEME KATIKA MIKOA ILIYOUNGWA KATIKA GRID YA TAIFA

Tunawataarifu Wateja wetu na Wananchi kwa ujumla kuwa, majira ya saa 8:49 Usiku kumetokea hitilafu katika mfumo wa Grid ya Taifa. Hitilafu iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya umeme katika Maeneo na Mikoa yote iliyoungwa kwenye Grid ya Taifa.

Baada ya Hitilafu hiyo Kutokea, Mafundi na Wataalamu wa Shirika Wamechukua hatua za haraka na bado wako kazini Kuhakikisha kuwa Huduma ya Umeme inarejea mapema kadri iwezekanavyo.


Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Tafadhali usishike wa kukanyaga waya ulioanguka au uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

MACHI 10, 2018


National Grid isiyo na back up....yaani ikitokea hitilafu ni Kigoma tu wanaobaki na umeme kwa kuwa wanatumia jenereta
 
Tanesco tanesco tanesco sijui mnaridhishana matatizo? Au kuna watu miongoni mwenu mnavibanda umiza Vya kuangalizia mipira? Maana morogoro DC kila siku kukiwa na mpira lazima saa 10 jioni muondoke na Umeme wenu sasa mnatupa hofu wateja wenu na tuwafikirie kuwa huenda nyinyi mnahusika moja kwa moja kwenye hili la Umeme kukata huku mkiwa na vijenereta uchwara vyenu Vya kuonyeshea mpira
 
Back
Top Bottom