Kilichosababisha mauaji ya Kamanda Barlow chabainika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichosababisha mauaji ya Kamanda Barlow chabainika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Oct 17, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  MWELEKEO wa upelelezi wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow umebadilika na sasa tukio hilo linahusishwa na kisasi cha mapenzi na tayari mtu mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi Mwalimu Dorothy Moses kutiwa mbaroni na polisi.

  Awali, ilidaiwa kwamba Kamanda Barlow ambaye aliuawa kwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi muda mfupi baada ya kumfikisha mwalimu huyo nyumbani kwake, alivamiwa na majambazi.

  Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI, Robert Manumba alithibitisha jana kukamatwa kwa mtu huyo (jina tulihifadhi) akisema: "Ni kweli mtu mmoja amekamatwa, lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia kwa kina kuhusu suala hilo kwa sababu bado tunamhoji na tunaendelea na uchunguzi. Tutakapokamilisha, tutatoa taarifa."

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lily Matola pia alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo. Hata hivyo, alisema amesikia habari hizo kwa kuwa yuko safarini kwenda mkoani Kilimanjaro kwenye mazishi ya kamanda huyo... "Hayo nimesikia, lakini kwa sasa sipo Mwanza hivyo siwezi kuzungumzia lolote."

  Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zinaeleza kwamba upelelezi wa mauaji hayo umefanikiwa kwa hatua kubwa na kwamba mtu huyo alikamatwa Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego na makachero waliopo katika timu ya uchunguzi na alisafirishwa hadi Mwanza ambako anashikiliwa na jeshi hilo.

  Ilielezwa kuwa mtu huyo alikamatwa kutokana na kuwapo kwa taarifa za siri za kiitelejensia kutoka kwa watu mbalimbali.

  "Kuna hali imefunguka na imesaidia sana. Inaonyesha kwamba Dorothy alikuwa na uhusiano na mtu huyu ambaye alikuwa akifika nyumbani kwake, kama mumewe na watu wanajua jambo hili," alieleza mmoja wa askari polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

  Alisema kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba uamuzi wa mwalimu huyo kusitisha uhusiano wa mapenzi na mtu huyo huenda ndicho chanzo cha mauaji hayo lengo likiwa ni kumshawishi Dorothy kurejesha uhusiano.

  "Mimi natambua kwamba huyu jamaa na Dorothy walikuwa na uhusiano na inajulikana mjini kuwa hata mke wa mtuhumiwa anatambua jambo hilo kwani walishagombana siku moja mjini na hata katika msiba nyumbani kwao na mtuhumiwa," alisema mama mmoja (jina tunalo), aliyejitambulisha kama mmoja wa marafiki wa karibu wa Dorothy.

  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitangiri (jina tunalo), anasema amekuwa akimfahamu mtuhumiwa aliyekamatwa kama baba mwenye nyumba hiyo na kila mara amekuwa akimkuta hapo nyumbani wakati wa kujisomea na wanafunzi wenzake.

  "Mimi ninamfahamu kama baba wa rafiki yangu na nimewahi kumkuta wakati wa kujisomea hapo nyumbani na watoto wa nyumba hiyo."

  Dorothy ambaye ametajwa kuwa mjane, ni Mwalimu katika Shule ya Msingi Nyamagana na tangu kufariki kwa mumewe Ofisa wa zamani wa TRA, Modest Lyimo mwaka 1997.

  "Watu wote wanajua kwamba mtuhumiwa alikuwa akitembea na huyo mwalimu, wameonekana mara nyingi wakiwa muziki," alieleza mmoja wa ndugu wa karibu wa mke wa mtuhumiwa.

  Hili ni tukio la tatu mkoani Mwanza kutokea kwa ofisa wa polisi kuuawa. Katika tukio la awali lililotokea mwaka 1987, askari aliyetambulika kwa jina la Inspekta Gamba aliuawa kwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Nyakato na katika tukio la pili mwaka 1997, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Kati ASP Mahende aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la Bugando saa nne usiku alipokuwa akifuatilia majambazi waliokuwa wakijitayarisha kuvamia.

  Dar wamuaga Kamanda Barlow
  Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal aliongoza waombolezaji waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Barlow nyumbani kwake, Ukonga Dar es Salaam jana.

  Mwili wa Kamanda Barlow ambao unasafirishwa leo kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi, uliwasili nyumbani kwake saa 6.45 kabla ya kupelekwa katika Kanisa la Mtakatifu Agustino, Ukonga kwa ajili ya ibada na kutoa heshima za mwisho.

  Akitoa salamu za Serikali, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima alisema kifo cha Kamanda Barlow ni pengo kwa taifa... "Tutahakikisha watuhumiwa wanapatikana kwa mikono yote miwili na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao."

  Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema alisema juhudi za kuwasaka watuhumiwa zinaendelea kwa ushirikianao wa wananchi.

  "Kifo cha Kamanda Barlow kimeacha pengo kwani hivi sasa askari mmoja analinda watu 1,300 hivyo kwa kifo chake unaweza kuona ni pengo la aina gani na ukilinganisha yeye alikuwa kamanda wa mkoa mzima," alisema IGP Mwema.

  Alisema jeshi lake litaendelea kulinda amani ya wananchi na kifo cha Kamanda Barlow kinalifanya liongeze nguvu.

  Akitoa mahubiri, Padri Veri Urio alisema kila jambo hutokea kwa wakati na kifo cha Kamanda Barlow kimesababishwa na watu. Alisema mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa mtu ni Mungu pekee hivyo waliosababisha kifo chake siku ikifika, watajibu kwa nini walifanya hivyo.

  IGP Mstaafu, Omary Mahita alisema atamkumbuka Kamanda Barlow kwa uchapaji wake kazi tangu akiwa polisi Interpol (polisi kimataifa)alifanya kazi kwa weledi uliotukuka.

  "Daima nitamkumbuka kwani nimefanya naye kazi sehemu tofauti na askari waliobaki waige mfano wake wa uwajibikaji" alisema Mahita.

  Mbali ya Dk Bilal, viongozi wengine walioshiriki katika ibada hiyo jana ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), makamanda wa polisi, viongozi wa Serikali na vyama vya siasa na wananchi.


  Imeandikwa na Frederick Katulanda, Mwanza na Ibrahim Yamola, Dar.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Apumzike kwa amani Kamanda Barlow.
   
 3. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  kamanda si angetulia na mke wake tu,nyumba ndogo zinaponza na mwisho wake unaweza kuwa mauti,RIP kamanda ulazwe panapostahili
   
 4. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hizi kei hizi! Cjui ziliwekwa nini??? Kwa nini usikae na kei ya mkeo tuuuuuuuuuu! Nways rip kamanda!
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nayakumbuka maneno ya mwalimu wangu wa BUNILIZI EDWIN SEMZABA ALISEMA 'PENZI KITOVU CHA UZEMBE'
   
 6. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli apumzike kwa amani! Yani binadamu wengine sijui ni mijitu! mtu unamtoa uhai binadamu mwenzio kwa mwanamke ambaye pia si mali yake kihalali! jamani tunakwenda wapi!
   
 7. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  OK, kumbe ni walikuwa wanagombea mwanamke! Hebu iwekeni picha ya mwanamke huyo tuone alivyo bomba hata afande kuondoka kabisa.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahaaaaa,,,,kuna wakat ukitaka kwenda MORO SI LAZIMA UPANDE ABOOD,,,,,UNAJARIBU NA COASTER
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  cacico,
  A Jamaican Man was making love to his
  woman for the first time in his lifr. He then
  suddenly screamed and ran out of the
  room.. then came back with a glass of water,
  and poured it in the woman's vagina.
  Frightened, the woman shouted 'Wot da Hell
  Ya Do Dat Faw?' ...and the man replied,
  'Damn'it woman ... dis ting too sweet man
  ~me gwan dilute it, rememba me diabetic'
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Lord is my shepherd I shall not want. 2 in green pastures Erbdhana. To comfort Jordna water. 3 He restores my soul. He leads me in the paths of righteousness for his name's sake. 4 also if I walk through the valley of the shadow of death, I will fear no evil, for You are with me. Your rod and your staff, they comfort me. 5 resulted veterans table toward Amadaiqi. I wiped fat head. RIA Cups. 6 Surely goodness and mercy Atavanni all the days of my life and I will dwell in the house of the Lord for days.
  Psalms 23
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mdau k,kitu kingine
   
 12. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  k tamu sana,cdhani kama kuna kitu duniani kinazid k,hayo mengine ni usanii tu!!!haya bana ngoja na si tusubiri kuua kwa jins tulivyo na wachumba wazuri kupindukia!!!!!kwa nini unilie k yangu bana?pumzka ila mh!!kama mungu yupo kazi unayo!!!!!!
   
 13. a

  ablood8 Senior Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kama vile wewe ni msafi saaana?
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kamanda aliona kei ya nyumbani imechuja utamu akaamua kusaka ingine
   
 15. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kweli nkuu, kidonda ni kisu kikali. kama inzi kuwa tayari kufaia juu ya kidonda! Amaa! Amekaangiza sana nadhani huyo mama. Picha tafadhali! Walimu bwana! Ukiwachanganya na maafande ndo kabisa ni zaidi ya makande.
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Polisi mmoja analinda watu 1300??
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Ndio bongo bwana
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  labda picha ya KOJOLEO,hapo ndo inahitajika
   
 19. m

  mamajack JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  eti hawataki kusema ukweli.wanatudanganya"alimsindikiza dada yake walikuwa kwenye kikao cha harusi"jamani lini tutakuwa wakweli,na walidhani isingejulikana kwamba alikuwa na kimada.pols nyie,acheni wake za watu,halafu acheni ubabe maana polis huwa wanajiona wanahaki kwa kila kitu,hata kwa wale za watu.mke unae umempaki dar baada ya kumzeesha,ticha noma.
   
 20. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Yessss, leteni nayo kama ipo. Huo ndio uchunguzi makini unaohitajika. Tutajua kwa nini ntu kakubali kufa bila masikhara. Imekaaje? Ni vizuri ikiwa active.
   
Loading...