Think2
JF-Expert Member
- Jan 3, 2025
- 2,204
- 3,983
Kuna kiongozi mmoja wa Simba alimtisha kocha Fadlu Davids kuwa watamfukuza kazi kama Simba itakosa ushindi kwenye Mchezo wowote ule Ujao na kama timu haitocheza vizuri ndani ya mechi mbili zijazo.
Hili lilimfanya kocha huyo kuhisi kuwa kazi yake HAIKO SALAMA na kuhisi kuwa anafanya kazi na kiongozi ambaye hayuko professional . Alisikitika pia kwani alimuona kiongozi huyo sio mtu wa mpira kwani kauli zake hizo zilionesha kutokufahamu kuwa kocha kufungwa kufungwa mara nne mfululizo na timu flani sio jambo la ajabu katika soka (Fadlu alipoteza michezo minne mfululizo aliyocheza na Yanga) na kiongozi huyo hakuelewa kwamba Timu Kuanza mechi ya kwanza ya msimu kwa taratibu na tempo ya Chini ni jambo la kawaida sana katika soka.
Fadlu Davids alifanya Maamuzi ya Kuondoka Simba baada ya mazungumzo na kiongozi huyo na akamfahamisha Mo Dewji ambaye alimsihi sana asiondoke .Mo Dewji alimpa ofa ya kumuongezea mshahara Fadlu Davids lakini alikataa .
Soma Pia: Klabu ya Simba Sc yathibitisha kuachana na kocha wake mkuu Fadlu Davis Kwa matakwa yake Binafsi
Ni kama mambo yalifuatana kwani punde tu baada ya Fadlu kumaliza mazungumzo na kiongozi huyo wa Simba ,simu ya maboss zake Fadlu wa Zamani,Raja Cassablanca iliita ,walimuulizia uwezekano wa yeye kurudi Raja kama kocha Mkuu huku wakimpa mshahara mnono zaidi ya ule anaoupokea akiwa Simba ,pamoja na bonasi kibao pindi akiwapa Mafanikio miamba hao wa Afrika na Fadlu hakuwaza sana haswa Baada ya kukorofishana na kiongozi huyo na akawakubalia Raja bila wasiwasi.
Fadlu na Simba waliagana siku moja Kabla ya mchezo dhidi ya Gaborone United na walikubaliana kuwa kocha atasimamia mchezo huo na baada ya mchezo huo yeye pamoja na wasaidizi wake hawatarudi Dar Bali watabaki Afrika Kusini na Kuanza safari Kwenda Cassablanca.
Isingekuwa rahisi kwa Fadlu Kuondoka Simba eti kwa Sababu Raja Casablanca wamekuja kwake na Fedha kubwa hapana,Fadlu alipewa project ya Simba ya miaka miwili ama mitatu ijayo na Mo Dewji..Usajili uliofanyika dirisha lililopita aliusimamia yeye,Neo Maema ,De Reuck ,Sowah ,Antony Mligo ,Naby Camara ,wote hao wamekuja kwa mapendekezo ya yeye Fadlu Davids .Maema na De REUCK ni yeye aliwapigia simu waje Kusaini Simba Kwahyo Alikuwa na matumaini ya kuijenga timu tishio