Habari za mida hii ndugu jamaa na marafiki wa jamii forum:
Naomba ushauri wenu wa kufanya baada ya kuguswa na haya yaliyonikumba,
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 nilitokea kupendana na kijana mmoja wakati niko nasoma chuo,alinieleza ana mtoto mmoja yuko vijijini kwa wazazi wake na ndiko anakolelewa huko,nilimuuliza kuhusu mwanamke aliyezaa naye akanieleza kuwa hawana mahusiano yaani walishatengana muda mrefu sasa,kwa sababu nilimpenda sana sikuona mbaya niliona yule mtoto hana sababu ya kunifanya nisiendelee kumpenda huyo kijana kwa bahati nzuri nikabahatika kupata mtoto naye mmoja,baada ya kumaliza chuo akaniambia twende tukaishi kwao,sikuwa na namna ya kukataa ukizingatia nishamfahamisha kwetu na tuna mtoto.
huwezi amini niliyoyakuta huko,hapo nyumbani kama ilivyo kawaida ya jamii za kiafrika huwezi ishi wewe na mume wako tu lazima mtakuwa familiya kubwa basi nilikuta watoto kama wawili na mama mkwe. siku moja mtoto mkubwa katika kupiga story alijikuta akiniambia kwamba yeye ndiye mtoto wa kwanza wa huyu mwanaume niliyenaye na yuko chuo,wa pili yuko form 2,wa tatu yuko la 5 na wa nne yuko nasari.mh! kweli sikuamini niliumia sana mpaka yule mtoto alijuta kwa nini aliniambia, alifahamu kuwa nafahamu.Mume wangu alivyorudi nilimuuliza alikiri lakini alistuka nimejuaje nilimtuhumu kwa nini alinidanganya,aliomba msamaha sana sana.
Sasa naomba ushauri kutoka kwenu NIFANYEJE?