Mtayarishaji
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 291
- 198
Siku moja nikiwa nimekolea ktk action iliyokuwa inaendelea ya makala kuhusu Tai Chi mlio wa msg ukasikika ktk simu yangu. Nikaichukua na kufungua, kucheki ujumbe ukasomeka; Helo mambo umeshapata mchumba? Wachuchu tupo.
Nikashangaa!
Huyu ni nani? Nikareply kwa kumuuliza.
Akajitaja jina akaeleza ni vipi amepata namba yangu. Wakati huo mimi nipo Sirari na yeye akasema anasoma Chuo cha kumbukumbu ya MwL Nyerere kilichopo Dar na akasema mwaka huu mwezi huu huu wa saba anamaliza digrii yake ya masuala ya Jinsia. Basi mawasiliano yakaanzia hapo akanitumia picha za sura yake mambo yakawa ni moto tukijengeana mazingira kuwa tutaoana.
Alinisumbua sana kwa kuniweka busy. Mwezi mmoja ulipokatika tangu tuanze kuwasiliana nikaanza kumtilia mashaka. Maana ilikuwa ni kutwa nzima kuwasiliana hadi usiku, nikawa najiuliza class huingia saa ngapi sipati jibu. Ila kwa vile nilikuwa ktk mishe zangu za Fisibility study ya kuanzisha radio station kanda ya ziwa na baadae Magharibi nikasema nikirudi Dar nitafahamu mengi maana itakuwa rahisi kumfuatilia.
Siku moja nikaenda Kigoma, huko niliishi wiki tatu, nikatembelea kiwanda cha kutengeneza chumvi Uvinza, nikavuka mto Malagarasi na kuingia Burundi kupitia huo mto. Pamoja na mizunguko yote niliyoifanya kuna wakati sikupata muda wa kuwasiliana naye mara kwa mara kama alivyopenda. Nikiwa hukohuko Kigoma akaanza kulalamika na kudai kwamba simjali hivyo kuna uwezekano akasitisha mahusiano na mimi. Nikakumbuka yale mashaka niliyokuwa namtilia yanaanza kujiumba. Tulifika mbali maana ndugu zake hasa Dada,Mama walisikia habari zangu na kwa upande wangu vivyo hivyo alifahamika bado tu kujitokeza mubashara ndio ilikuwa bado.
Nifupishe kwa kusema kwamba, hadi naondoka Kigoma huyo binti aliniambia tusiwe wachumba wala kusiwe na mahusiano zaidi ya urafiki tu wa kawaida. Katika hiyo miezi mitatu ambayo tumefahamiana kwa kuwasiliana na kuonana kupitia teknolojia kuna mengi tulipanga ya kimaisha.
Wakati sasa ninakaribia na nipo najiandaa kurudi Dar ni wiki sasa tangu aamue na akaniambia kuhusu kusitisha kila kitu. Hakuna cha urafiki, mawasiliano wala nini na ndio tume end up kiivyo yani.
Bado ninajiuliza amekumbwa na nini!?
Maana hata nikiamua kuwasiliana nae naambulia matusi. Nimeamua kunyamaza tulii nikomae na yale nilikuwa na study maana naamini mwishowe nitakuja kuwa miongoni mwa wa miliki wa Radio Station Tanzania.