Kilichomponza Tundu Lissu ni maneno haya aliyoandika JamiiForums...

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,202
Huu ni mtazamo wangu...
Kilichomponza Tundu Lissu ni Jamii Forums na nguvu kubwa ya maoni ya wachangiaji wake.

Tutake tusitake Jamii Forums imekuwa ni chanzo muhimu cha ku "influence" mawazo ya wengi Tanzania, hususan wanasiasa. Ukiwasikiliza wana siasa wanapotaja "mitandao ya kijamii" (hata wakizuga kwa kutaja mingine kwa majina na kuiacha JF) wana JF tunaelewa hilo linatoka JF. Na hata wasipotaja mitandao ya kijamii tunaelewa kabisa wanayoyapata humu. Licha ya wanasiasa, waandishi wa habari wengi tumewaona wakiandika habari ambazo wazi tunafahamu zinatokea JF.

Mwaka 2014 Ng'wamapalala alileta uzi kwa aliyoyasema Tundu Lissu bungeni: Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu! - JamiiForums

Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl. Nyerere. Tundu Lissu amepasua jipu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum.

Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya haramu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, ?Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'.

Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana.

Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.

Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.

Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).

Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.

Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.

Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadhalilisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.

Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.

Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uhalali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.

Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.

Aliyoyasema Tundu Lissu kuhusu marehemu mzee Nyerere ni "taboo" kwa Tanzania.

Post ya pili tu ya uzi huo, The Boss akatahadharisha kuhusu kauli za Tundu Lissu:

Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

Katika uzi huo chadema wote kama walipigwa bumbuazi Ritz akaliona hilo:

Tundu Lissu, kwenye ili la kumponda Nyerere, pro-Chadema wapo kimya masikini.

Wengine wakashindwa kabisa kutia lao, almaaruf Bujibuji akajisemea kweli yake:

No comment

Binafsi nilichangia kwenye uzi huo. Siyo muhimu kuyaleta hapa kwa sasa. Lakini nnaamini, kama ilivyo kwa wanasiasa wote kuwa ni ma "opportunist" huja JF na kusoma nini jamii inasema na kuchukua wanayoona na kuyatumia kwenye siasa zao. Lissu ni mmoja wao. Ni "opportunist" aliyetumia mawazo ya kinadharia ya wachangiaji wa JF na biila kufikiri gharama (cost) zake akayapeleka bungeni na kuyajengea hoja.

Je, kinachomgharimu Tundu Lissu ndicho hicho? Kama sicho, kwanini?
 
Last edited:
Nafahamu, kigugumizi kinachowapata kwenye uzi huu ni kama kigugumizi kilichowapata kwenye uzi niliounukuu post namba moja.

Tunashindwa kusema ingawa Tundu Lissu tunampenda lakini hakupaswa kumsema Marehemu Mzee Nyerere au tunashindwa pia kusema Tundu Lissu hicho sicho kinachomgharimu kwa kuwa alisema ukweli!

Tunaweza kutafuta mchawi kumbe wachawi tupo JF.
 
Nafahamu, kigugumizi kinachowapata kwenye uzi huu ni kama kigugumizi kilichowapata kwenye uzi niliounukuu post namba moja.

Tunashindwa kusema ingawa Tundu Lissu tunampenda lakini hakupaswa kumsema Marehemu Mzee Nyerere au tunashindwa pia kusema Tundu Lissu hicho sivyo kinachomgharimu kwa kuwa alisema ukweli!

Tunaweza kutafuta mchawi kumbe wachawi tupo JF.
Hilo na kwako pia, mara nyingi maovu yakifanywa na mtu/watu wa imani yako huwa mzito kukosoa zaidi ya kujenga hoja kupia imani yake.

Afadhali siku hizi kwenye maswala ya kisiasa umekuwa ukikosoa chama chako mara moja moja ila hukuwahi kufanya hivyo wakati wa kipenzi chako Kikwete.

Na hizo sababu ndio zinazofanya umwite Mzee Nyerere badala ya Baba wa Taifa.!
 
Huu ni mtazamo wangu...
Kilichomponza Tundu Lissu ni Jamii Forums na nguvu kubwa ya maoni ya wachangiaji wake.

Tutake tusitake Jamii Forums imekuwa ni chanzo muhimu cha ku "influence" mawazo ya wengi Tanzania, hususan wanasiasa. Ukiwasikiliza wana siasa wanapotaja "mitandao ya kijamii" (hata wakizuga kwa kutaja mingine kwa majina na kuiacha JF) wana JF tunaelewa hilo linatoka JF. Na hata wasipotaja mitandao ya kijamii tunaelewa kabisa wanayoyapata humu. Licha ya wanasiasa, waandishi wa habari wengi tumewaona wakiandika habari ambazo wazi tunafahamu zinatokea JF.

Mwaka 2014 Ng'wamapalala alileta uzi kwa aliyoyasema Tundu Lissu bungeni: Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu! - JamiiForums

Aliyoyasema Tundu Lissu kuhusu marehemu mzee Nyerere ni "taboo" kwa Tanzania.

Post ya pili tu ya uzi huo, The Boss akatahadharisha kuhusu kauli za Tundu Lissu:

Katika uzi huo chadema wote kama walipigwa bumbuazi Ritz akaliona hilo:

Wengine wakashindwa bisa kutia lao, almaaruf Bujibuji akajisemea kweli yake:

Binafsi nilichangia kwenye uzi huo. Siyo muhimu kuyaleta hapa kwa sasa. Lakini nnaamini, kama ilivyo kwa wanasiasa wote kuwa ni ma "opportunist" huja JF na kusoma nini jamii inasema na kuchukua wanayoona na kuyatumia kwenye siasa zao. Lissu ni mmoja wao. Ni "opportunist" aliyetumia mawazo ya kinadharia ya wachangiaji wa JF na biila kufikiri gharama (cost) zake akayapeleka bungeni na kuyajengea hoja.

Je, kinachomgharimu Tundu Lissu ndicho hicho? Kama sicho, kwanini?
Haka kadeeemu bwana
 
Back
Top Bottom