Kilichomponza mdogo wa Askofu Pengo hadi mauti

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,397
Yaweza ikawa ni chanzo kweli cha kifo chake ama isiwe.Wakristo huamini katika Kristo daima.

Yupo mdogo wa askofu Pengo aliyebahatika kusoma masomo ya uchumi na akabobea.Alifanya kazi kwa weledi mkuu.

Katika kazi yake aliwahi kufanikiwa kupata pesa nyingi kiasi kwamba huyo mchumi alijiona yeye ndiye kila kitu. Wakati huo huo kila mali aliyonunua ilikuwa desturi yake kuipeleka kwa kaka yake huyu askofu Pengo ipate baraka.

Basi huyu msomi alinunua gari ya kifahari ya zaidi ya milioni 60 ambapo kwa wakati huo ni wachache Tz walikuwa nayo.

Alipofika kwa kaka yake huyu askofu inadaiwa alimwambia maneno ya kuudhi kuwa, wewe umezoea kupata hela za mteremko kutoka kwa wazungu bila kuumiza vichwa, angalia mimi(huku akigonga kichwa chake) nimenunua gari kali nimeileta uibariki.

Maneno hayo aliyoyasikia Pengo kutoka kwa mdogo wake hakusema kitu zaidi bali alimwambia hiyo gari yako siwezi kuibariki. Alipokataa kuibariki hiyo gari mdogo wake akapanda akaondoka kwa mbwembwe.

Miezi michache yule mdogo wake akagonga nguzo na kufa hapo hapo.Ndugu walimulaumu Pengo kuwa hakumsamehe mdogo wake kwa kauli hiyo chafu kwake.

Hata msibani aligoma kwenda sijui ni majukumu ya kitawa au vipi.
 
Mbona mengine tunayajadili hampanic kiasi hiki.Kuna kosa gani jenga hoja bwana ulweso.
Unajua kuna vitu vingine vyawatu huwezi jua undani unaweza sutwa huwezi jua labda aliulizwa hizo hela umetowa wapi akajibu vya kujibu, na kiongozi hawezi bariki kama kuna kitu kisicho sawa, mpe heshima basi bishop wako, tutenzi wikolo
 
Unajua wafipa huwaga ni waongo waongo mno nyie na mnazusha na ku-exaggerate mambo mengi mno ya kijinga na ndio hasa chanzo cha mji wenu Sumbawanga kuogopwa na kuchelewa sana kuanza kupiga hatua japo ulikuwa na kila sababu za kufanya hivyo mapema.
 
Tunatakiwa tujifunze nini toka kwenye hili? Kuwa sio vizuri kununua magar ya bei mbaya
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom