Kilichoisambaratisha NCCR-Mageuzi ile ya 1995 ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichoisambaratisha NCCR-Mageuzi ile ya 1995 ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Naipendatz, Sep 1, 2011.

 1. N

  Naipendatz JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 917
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 80
  Wazee kwa wale waliokuwa wafuatiliaji wa siasa zetu kipindi cha between 95 to 2000 naomba mnisaidie kwa hili! Ni sababu zipi zilisababisha kuanguka kwa lile chama ambalo lilikuwa tishio hadi kwa mkuu Nyerere? Is it unafiki? ulafi wa madaraka? uroho wa fedha? ukabila? ukanda? uzushi?......?

  pls wazee naomba mnisaidia all the details and stories behind anguko la nccr ya enzi hizo?

  CAN HISTORY REPEAT ITSELF TO CHADEMA?

  TOFAUTI KUBWA NI NINI KATI YA CHADEMA YA SASA NA THAT NCCR???
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,088
  Trophy Points: 280
  Umetumwa lakini tutakusaidia usiwe na wasi

  Kwanza hapakuwepo na matatizo makubwa sana ya kuwafanya watu waichukie ccm kama ilivyo sasa,pesa ilikuwa na thamani na ufisadi haukuwa mkubwa kama sahivi

  Pili elimu ilikuwa bado ndogo kwa wananchi hvyo walikuwa hawana uwezo mkubwa wa kuchambua mambo tofauti na sasa wasomi ni wengi karibu kila familia kuna mtu kapita ama anasoma sec n,k

  Tatu kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari kumewafanya wananchi kuelewa mambo mengi waliyokuwa hawayajuhi yaliyokuwa yakiwafanya kuwa maskini k.v. rushwa,dili feki,ufisadi,kuuzwa kwa nchi yao n.k

  Nategemea wenzangu wataelezea na mapungufu mengi ya nccr na kufa kwake
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania walikuwa waoga wakati huo,sasa sivyo.Mabadiliko ya Kisiasa duniani ni tofauti kwa sasa na wakati huo.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,383
  Likes Received: 22,257
  Trophy Points: 280
  Mrema pandikizi la magamba
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Sep 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mwaka 1995 Watanzania walikuwa na hamasa kubwa sana ila tu tatizo ilikuwa ni kwamba walikuwa wakimpenda mtu na si sera. Watanzania walimpenda Mrema. Nakumbuka siku alipojiunga na NCCR mageuzi mtaa wa Aggrey siku hiyo kadi za NCCR ziliuzwa kama karanga.

  Vyombo vya habari hasa magazeti yalikuwepo mengi tu: Tazama, Motomoto, Majira, Cheche, n.k. Kuhusu suala la elimu ni kweli walikuwepo wachache ukilinganisha na sasa.

  Watu wanasema Marando alichangia anguko kubwa la NCCR baada ya varangati kule Tanga na Mrema kutupwa nje kupitia dirishani. Ila mimi naamini NCCR ilikufa kwa sababu ya kugombea Ruzuku. Ruzuku kwenye Chama ni sumu kubwa na inawagombanisha watu.

  Nakumbuka wakati huo NCCR kulikuwa na watu kama Anthony Komu (yupo CDM kwa sasa) na Mabere Marando na hawa walikuwa na nafasi yao kubwa tu katika kuanguka kwa NCCR Mageuzi.

  Mkuu CHADEMA pia kuna fukuto kuhusu Ruzuku: Wangwe (mwenyezi mungu amrehemu) aliipigia kelele kwamba iende kuimarisha Chama mikoani badala ya kubaki makao makuu na kulipana madeni ya helcopita; bahati mbaya hatunaye. Kuna mambo yanenda chinichini kwamba ruzuku inaliwa na wakubwa kwa njia ya posho. Wakubwa wanalipwa posho kubwa wakati wakitekeleza majukumu ya chama lakini wa chini wanatakiwa wajitolee!!

  Watu wameichoka CCM lakini CHADEMA wasipoangalia masuala ya posho na ruzuku yatawafarakanisha.
   
 6. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #6
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Labda ukisoma kitabu cha Ndimala Tegambwage, cha Mtafaruku na Hatima ya Mageuzi Tanzania utafahamu kwa undani zaidi. Pamoja na hayo yote, nikuhakikishie NCCR-Mageuzi itaendelea kuwepo.
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  George weka hicho kitabu hapa kama unacho!
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  NCCR imesambaratika lini wewe au unaharisha maneno! NCCR ipo labda CCJ ndio imesambaratika.
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Wangwe Bangi zilikuwa zinamsumbua na alidanganywa na UWT kupitia wastaafu wa Jeshi kutoka Tarime kuikengeuka CDM. Baada wao kuona wamemshirikisha mambo mengi ambayo yote hayakuzaa matunda walikuwa hawana jinsi maana siri zao bado walitaka ziendelee kuwa siri.
   
 10. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #10
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Samahani mkuu, sina softcopy, kama uko Tanzania fika makao makuu NCCR- Mageuzi Ilala. Omba hicho kitabu watakupatia.
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  A.l MREMA
   
 12. e

  ebrah JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  walifitiniwa, na kwa cdm nawasihi wawe makini na wanachama wahamiaji toka ccm!
   
 13. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Asante mkuu kwa maelezo yako
   
 14. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwani NCCR imesambaratika? Mbona ina wabunge bungeni, au maana ya kusambaratika ni nini?
   
 15. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Mkuu mi naona neno kusambaratika limekuwa gumu kuelewa, jamaa ametumia kusambaratika akimaanisha kukosa nguvu kama awali na sio kufa kama chama cha ccj
   
 16. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba NCCR ilianzishwa na maofisa wa usalama ili ku-contain opposition, na kuchafua image yote ya upinzani. Baadaye ikajulikana kuwa wananchi wenye nia ya mageuzi wanaburuzwa na wahuni wanaojidai wanamageuzi. kwa sasa inaonekana kuwa baada ya kumaliza kazi yao NCCR wameanza kuingia CHADEMA, the fact is NCCR imekufa, kilichopo ni kuwa ipo kwenye makaratasi na kuthibitisha uwepo hewa wake kwa wabunge wawili watatu iliyo nao.
   
 17. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,802
  Trophy Points: 280
  Mmmh!!!
   
 18. LuCKNOVICH

  LuCKNOVICH Senior Member

  #18
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tuwekee soft copy please,if possible
   
 19. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  watu ambao awaaminiki ni marando huyu ni kama mbegu ya gamba lakini viongozi wa cdm ni makini akistukiwa wakwanza kujitoa nae muhanga ni yeye
   
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kuna kosa kubwa sana la kimkakati ambalo vyama vyetu vimekuwa vikilifanya kila siku. Utakuta ma-opportunist kama huyu Komu kila wanapokwenda wanapewa nafasi za haja, hivi hakuna wanachama waaminifu wakuweza kushika nafasi hizo kuliko hawa wapima upepo? Hata hivyo kilichoiua NCCR ni ile tabia ya Mrema kuamini kwamba yeye ndiye alikuwa kila kitu. Hata hiyo ruzuku alitaka yote iwe mikononi mwake kwa kuamini kuwa ilipatikana kwa ubavu wake. Kumbuka kauli yake wakati akienda TLP kuwa alikuwa na mtaji (wanachama wa kuhama nao). Leo hii yuko wapi na mtaji wake huo? Hili laweza kuwa funzo kwa makamanda wetu wa leo.
   
Loading...