Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,662
Hii ni makala inayoongelea kisa kimoja cha kutisha na kusisimua sana kilichowakumba familia ya PERRON nchini MAREKANI katika himaya yake ya KISIWA CHA RHODE ambako ndani yake ndo kuna kijiji cha HARRISVILLE walikokuwa wakiishi familia hii.
HARRISVILLE ni kijiji kidogo ila chenye historia kubwa na kinaitwa kijiji cha historia kutokana na mambo ya zamani yaliyotokea katika kijiji hicho hasa mambo ya kichawi na kishetani.
Sasa katika kijiji hicho kulikuwa na nyumba moja kubwa yenye vyumba kumi na familia hii wakaipenda nyumba hiyo na kuamua kuinunua ili yawe makazi yao bila kujua walikuwa wamejiingiza ndani ya tanuru la meteso.
Kabla hawajakabidhiwa nyumba hii na mmiliki aliyekuwemo aliwaambia kuwa nyakati za usiku msiwe mnazima taa yani ni kulala na taa maisha yao yote ila wakapuuzia hilo sharti labda kwasababu walikuwa ni wageni katika hicho kijiji cha historia chenye watu wachache, elfu moja.
Huko wanaishi wazawa wenyewe wageni wengi wanapashindwa na kukimbia na familia ya PERRON walikuwa ni wageni, sasa wakawa wamevunja sharti la kuzima taa usiku na kilichowakuta hawawezi kusahau maisha yao yote.
Hilo sharti lilikuwa na maana yake kwani kuna historia ya zamani sana ya miaka ya 1800’s kwa mmiliki wa kwanza wa nyumba hiyo ambaye alikuwa ni mbibi fulani na wanakijiji wa HARRISVILLE wanajua historia hiyo ila wanakaa kimya ili ujifunze kitu kizuri.
Toka miaka ya 1800’s baada ya mbibi kufa kifo cha utata kukutwa amejitundika kweye kamba ndo nyumba ilibadilika kuwa ya kishetani yenye kuwinda roho za watu na imeondoka na watu wengi maana hapo unakuwa kama unafufua mizimu nyumba inatingishika hatoki mtu haingii mtu na ina eneo kubwa limezungukwa na shamba.
Sasa ndugu zetu familia ya PERRON ndo wakawa wameingia humo ndani na ina filamu yake imeuza sana ila kisa chake kinatisha zaidi ndo maana wanataka kuandaa filamu nyingine ili ibebe uhusika zaidi wa kisa na ndani ya makala tutaona historia nzima toka mbibi akiwepo mpaka misukosuko watakayokutana nayo familia ya PERRON.