Kilichofanyika jana hapa dodoma ni uhuni mtupu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichofanyika jana hapa dodoma ni uhuni mtupu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Smallnick, Apr 8, 2011.

 1. S

  Smallnick Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jana wananchi wengi wa dodoma tuliokusanyika nje ya ukumbi wa bunge tukisubiri kuingia ndani ya mjengo kutoa madukuduku yetu juu ya mswada wa kuunda katiba mpya ambao kimsingi unanuka madudu tupu. tuliambulia kupigwa mabomu ya machozi na kukimbizwa kana kwamba sisi ni wageni na sio watanzania..... IMENIUMA SANA
   
 2. B

  Batale JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,070
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Heri yenu nyie Watanzania mlioletewa hiyo rasimu ya katiba japokuwa pia hamkupewa fursa ya kuijadili, lakini cha kustaajabisha serkali imeona Tanzania inaundwa na mikoa mitatu tu, Dar es salaam, Dodoma na Zanzibar kama sehemu ya muungano, sasa cha kuuliza mikoa mingine si Tanzania? je nako kutakuwa na rasimu zingine?. Hakika mwachezea taifa hili.
   
 3. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  mi sioni haja ya hiyo katiba mpya kwa sasa tungejikita kwenye uchumi zaidi ingekuwa maana uchumi wetu uko hoi serikali ingeelekeza nguvu zaidi huko kuliko kwenye katiba ya nini kuwa na katiba mpya ili hali watu ni masikini je katiba mpya itaongeza pato kwa wananchi,na je baada ya kupata katiba mpya uchumi wetu utapaa na je hela ya kufanikisha mchakato wa kupata katiba mpya itatoka wapi na je kama ingetumika kwenye ishu nyingine kungepatikana manufaa yapi wote wanaolaumu katiba siwaelewi kabisa na ndo maana wananchi wengi hawana hata wanalojua kuhusu katiba watu wanahitaji maisha mazuri na si katiba hivi itakuwaje tukijisifia kuwa na katiba mpya wakati watu hawawezi kupata chakula!!!! Tafakari
   
 4. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mkuu mawazo mazuri ila ukumbuke bila katiba,bila utawala bora,bila utaratibu,uyasemayo yatakuwa ni ngonjera! Tungekuwa na katiba wajibisha taifa lingekuwa mbali mkuu!
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Chijana nadhani unahitaji kurudia somo la Uraia darasa la Sita...sina uhakika sana na elimu yako na hata kama ni graduate kwa ngazi yoyote ushauri wangu kwako ni uchukue vitabu vya uraia shule ya msingi usome juu ya katiba (kama itakuwa bado havijachakachuliwa bado)

  Unashindwa hata kuelewa uhusiano uliopo kati ya Katiba na ukuaji wa Uchumi? Au unafikiri uchumi unashuka tu bila kuwa na miongozo sahihi na vitu vya kufanya?

  Everything fall in the hand of a leader, na unahitaji kuwa na miongozo na sheria za kusimamia viongozi katika kufanya mambo sahili ikiwamo kusimamia ukuaji wa uchumi jambo mambo ambayo huzaliwa kutoka kwenye katiba...Ndiyo maana inaitwa Sheria mama
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  sina rekodi kama dodoma waliwahi kuchagua mbunge au diwani ambaye si wa CCM (forgive me if I am wrong) sasa mlikwenda kuipinga? ninyi si wa ccm na kila anayepinga huo mswada anaonekana ni wa upinzani?
   
 7. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mdau, Katiba na maishA ya mwananchi ni pete na kidole. huwez kutenganisha hivi vitu, yapasa uelewe hili.

  Nchi ikiwa na katiba mbovu hata maisha ya wananchi yatakuwa mabovu, kwa sababu kutakuwa hakuna uhuru halisi,hakuna control ya rasilimali za nchi,hakuna mgawanyo mzuri wa madaraka kwa manufaa ya Taifa, kutakuwa na udikteta,ufisadi na mambo mengine mengi yanayoendana na hayo.
  Hawezi ukaongelea kuinua maisha ya mwananchi bila kugusa katiba ya nchi, utakuwa utwanga maji kwenye kinu tu! kama katiba ni mbovu maisha bora kuja ni ndoto za mchana.

  Kwa mfano mdau hebu tafakari; Katiba ikisema wazi kuwa;

  1. kima cha chini cha mshahala lazima kiendanae na ghalama za bidhaa muhimu ili kila mfanyakazi awe na uhakika wa kupata bidhaa muhimu. Hapa wananchi wangapi watapona na ughali wa maisha?

  2. Mkataba wowote unaogusa maslahi ya Taifa lazima ujadiliwe kwanza bungeni au balaza la mawaziri. Hapa tutaokoa mabilioni mangapi tunayopeteza kwa ufisadi na kutupa maisha magumu. Haya mabilion yanayopotea yangejenga hosp ngapi?shule ngapi? barabara ngapi? Biala shaka tungepunguza umaskini kwa kutumia rasimali zetu kwa kiasi kikubwa sana. Tofauti na ilivyo sana, wachache tu ndo wanazifaid kwa mikataba mibovu inayolelewa na katiba mbovu.

  3. Katiba ikonyesha mwongozo wa jinsi ya kuchagua mawaziri,wakuu wa mikoa,wakuu wa milaya na kuweka mipaka ya idadi yao.
  Hapa tutakuwa tumeepusha kwa kiasi kikubwa cha viongozi wa kujana na kulipana fadhila, tukawa na wafanisi watako control mahitaj ya wananchi ikwepo kupanda kwa bei za bidhaa,mafuta,kodi za kinyonyi nk nk.

  4. katiba ikiweka wazi utaratibu wa kucontrol mfumuko wa bei, na vyombo huisika na kuvipa nguvu vyombo hivyo bila kuingiliwa na Rais na vikifuata sheria,na wanachi wakiwa waamuz wakuu ktk vyombo hvyo. Hii itaondoa kupandishwa kwa bei kienyeji kwa maslahi ya chama tawala,au kikundi kidogo.

  Hiyo ni mifano michache tu mdau, kuonyesha uhusiano wa katiba na maisha ya mwanachi. TAFAKARI
   
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Siku nyingine nendeni mkiwa full ngwamba, Helmet au sufuria kichwani weka, Dasani maji kubwa mbili, mfuko wa mchanga ukiwa na kipande cha bati kifuani kwa mbele,Mkia wa taa ndani ya shati, chini weka ndula inayoendana na wakati, mwilini mjipake mafuta mgando kuzuia mawashawasha yao halafu pigeni hodiiiiiii nyumba hii...nahisi mtaruhusiwa tu,
   
Loading...