Kilicho kusibu ....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilicho kusibu .......

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Cyclone, Nov 26, 2011.

?

Unadhani kwa mkasa huu tunahaja ya kuwa makini na kutafakari upya nyendo zetu?

 1. Ndiyo

  100.0%
 2. Sina uhakika

  0 vote(s)
  0.0%
 3. Hapana

  0 vote(s)
  0.0%
 4. Sijui

  0 vote(s)
  0.0%
 1. Cyclone

  Cyclone Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimatumaini yangu makubwa mwana JF unaendelea vizuri, kwani bila hivyo usinge upata wasaa wa kuipitia thread hii kama ifuatavyo:-

  Umekutana na huyu mpenzi mpya kwa mara ya kwanza kabisa mko hotelini au nyumbani kwake,baada ya muda mfupi sana chini ya nusu saa tokea umeingia humo ndani unatamani kutafuta sehemu ya kutokea na unafanikiwa kuondoka kwa kuaga au bila kuaga .

  Nini kitakuwa kimekufanya umkimbie huyu mtu? Mkiwa ndani hukutishiwa maisha hata chembe, kwanza huyu mtu alikukaribisha kwa ukarimu wote, kama wewe ni mwanaume basi huyu mwanamke kwa kuondolea uchovu alikufanyia massage ya nguvu sana kukufanya mzee urelax na kwa mwanamke pia jamaa alifanya ukarimu unao stahili na uka feel kufurahishwa na huo ukarimu.

  HAPA SASA
  Gafla unagundua kitu ambacho kinakufanya ukose amani, huonekani kuhamaki ili mwenzio asikustukie, kwani yeye hakudhania kabisa unaweza kushtushwa na ulicho kigundua, unawaza jinsi ya kuondoka, mnaweza hata kuwa mmeanza kuninihii huku akili haipo kabisa unataka nafasi ya kuondoka tu,Kama unamoyo mgumu unaweza ukaaga gafla kwamba mimi ninaondoka nitakutafuta wakati mwingine ,kwa kuwa mwenzio hakutarajia uondoke mapema hivyo anaanza kukuuliza uko sawa lakini mbona hivyo, wewe unasema niko safi kabisa wala usijali ok, ok mzee unaondoka, ukifika nje unashukuru kuwa umetoka salama na kule ndani hauko tayari kurudi tena hata kwa risasi ya chuma.kama roho yako ninyepesi sana lazima utakuwa umekimbia bila kuaga na viatu mkononi , japo huko ndani huku lazimishwa kufanya chochote kile kibaya kwako, basi tu kwa ulicho kigundua ni lazima uondoke.

  SWALI
  Baada ya kuwa uko sehemu yeyote ambayo ni salama kwako labda nyumbani, au hotelini kwako n.k, unaapa kuwa hautarudia na umejifunza.Maswali ni kama ifuatavyo?
  1.Unadhani kule ndani uligundua nini?
  2.Unaapa kuwa hautorudia kufanya nini?
  3.Unadhani utakuwa umejifunza nini kutokana na mkasa mzima huu toka mlivyo anza mawasiliano hadi leo ulivyo mkimbia?

  MLIKUTANA HIVI
  1.Kwenye mtandao , chit chat zakutosha , mlitumiana picha zenu n.k
  2.Wazee wakusafiri umenda sehemu yeyote ugenini hapa nyumbani au nje ya nchi, labda ulimuanza au yeye alikuanza.
  3.Mmekutana kokote club mkabadilisha number then mkakutana
  4.Mmekutana katika njia yeyote ya usafiri, Meli , Bus, Daladala, Ndege, n.k
  5.Mmekuta kwenye lift, Bank au sehem nyingine yeyote

  Au mkekutana vyovyote vile, ila tu haukupata nafasi ya kuchunguza,kwani kile kilicho kukimbiza ungekigundua mapema usingeendeleza mawasiliano.

  KWANINI HUKUMCHUNGUNGUZA?
  Wewe ni mgeni kabisa uko nchi au sehem za watu,au haukutaka kumuuliza mtu yeyote yaani uliamua kufanya siri au uliuliza hakuna mtu aliye fahamu kuhusu hicho kitu kilicho kukimbiza.

  Ninaomba tusaidiane mawazo kujibu maswali ya hapo juu, hatakama wewe siyo mtu wa kukutana na mtu usiye mjua vizuri kabisa, Jiweke kwenye hiyo nafasi na uchangie tafadhari
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  I hate guessing games. . . .

  Kwanini we usiseme kilichogundulika sisi tuchangie uzito wake?Maana siwezi jua madhara ya kitu na kukubali kwamba au kukataa kwamba uangalifu zaidi ulihitajika bila kujua unachoongelea. . . ana miguu mitatu?Ni jini?Kaweka cheti cha +HIV kwenye fremu?Anatembea na hirizi?Dawa za kuongeza nguvu mwilini?
   
 3. Cyclone

  Cyclone Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Lengo siyo kilicho gundulika, bali ni kitu gani kinaweza kupelekea kilicho tokea, umejibu vizuri lakini , kuwa hizo hapo ni miuongoni mwa sababu zitakazo mfanya mtu asepe

  It`s not a guessing game though, It`s all about open ended opinions
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  kwa mfano, kwenye picha walizotumiana alikuwa ni msichana mrembo sana, lakini siku wanakutana chumbani kwa ajili ya kufanya tendo mdada anaanza kutoa wigi, kumbe aliwahi kuungua na moto kichwani na hana nywele, anataa meno yake ya bandia, kumbe hata meno ya mbele alikuwa hana, anapovua nguo anagundua hata makalio yalikuwa ni yale ya kupachika, yaani ya Mchina,............. Lo lo lo lo....... Kama mwanaume alivutiwa na ule muonekano wa bandia na hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mdada................ Lazima atoke nduki.
   
Loading...