Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Kampuni ya Kilimanjaro Marathon inayoendesha Mbio maarufu za kila mwaka za “Kili Marathon” zinazofanyika Mkoani Kilimanjaro imetangaza kuwa kutakuwa na zoezi la ugawaji wa barakoa kabla na baada ya mbio kwa wakimbiaji wote wa mbio fupi na ndefu.
Vilevile wameeleza kuwa kutakuwa na kamati maalumu itakayokuwa inagawa vitakasa mikono kwa washiriki kwenye vituo maalumu, njiani mpaka mwisho wa mbio, na uwanjani kwa siku nzima ya mashindano. Watoa huduma wote katika vituo vya maji pamoja na uwanjani watavaa barakoa, gloves, aprons na watahakikisha wanatakasa mikono mara kwa mara muda wote wa mashindano
Wamesema hatua hiyo ni kutokana na wingi wa watu watakaoshiriki katika tukio hilo litakalofanyika Februari 28, 2021 Mjini Moshi. Mbio hizi zinafanyika huku kukiwa na madai ya COVID19 kuenea mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amekanusha madai hayo na kusema mkoa uko salama na magari ya maiti yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni kutoka mikoa mingine.
Pia soma
Kili Marathoni huhusisha ukimbiaji wa mbio fupi/nusu (half marathon) kwa umbali wa Kilomita 21.1 na ndefu/kamili kwa urefu wa Kilomita 42.2.