Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Katika kozi mojawapo kwenye chuo fulani kuna makabrasha kadhaa ya kihistoria yanayodai kuwa biashara ya kilevi ilikuwa na faida kubwa sana toka enzi za ukoloni. Mataifa ya Ulaya yalikataa katakata kuacha kupeleka pombe barani Afrika pamoja na kilio kikubwa cha wamishionari kuzuia ulevi. Pia yalikataa kubadili tozo katika uingizaji wa kilevi. Jamii za Kiafrika zilinunua kilevi kwa wingi na hata kupelekea jamii kadhaa ziuze watu wa jamii zingine utumwani ili zipate fedha za kununua kilevi hicho kutoka ughaibuni ambacho waafrika walikiona ni kikali na kinachodumu, yaani, bora kuliko pombe zao za asili!
Je, kilevi ndio msingi mkubwa uliofanya waafrika watawaliwe na waendelee, kwa ujumla, kuzidiwa mno katika medani ya kimataifa hadi leo. Zakumi, Nyani Ngabu, Gaijin na wanataaluma wengine wa hali ya waafrika karibuni mchangie mawazo!