Kilaza/kipanga ni yupi hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilaza/kipanga ni yupi hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by tindikalikali, Aug 28, 2011.

1. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#1
Aug 28, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
Wadau nimekuwa nikitatizwa na uwezo wa watu katika kufaulu mitihani. Kuna watu huwa wanafeli std 7 lakin huja kufaulu form 4, wapo wanaofaulu form 4 na kuja kufeli form 6. Na wengine wanafeli vibaya form 6 na wanafaulu vizuri. Vivyo hivyo chuo kikuu. Hapa nashindwa kuwatofautisha vipanga na vilaza{ukiwatoa wale ambao hawajawah kufeli katika masomo yao}.

2. Engager

Engager JF-Expert Member

#2
Aug 28, 2011
Joined: Jan 12, 2011
Messages: 329
Likes Received: 10
Trophy Points: 35
Mkuu huo ukiliza na upanga mnaujua nyinyi (wewe na wengine wenye mawazo yako) lakn in actual sence, hakuna kilaza wala sijui kipanga. Nakushaur unapoangalia uwezo wa mtu usiangalie ki masomo2. Angalia hata uwezo wa kutafta maisha na kuyamudu.

3. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#3
Aug 28, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
nashukuru kwa ushauri, mi nipo ktk masomo{ndiyo maana nimekuwa specific kwani}, ngoja niwasubiri wenye mawazo ya aina yangu.

4. King Kong III

King Kong III JF-Expert Member

#4
Aug 28, 2011
Joined: Oct 15, 2010
Messages: 25,154
Likes Received: 2,407
Trophy Points: 280
Muanzisha sredi unaonekana mjivuni sana wewe!!! wengi wenu mnakuja kufeli kwenye maisha tu,shule mnakuwa mnafaulu sana lakini mkiingia mtaani hamna kitu haaaaaaaaaaaaa!!!!! O-Level:DIv I Point 7--- A Tisa,A-Level:DIV I Point 3,CHuo unapata GpA 4.9,,,,Then unaingia mtaani mpaka miaka mitatu huna hata kiwanja full kutembea kwa mguuu haaaaaaaaaaaaaaa!!!

5. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#5
Aug 28, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
duh yamekuwa hayo? Ni kweli kufaulu mitihani siyo kufaulu maisha, ni vitu viwili tofauti lakini vinategemeana, lengo halikuwa kuonesha ujivuni>kufel ni tatizo{fikiria mtu mwenye div 1 form 4 then akapata div 0 form 6}, huyu lazma ana matatizo au kuna matatizo.

6. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#6
Aug 28, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,973
Likes Received: 2,967
Trophy Points: 280
Kuna sababu nying za kufel au kufaulu.
1. Mazingra: mazngra yanachangia maendeleo ya mtoto. Na hakuna mazngra yanayo fit kwa kila mwanafunz. Mf. Mwanafunz o level alisoma day then advance aende boarding inaweza badil matokeo yake.
2. Kujisahau. Kuna kipind mwanafunz anajisahau kwa kujihis kuwa tayar ameshafika. Mf. Mwanafunz anaweza o level atoke fresh then advance anajisahau, si ukilaza wala ukipanga.
3. Family problem kama kufiwa na watu wake wa karbu inaweza kuwa sababu ya kubadil matokeo.
Sababu zipo nying ila hakuna kilaza wala kipanga.

7. King Kong III

King Kong III JF-Expert Member

#7
Aug 28, 2011
Joined: Oct 15, 2010
Messages: 25,154
Likes Received: 2,407
Trophy Points: 280
Basi kwa hoja yako hiyo nakiri kwamba hakuna mtu kilaza wala kipanga.

8. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#8
Aug 28, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
kuna mtu nilipata kumsikia akidai kwamba vilaza hawapo, lakini hili sikubalian nalo sana, inatokea mtu ana favourable conditions na still anafeli, lakin mwingne ndan ya mazingira magumu anafaulu.

9. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#9
Aug 29, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,973
Likes Received: 2,967
Trophy Points: 280

thats why nimesema hakuna mazingira yanayomfaa kila mwanafunzi. Wengine ukiwapa mazngra mazur ndio tayar umeshampoteza and viceversa is true.

10. MBUFYA

MBUFYA JF-Expert Member

#10
Aug 29, 2011
Joined: Aug 15, 2011
Messages: 445
Likes Received: 1
Trophy Points: 33
Kwahiyo unataka uniambie kuna kipanga na kilaza wa shule na maisha?

11. MBUFYA

MBUFYA JF-Expert Member

#11
Aug 29, 2011
Joined: Aug 15, 2011
Messages: 445
Likes Received: 1
Trophy Points: 33
jamani hata hayo mazingira ambayo mnayazungumzia yanaweza kumfanya mtu aonekane kilaza au kipanga. kwa mfano wanafunzi wote wanaweza kuwa katika mazingira magumu, lakini ile kutambua kuwa upo katika mazingira hayo na kutafuta jinsi ya kufaulu katika mazingira hayo, ni ukipanga, kinyume chake ni ukilaza. pia watu katika mazingira mazuri, bado humohumo wapo wanao feli. kwa hili huwezi ukaniambia hakuna vilaza bwana. Au utamkuta mtu yuko chuo kikuu halafu yupo bize sanaa na mambo mengine kama uongozi, mahusiano, nk, na anasahau kabisa kutia bidii kwenye masomo, ukilaza umekaa hapo bwana. Sisemi mkiwa cuo msifanye mambo mengine, kipanga ni yule anayeweza kujitambua na kubalansi mambo bwana, mfano muandishi wa makala ya maswali magumu, aliweza kuandika na cw zilisoma vizuri.

12. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#12
Aug 30, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
Umeeleweka vizuri, nadhani ulitaka kusema hakuna kipanga/kilaza wa kudumu katika maisha ya shule?

13. mayenga

mayenga JF-Expert Member

#13
Aug 30, 2011
Joined: Sep 6, 2009
Messages: 3,759
Likes Received: 558
Trophy Points: 280
Unaweza ukawa kipanga kwa vilaza na ukawa kilaza kwa vipanga.Mimi nilianzia shule kijijini,nilikuwa sivuki top 3,lakini nilivyohamia mjini,mtihani wa kwanza nikashika nafasi ya 95 kati ya 120,mpaka nilipojipanga upya na kurudisha heshima.Hivyo haya mambo yanategemea na mambo mengi yakiwemo mazingira ya nyumbani na ya shulen pia.Shule za kata zimeongoza kwa wanafunzi waliopata sifuri lakini kwenye mitihani ya shule zao walikuwepo waliokuwa wanashika nafasi ya kwanza,ilipokuja NECTA wakaangukia visigino.

14. MWAKIGOBE

MWAKIGOBE Member

#14
Aug 30, 2011
Joined: Nov 1, 2010
Messages: 65
Likes Received: 1
Trophy Points: 0

Mmmh hili nalo linahitaji kautafiti

15. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#15
Aug 30, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
kweli mkuu na ndiyo maana kuna vipanga wa supplementary

16. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#16
Aug 30, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
ni kweli unachokisena, nilipata kufundisha hesabu katika shule ya kata miaka michache iliyopita. Test ya kwanza walianzia 35%, ndipo nilipowatambua wakoje. Test ya pili wa kwanza alipata 85%, huyu alijiita/walimuita kipanga.

17. Perry

Perry JF-Expert Member

#17
Aug 30, 2011
Joined: Feb 24, 2011
Messages: 10,029
Likes Received: 868
Trophy Points: 280

kumbe na we ni mwalimu?hongera sana!

18. tindikalikali

tindikalikali JF-Expert Member

#18
Aug 30, 2011
Joined: Jan 14, 2011
Messages: 4,883
Likes Received: 96
Trophy Points: 135
kwa hiyo katika yote niliyoandika umeliona hilo tu? Kwako kila aliyepata kufundisha ni mwalimu? Naona hata topic imekushinda kuchangia, kwa vyovyote ukilaza unakuhusu.

19. K

KAUMZA JF-Expert Member

#19
Aug 31, 2011
Joined: Aug 31, 2010
Messages: 685
Likes Received: 22
Trophy Points: 35
Inategemea na unamfasir vipi kilaza/kipanga. Kuna wanaofaulu sana darasani(kwa sababu wanakariri sana ilichosema mwalimu wake) lakini unapomleta katika uchambuzi na mazingira akawa mtupu kabisa. Mtu huyu kwangu ni kilaza. Na wapo ambao wanafeli sana darasani lakini katika maisha ya kawaida, ni mjuzi sana. Huyu kwangu ni kipanga. MFANO: Wakati nasoma chuo kikuu, kuna jamaa mmoja alikuwa akisimama kuelezea jambo fulani, darasa zima linatulia kwa kuwa anaeleza vitu alivyovifanyia utafiti hasa na anatoa reference sana. Tulikuwa tunamuita Encyclopedia, lakini siku ya mwisho alipata PASS nami nilikuwa na 2nd class, Upper division. Lakini pamoja na yote hayo, bado namkubali kuwa ni kipanga sana zaidi yangu. Na sasa ni mwanasheria wa ofisi fulani na anafanya vema kuliko wale waliofaulu sana darasni

20. U

Ulimakafu JF-Expert Member

#20
Aug 31, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 18,037
Likes Received: 750
Trophy Points: 280
Sawa kabisa.

Loading...