Kila nikipika wali nakosea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila nikipika wali nakosea

Discussion in 'JF Chef' started by Skillionare, Oct 22, 2012.

 1. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Wakuu kila nikipika wali bado hautoki vizuri ,nipeni ujanja wali utoke mmoja mmoja,sababu nikuandalia wali unaweza usitofautishe na ugali.
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Kama wewe ni bachala kama mimi hatua uliyopiga ni kubwa sana..........Acha mbwembwe
   
 3. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ratio ya maji na mchele ni muhimu sana.
  Unatakiwa kutumia 1:1.5 (mchele:maji). Hakikisha umefunika na umeweka kila kinachitakiwa. Usifunue funue wala kugeuzageuza. Hakikisha moto sio mkali bali wa wastani.
  Utashangaa matokeo super just like in a rice cooker.

  Kama huwezi kufanya hivyo pata/nunua rice cooker but it works the same.
   
 4. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  tumia rice cooker..simple!
   
 5. D

  Dina JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,779
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Inawezekana unaloweka mchele halafu wakati wa kupika bado unajaza maji kana kwamba mchele ni mkavu sana........Angalizo lingine, kama mchele ni mpya nao unawasumbua wengi, kwani kimsingi unakuwa ni kama ambao ulilowekwa, kwa hiyo mapishi yake ni muhimu maji yakalingana na mchele (vikiwa jikoni). Kwani maji yakiwa mengi, huo wali wako utatota (utakuwa kama ugali)...
   
 6. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hiyo rice cooker itabidi niitafute asante mkuu
   
 7. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  nimecopi ..asante dina
   
 8. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,265
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  nakumbuka mama wakati ananifundisha jinsi ya kupika wali wa nazi kipindi hicho alikuwa akinieleza ipo siku utakuwa peke yako nakumbuka nilikuwa na miaka 12. siku ya kwanza akanifundisha kuondoa mawe kwa kutumia maji siku ya pili na kisha kupika wali nakumbuka alikuwa akisema utamu wa wali mahaba ndio yakuonja kujua wali imtamu kiasi gani halafu akachukua ukoko wa chini akaniambia nile kama nikikuta kokoto au mchanga atanipa 200/= sikukuta mchanga wala kokoto akaniambia kesho yake nikanunue sufurua ndogo nipike na nikiupika vizuri basi atanipa 500/= nikanunue nitakacho kwakweli alitumia technic ya zawadi kunifundisha na kwakweli kama alijua kuwa kuna kipindi nitaisha mwenyewe mbali na nyumbani na miaka kadhaa kabla ya kuoa.

  Nakumbuka alikuwa akinieleza kuna wali waweza kuwa
  1. wa kiini cha 1 au 2
  2. uliotota
  3. bokoboko
  4. uji

  Ahsante sana mama ulivyokuwa unanifundisha bibi alikuwa akikulalamikia kuwa unanitesa kwa kunifanya nipike na kama sio ukali wako nisingejua kupika vyakula mbalimbali hii inanifanya wakati mwingine kumsaidia mke wangu kupika siku za weekend au nikimuona kachoka kwasababu ya kulea mtoto na kipindi chake cha ujauzito. Ni wewe mama uliyenifundisha kuwa hakuna kazi ya mwanamke kwani nilikuwa mtoto pekee wa kiume na sikuwa na dada au kaka kwa sasa naweza pika chochote nitakacho kuanzia pilau biriani vibibi hadi mikate karibia yote tupendayo kula kuunga kwa nazi au kwa mafuta. Ahasante mama ijapokuwa leo unatimiza miaka 17 tangu ututoke hakika najivunia kuwa na mama kama wewe nakupenda sana na Mungu akulaze pema peponi wewe pamoja na Baba sintoisahau ajali ile iliyoondoa roho zenu nami kupona kwa miujiza
   
 9. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,846
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kupika wali kumbe ni mtihani kwa wengine....
   
 10. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,255
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Pika chai. Utaweza!

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 11. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,255
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Njoo unipikie


  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 12. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,846
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Endelea tu kula ubwabwa wako......haji mtu :becky:
   
 13. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,255
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Itabd nile pepeta. Unaujua?

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 14. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,846
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  najua bana, si ndo chakula ya visiwani hiyo.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,025
  Likes Received: 5,193
  Trophy Points: 280
  usitie maji mengi utatoa bokoboko kama sio uji.....

  Kama hujui kabisa nunua rice maker ile ukifuata kipimo walichokuaandikia unatoa wali super
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,220
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  Wali ili utoke umenyooka kwanza kaanga mchele uliooshwa, kulowekwa dk chache na kuchujwa maji kwa kuutia kwenye mafuta ya motoo (vijiko vikubwa 2 vinatosha ubwabwa wa watu 2, manake najua kiporo kina sehemu yake,lol). Geuza kama dk 1 tu, kisha tia maji ya moto kiasi cha kufunika mchele wote tu na sio zaidi. My moms recipe ilikuwa kikombe cha mchele kwa kikombe unusu kwa maji japo siitumii hiyo. Mchele ukianza kuchemka tu punguza moto na hakikisha umefunika sufuria. Usigeuze hadi maji yakauke. Geuza na angalia kama una kiini. Unaweza kumalizia kwa kuweka kwenye oven ama kupalia mkaa.

  Tip: kubadilisha ladha ya ubwabwa wako unaweza kuweka:
  1 binzari nyembamba aka jeera kiduchu.

  2 Baada ya ubwabwa kukauka maji unaweza kuweka a grated onion kabla ya kugeuza. Ladha yake utaomba poo.

  3 Well, kichaa kikikushika a pinch of binzari sio mbaya.
   
 17. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,639
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
 18. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,639
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  pole sana mkuu kwa kupoteza wazazi..

  iliujatoa msaada wa kupika wali bwana..
   
 19. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,836
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Vp jinsi ya kupika biliani
   
 20. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,929
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hakuna haja ya Rice cooker,
  kula desa hili...

  1.Osha mchele wako vizuri then uweke pemben,then

  2.weka safuria jikoni,then weka mafuta yanayokutosha kwenye safuria yasubiri yachemke.

  3.yakisha chemka,weka mchele wako,chukua chumvi weka moja kwa moja,then funika.

  4.Acha kama 5 mpaka 6,mchele uive kwa mafuta,funua,ugeuze funika tena kama 2dk,then weka maji yako kwa juu yasiwe mengi sana,weka machache.funika mpaka ukauke na usiugeuze,hauta ungua chini kuna mafuta.
  Fanya hvyo leo utanipa jibu.
   
Loading...