Kila mtu Tanga anamiliki TZS3,204,244 kwa mwaka

Bibianna

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2025
Posts
400
Reaction score
135
1754287665161.png

===
Rais Samia Katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Tanga umepokea shilingi 3,091,742,180,252.12 (trilioni 3.091) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya kisekta, ikijumuisha sekta za huduma za kijamii, uchumi, miundombinu na mazingira, hali inayochochea zaidi ukuaji wa uchumi wa Mkoa na kuboresha ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa Takwimu za NBS za mwaka 2024, pato la Mkoa wa Tanga (GDP) limeongezeka kutoka shilingi trilioni 6.818 mwaka 2020 hadi trilioni 9.581 mwaka 2024, ambalo ni sawa na asilimia 4.7 ya pato la Taifa (shilingi trilioni 205.846).

Aidha, wastani wa pato la mtu mmoja (Per Capita Income) umeongezeka kutoka shilingi 2,783,908.00 mwaka 2020 hadi shilingi 3,433,368.00 mwaka 2024, ikiwa ni juu ya wastani wa kitaifa wa shilingi 3,204,244.00. Hii imeuweka Mkoa wa Tanga katika nafasi ya sita kitaifa katika mapambano dhidi ya umaskini na mchango wa pato la Taifa.

Uchumi wa Mkoa wa Tanga unategemea zaidi shughuli za wananchi katika sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Maliasili na Utalii. Takriban asilimia 80 ya wananchi wanajishughulisha na Kilimo, Mifugo na Uvuvi, asilimia 9 na shughuli za mazao ya misitu, ufugaji nyuki na uchimbaji madini, asilimia 6 na biashara, viwanda, usafirishaji na sekta ya fedha, huku asilimia 5 wameajiriwa kwenye sekta ya umma na binafsi wakitoa huduma mbalimbali za kijamii.
 
Attachments

  • 1754287666496.png
    1754287666496.png
    9.4 MB · Views: 30
Ndio maana naona threads kibao kumbe ni chawa ingizo jipya posho imetembea leo.

Kuandika thread na kujijibu ni aina moja wapo ya mental disorders.
posho ya nini CCM ni kujitolea tu
 
TANGA YA MATANGA AU TANGA TANGANI😂😂😂
 
Ambayo kwa mwezi ni laki 2 na nusu ...kwa siku ni elfu 8.
Basi sawa.
 
===
Rais Samia Katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Tanga umepokea shilingi 3,091,742,180,252.12 (trilioni 3.091) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya kisekta, ikijumuisha sekta za huduma za kijamii, uchumi, miundombinu na mazingira, hali inayochochea zaidi ukuaji wa uchumi wa Mkoa na kuboresha ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa Takwimu za NBS za mwaka 2024, pato la Mkoa wa Tanga (GDP) limeongezeka kutoka shilingi trilioni 6.818 mwaka 2020 hadi trilioni 9.581 mwaka 2024, ambalo ni sawa na asilimia 4.7 ya pato la Taifa (shilingi trilioni 205.846).

Aidha, wastani wa pato la mtu mmoja (Per Capita Income) umeongezeka kutoka shilingi 2,783,908.00 mwaka 2020 hadi shilingi 3,433,368.00 mwaka 2024, ikiwa ni juu ya wastani wa kitaifa wa shilingi 3,204,244.00. Hii imeuweka Mkoa wa Tanga katika nafasi ya sita kitaifa katika mapambano dhidi ya umaskini na mchango wa pato la Taifa.

Uchumi wa Mkoa wa Tanga unategemea zaidi shughuli za wananchi katika sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Maliasili na Utalii. Takriban asilimia 80 ya wananchi wanajishughulisha na Kilimo, Mifugo na Uvuvi, asilimia 9 na shughuli za mazao ya misitu, ufugaji nyuki na uchimbaji madini, asilimia 6 na biashara, viwanda, usafirishaji na sekta ya fedha, huku asilimia 5 wameajiriwa kwenye sekta ya umma na binafsi wakitoa huduma mbalimbali za kijamii.
kazi inaendelea vizuri sana
 
Back
Top Bottom