Kila mtu anahitaji mchango wake kutambuliwa

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,488
6,422
Habar Wana JF,

Nimevutwa kuandika Uzi huu baada ya Leo asubuhi kumuaga dada wa kazi ambaye alikuwa hodari Sana katika kuwahudumia watoto wangu,kipindi chote tulicho ishi nae akifanya kazi vizur Sana na Kwa mapenzi makubwa,tunajisikia fahari juu yake.

Kabla ya kuondoka nilimshukur Sana Kwa kipindi chote ambacho aliishi na Sisi na kuonyesha mapenzi makubwa Kwa wanangu,wakati namwambia maneno hayo ya shukrani na kutambua mchango wake hakika niliona tabasamu zuri na nuru katika Sura yake,alionyesha kufurahi Sana kusikia maneno Yale kutoka kwangu,hata binafsi nilijikuta nafurahi kuonyesha na kushukuru huduma yake kwetu.

Nikawa najiuliza je ingekuwaje kama ningekuwa natoa shukrani zangu hizi hata wakati hajaondoka,Bila Shaka ingempa hamasa ya kujituma zaidi katika KAZI zake,lkn wewe msomaji wa uzi huu hujachelewa bado,tambua mchango wa shamba boy wako,dada wako wa kazi na wale wote ambao Kwa maana moja au nyingine wanakusaidia katika shughuli zako,ni Jambo zuri Sana na litaongeza motivation ktk kazi zao.

Nadhani baadhi yetu tumeshaona ktk mabenki utakuta kuna picha ya mfanyakazi Bora wa wiki au wa mwez,kwanini wanafanya vile? Wanafanya vile kwakuwa wanatambua mfanyakazi yoyote mchango wake au juhudi yake ikitambulika basi huwa ni chachu ya kuongeza hamasa katika KAZI zake,na Kwa wafanyakazi wengine pia.

Je, vipi kuhusu hawa watu ambao wanawaangalia watoto wetu,wanapika chakula chetu,wanafanya usafi katika majumba yetu? Kwa mtazamo wangu Mimi hawa ndio wanastahili kutambua mchango wao mkubwa na kuwaonyesha mapenzi yetu makubwa kwao,kwakufanya hivyo watakuwa wema kwetu pamoja na familia zetu.

Ni hayo Tu.
 
Moja ya nyuzi bora kabisa kwa leo hapa JF.
Hili la kutotambua mchango wa mtu katika jamii yetu ni tatizo kubwa sana.
Kuna ukweli mkubwa sana wa kuwa binadamu yeyote akionyeshwa kuthaminiwa kwa jambo fulani afanyalo,basi tija katika jambo hilo ilakuwa mara dufu.
 
Back
Top Bottom