Mtu anakukosea au mwenzio anakufanyia kitu kibaya eti unakaa nacho moyoni hutaki kumwambia na unaendelea kusalimiana naye tu vizuri na unacheka huku moyoni ukiwa na maumivu, je wewe umekuwa MTUSI/ MHUTU ? mpe makavu laivu AJUE ALIKOSEA NA ALIKUFANYIA AMBAVYO SIO AJUE KABISA.
Mke au mume anatoka nje ya ndoa au ana chepuko unakaa kimya eti unavumilia tu kwa nini usimpe makavu, kwanini unateseka hayo magonjwa utaweza kuyatibu baada ya kukaa na maumivu kwa muda mrefu, acha ujanja wa kusema eti namlia hela kwanza, iyo pesa haitatibu magonjwa ya moyo, presha na vidonda vya tumbo na anaweza akakuacha ukabaki nayo na hela ikaisha unabaki unahangaika mwenyewe.
Eti namuogopa ni mkwe wangu au shemeji yangu hata nisaidia nikikataa kufanya naye mapenzi wewe akiwa na ukimwi, akikupa ujauzito akikuharibia maisha itakuwaje, mwambie ukweli haifai.
Kuna mmoja aliniona bwege kabisa, akiwa na shida ndio atanitafuta kwa bidii siku yote hiyo, asipokuwa na shida ahaha atakwambia yuko buzy na unaweza ukamtafuta weekend usimpate eti ana wageni ila akiwa na shida anakuja fasta kwenye mtandao mawasiliano yanaanza nikaona hapa nikimwambia kitu flani atakasirika basi nikamchokoza achukie ili nikimbie mazima hadi leo na siwezi pokea simu zake.