Kila msichana ninaemtongoza ananiomba hela, whats this?

Kila msichana ninaemtongoza ananiomba hela, whats this?

geophrey140

Senior Member
Joined
May 4, 2013
Posts
134
Reaction score
209
Mimi ni kijana wa miaka 25, ninafanya kazi nimefikia umri wa kutafuta mchumba wa kuoa ila hawa mabinti sijui wakoje, kila ninayemtongoza haipiti siku ananiomba hela kwa visingizio mbalimbali na mimi msichana akishaniomba hela design hii hapo hapo naona sio namuona kimeo ndio wale wale.

Kwani mapenzi siku hizi lazima usambaze hela kwanza ndio upendwe ama?

Naomba ushauri
 
Pole
Hiyo ya kuomba hela imekuwa janga la kitaifa, kila mwanaume alia hilo humu.
Wakati wa kutafuta mke, kuwa makini mnoo. Wengi wanatafuta wa kuwasogezea siku tu na sio kuolewa. Miaka yako kumpata mwanamke wa kutulia nae ni pagumu,wengi wako vyuoni na waliobaki wanatafuna ujana taraaatiiibuuu ndo maana wanakuomba hela tuu hawawazi lingine !!!!

Mshirikishe Mungu kwenye hilo
 
Kama upo serious unatafuta mwenza wa maisha, achana na visichana vinavyokwambia baby nina njaa, mara baby ninulie iPhone, mara baby njoo na baga, mara baby unajua kodi ya safari hii sijui nitapata wapi. Achana nao hao, hawanaga future kabisa. Tafuta mwenza ambae atakwambia baby tufungue kabiashara, baby leo nikupikie nini, baby tupunguze mambo ya anasa tusije tukashindwa kulipa kodi n.k.
 
Sakayo umeongea bonge la point. [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] . Haya yananisumbua sana. Kunamuda nilijiwazia kuwa Mungu hayuko fair. Why nakutana na watu wa ajabu ajabu tu
 
Sio watu wa ajabu,bado hawajui wanataka nini, hujakushtuka wakati wameshachelewa!!!
 
Back
Top Bottom