Kila la kheri Taifa Stars, ni zamu yetu AFCON 2019

Dec 13, 2018
30
140
KILA LA KHERI TAIFA STARS, NI ZAMU YETU AFCON2019.

Leo 12:15pm 24/03/2019.

Taifa Stars leo Jumapili jioni itashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kuandika historia ambayo vijana wengi wa kizazi kipya hawajawahi kuiona. Taifa Stars inacheza Grand Finale yake leo jioni kufuzu fainali za Afcon ambazo imethibitishwa zitapigwa hapo baadae Nchini Cameroon.

Stars ipo kundi L lenye timu zenye historia nzuri kisoka za Uganda, Cape Verde na Lesotho. Mechi hiyo ya Stars ni ngumu kwani licha ya matokeo ya ushindi pia itahitaji tokeo la Cape Verde kumfunga Lesotho,Tanzania inahitaji kushinda kwani isipofanya hivyo hata Cape Verde na Lesotho bado ana nafasi ya kufuzu.

Stars yenye pointi tano,Leo chini ya Captain Mbwana Samatta na Kocha Emmanuel Amunike inahitaji kwa vyovyote vile kushinda ili kufikisha pointi nane ambazo hazitaweza kufikiwa na Cape Verde na Lesotho,iwapo Cape Verde atamfunga Lesotho ama Lesotho kutoka droo na Cape Verde.

Cha muhimu ambacho Stars wanapaswa kufanya leo Jumapili ni kutuliza akili uwanjani na kufanya vile vitu sahihi na maamuzi ya haraka kama alivyofanya Juma Pondamali, kuupiga mpira kumfikia Hussein Ngulungu ambaye nae baada ya kuutuliza alimpigia pasi ndefu Mshambuliaji Peter Tino aliyewalamba chenga mabeki wawili na kuachia shuti kali nje ya 18 lililomshinda Efford Chabala kufuzu Afcon 1980.Akili waliotumia Juma Pondamali, Hussein Ngulungu na Peter Tino waitumie leo kina Mbwana Samatta,Aishi Manula, Simon Msuva,na Jonas Mkude kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuwapa raha mashabiki wa Tanzania.

Mashabiki kibao wa Taifa Stars watakuwa Uwanjani kwa Mkapa na kwenye runinga zao jioni ya leo wakiwaombea Stars kila la kheri na ushindi upatikane.

Kama kweli wachezaji wakiweza kutimiza azma hiyo ya mashabiki, tunaamini Watawekwa sambamba kwenye historia pamoja na akina Peter Tino na Juma Pondamali na furaha ya aina yake ambayo yote itatokana na dakika 90 za leo,na kama watakwenda Cameroon na kuchukua Ubingwa wa Afrika basi Wachezaji wa Taifa Stars watapewa heshima sawa na Wapigania Uhuru wa Nchi yetu.Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Taifa Stars, Tupe neema ya kuweza kushinda mechi ya leo na siku zote, Amina.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Umekosea saana kuwafananisha stars na WAPIGANIA UHURU aise

Nimepoteza hamasa ya kuwashangilia toka nilivyojua kuwa kufuzu kwa stars kunategemeana na matokeo ya Lesotho

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Uchangiaji wa aina hii unaonyesha mtu anaandika jambo ambalo hana taarifa za kutosha kuhusu anachoandika, hivyo hata maana ya lengo la uandishi wake linakosa uzito, fainali za AFCON 2019 si Cameroon, hakuna uwanja wa Mkapa Tanzania..
 
Huyu atakuwa ni muuza jezi zenye alama ya kujumlisha!
 
Bora tupigwe tu tujue moja maana taifa star imefanywa mali ya ccm.
Mpira umeingiliwa na wanasiasa tusitegemee matokeo mazuri kwenye mechi ya leo
 
Back
Top Bottom