Tuombe Mungu, haya mambo hayatabiriki, mimi kwa kusikia, nasisitiza kwa kusikia jinsi kesi ilivyoendeshwa nina imani Lema atashinda, ila chochote kinaweza kutokea hivyo inabidi tumwombe Mungu. Kinachoniudhi CDM ni migogoro isiyoisha, hivi, mtego mdogo kama wa Wassira mmeshindwa kuutegua? Hii serikali haiwezi hata kufanya jambo lolote la maana, mfano kuua, inaishia kung'oa meno, inaweza kweli kununua watu makini kama wa CDM?