Kila la kheri Kamanda LEMA

Ukifuatilia uzi huu utagundua Lema ni tumaini la wengi. Watu wamechoka na hawa vijana wanaonunulika kwa bei ndogo na kusaliti wapambanaji wanaojitoa kwa moyo mmoja kutetea wanyonge.
Kwa vile wapuuzi tumeshawafahamu tuchukue hatua ila Lema kumbuka ushinde au ushindwe hakuna cha kukuzuia kuendeleza hili libeneke maana hata ulipokuwa umezuiwa kuingia Bungeni mziki wako kila mtu aliuona nchi nzima
 
Nimeanza kusherehekea ushindi wa lema toka leo. Watakao ungana na mimi,wani inbox,nitalewa zaidi ya daimond
Nadhani nilizungumza hili toka jana,sasa waliokuwa na imani na kauli yangu walianza kula kuku(si bata mana bata ni mchafu).
 
Anakuja kutuletea fujo tu Arusha kulikuwa na amani muda ambao hukuwepo sasa tumerudi kulele.
Hukumu ya rufaa yako ya kupinga kuvuliwa Ubunge ni kesho pale Mahakama ya Rufani ya Tanzania. Wewe ni Kamanda makini,mjenzi wa hoja,mpambanaji,mpigania chama,huna makundi,huongozi kakikundi cha wasaliti,hukeshi mitandaoni ila mikutanoni kwenye M4C pamoja na Makamanda wengine wa jeshi la ukombozi la CHADEMA.

Kesho utaandika historia.Utaionja ladha ya haki.Kwa lolote liwalo,tupo pamoja nawe. Kesho,utauvaa utu upya. Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani watakuwa mboni ya haki yako kesho. Tunaombea waseme kama hivi " In the premises, we allow this appeal with costs...."

Ubarikiwe Kamanda Godbless Lema!
 
Lema ,

Boneka waitu akakubi ka X- mas no mwaka oguya. Ebiro bikyaliyo:
obanze okalise kagile ebishaju.
 
Kamanda lema unatisha!huu ndio mwanzo wa ukombozi!watanzania saa ya ukomboz ni sasa! Lem mfan wa viongoz shujaa,hodari na mzalendo!nyerere alitukomboa kutoka ktk makucha ya wakolon wanyonyaj!wewe utatukomboa kutoka ktk makucha ya mafisad wa ccm!
 
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Godbless Lema amerudishiwa ubunge wake baada ya kushinda katika rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo.


Hukumu imeangalia haswa swala la “Locus Stand” ya kama “waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo”. Kadiri ya pingamizi ya mawakili wa Lema Ndg. Kimomogoro na Tundu Lissu, waliofungua shitaka dhidi ya Lema hawakuwa na “Locus Stand” ya kufanya hivyo. Kwa hiyo mengine yote yanakuwa “null and void”. Hukumu haikuchukua hata nusu saa aibu iliyoje hii?.


Hoja moja tu tena ya kwanza kati ya hoja 18 zilizowasilishwa na upande wa rufaa kupinga hukumu hiyo mbele ya majaji Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao Nathalia Kimaro imeonesha ukomavu wa mawakili Kimomogoro na Tundu Lissu. Nachukua fursa hii kuwapongeza majaji hawa Salum Massati, Bernard Luanda na Nathalia Kimaro na mawakili Kimomogoro na Tundu Lissu kwa kuonesha ukomavu wao na kuthibitisha kuwa taaluma yao haina mashaka hata chembe. Mungu awajaalie wazidi kuwa na mafanikio makubwa na heri katika kazi zao, tunahitaji wazalendo kama hawa ili nchi iwe na ustawi na kudumisha haki.


Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Serikali inatakiwa kumchunguza kwa makini Jaji Gabriel Rwakibalira. Kwa maoni yangu nadhani huyu ni kada wa CCM na kama sivyo basi taaluma yake ni batili na butu sharti achunguzwe pia alisomea wapi kwani hawa ndiyo akina KIHIYO wanaogushi vyeti na kukalia nyadhifa muhimu huku wajuzi walio makini wakikosa nafasi kwa kuwa hawana ndugu wa kuwapachika katika nafasi hizo. Hivi karibuni kulitokea tuhuma zilizoenea kuwa baadhi ya majaji na mahakimu hawajui Kiingereza hali inayosababisha kushindwa kutoa hukumu sahihi kwa misisngi ya haki bali wanahukumu kwa utashi na matakwa yao hii ni hatari kwa taifa letu. Hakika kuna haja ya uteuzi wa Majaji kuchunguzwa upya hii ni aibu kwa Mheshimiwa Rais na washauri wake kwani huu ni mfano mmoja tu wa majaji uozo, Je, wako wangapi wa sampuli yake?


Swali la msingi la kujiuliza ni: Je, ni raia wema wangapi wameathiriwa na hukumu butu kama hizi hizi za Jaji Gabriel Rwakibalira na wakatumikia adhabu zisizo sahihi kwa kukosa utetezi wa mawakili makini?
 
mkuu hii lugha ya kihaya umejifunza wapi?

Huko huko Bongo kwani nimeishi kwa takriban miaka 7 kanda ya ziwa. lakin hapa nimebandika baada ya kuona jila la jaji aliyehukumu kwa mara ya kwanza.

Nyegera waitu
 
Back
Top Bottom