Kila la kheri Kamanda LEMA

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Hukumu ya rufaa yako ya kupinga kuvuliwa Ubunge ni kesho pale Mahakama ya Rufani ya Tanzania. Wewe ni Kamanda makini,mjenzi wa hoja,mpambanaji,mpigania chama,huna makundi,huongozi kakikundi cha wasaliti,hukeshi mitandaoni ila mikutanoni kwenye M4C pamoja na Makamanda wengine wa jeshi la ukombozi la CHADEMA.

Kesho utaandika historia.Utaionja ladha ya haki.Kwa lolote liwalo,tupo pamoja nawe. Kesho,utauvaa utu upya. Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani watakuwa mboni ya haki yako kesho. Tunaombea waseme kama hivi " In the premises, we allow this appeal with costs...."

Ubarikiwe Kamanda Godbless Lema!

-YAMETIMIA-


 
wana wa arusha wanasubiri kwa hamu!
Vyovyote itakavyokuwa atapokelewa kama shujaa.tumeandaa ndege ya kumrudisha kamanda nyumbani!
 
Nimeanza kusherehekea ushindi wa lema toka leo.

Watakao ungana na mimi,wani inbox,nitalewa zaidi ya daimond
 
Mungu asaidie kwa kweli....inaweza kupunguza hii tension ya vijana vibaka na wenye tamaa wanaoharibu chama
 
From my heart, kwa nia safi ya Lema na Tanzania hii namtakia heri.

Najua atashinda!
 
Da, sijui itakuwaje hiyo kesho, Ila kwa vyoyote vile itakavyo kuwa, poa tu, Mungu awatangulie
 
Itakuwa pigo kwa Zitto coz alimtaget Kamanda lema.hawa wawili hazipandi kwa kuwa zitto hataki kupigwa bao asalie na umaarufu bila mbadala wake kuwepo.
 
Yes, Namuombea Lema ashinde na moyo wangu unaniashiria atashinda kwa jinsi kesi ilivyo kaa. Lema, endelea kujenga chama. Achama na Makundi ya wapumbavu. Sijakuona katika mabaraza ya wenye mizaha. Chama kitajengwa na wenye moyo siyo wenye njaa. Propaganda zote hizi ni upepo zitapita.....................
 
Naamini kwa uweza wa mungu utashinda hii kesi braza.ww ni jembe mkubwa,CDM tunakuhitaji WTZ wanakuhitaji na hata WANA-A TOWN wanakuhitaji.Hakika Lema akishinda hii kesi tutapunguza huu upuuzi unaofanywa na hawa was8****.GODBLESS BRAZA
 
mungu ni mwema atawaogoza majaji kutenda haki! Lema napenda sana siasa zako!
 
kwa uwezo wake Allah mwingi wa rehema, naamini kamanda lemaa atashinda.
 
Our prayers with him, we are crossing our fingers for his victory tomorrow
 
Baada ya kesho tutajua, tuishi tanzania au Tutafute hifadhi msumbiji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…