Radium
JF-Expert Member
- Aug 5, 2022
- 490
- 871
Hapa kuna nyekundu kijani na blue. Lakini nini kinafanya ujue kwamba unachokiona ni cha blue na mimi nakiona ni cha blue?
Rangi tumezipa majina ili iwe rahisi kupata reference wakati wa mawasiliano. Yani kama nikisema nataka shati jekundu, ujue naongelea nini kama kwa wakati huo siwezi kukuonesha kitu chekundu kama mfano.
Lakini sasa, hakuna jinsi ya kujua kama ninachoona ni cha blue basi na mtu mwingine anaona ni cha blue. Pamoja na hatua kubwa tuliyopiga katika ugunduzi as a specie, bado kuna KILA KITU TUSICHOKIJUA.
February, 26 2015 picha moja ya gauni iliwagawa internet users kwa sababu ya rangi zake. Wote tunazijua optical illusions. Hizi ni kigezo tosha kwamba wewe unachokihisi sio lazima kiwe ninachokihisi.
Unachokiita blue inawezekana ndicho ninachoita kijani. Ni sahihi kuhisi kuwa sehemu fulani duniani kuna mtu anatuona wanadamu tuna meno ya dhambarau.
71% ya dunia imefunikwa na maji.
60% ya mwili wa mwanadamu ni maji.
80% viazi mbatata.
93% tikiti maji.
95% tango.
Iko wazi kuwa maji ni kiuongo cha lazima kwa maisha duniani. Lakini hatujui mengi sana kuhusu maji. Kidogo sana kuhusu bahari.
Mpaka sasa mwanadamu ameweza kuchunguza 5%-10% ya sehemu ya bahari.
Kuhusu hizo asilimia 90% zilizobaki...... hatujui kitu. Inatisha zaidi kwamba kuna samaki kama barrel-eyed na bulbfish wamegundulika ila pia wapo kwenye asilimia hizo hizo chini ya 10%.
The Deeper You Go The Craziest Things Seems To Get.
Nini kipo kwenye kitako cha bahari?...... simply WE DON'T KNOW.
Wanadamu kama specie, tumejitahidi kwa upande wetu. Tumeunda nguo kutokana na hali ya hewa, tumeunda makazi kueouka wanyama wakali, silaha kwa ajili ya uwindaji, pesa kurahisisha biashara.
Lakini vipi kuhusu moto. Moto ni uvumbuzi au ugunduzi(invention or discovery)??
We don't know.
Vipi kuhusu muziki.
Wanasayansi wanadai kuwa muziki ni miongoni mwa inventions za mwanadamu. Kwamba wakale walitumia muziki kuziunga jamii zao.
Lakini je ni kweli mwanadamu alivumbua muziki?
Je hatujaugundua tu kutoka kwenye sauti tulizosikia ambazo hufurahisha masikio?
Ndege wanaimba, nyangumi anaimba hata vyura wa mitini wana sauti nzuri baadhi ya nyakati.
Je kweli tunaweza kusema binadamu ndiye mvumbuzi wa muziki?
Kama ni ndio, Je niipi maana halisi ya muziki?
NADHANI HATUTAWAHI KUJUA.
Moja ya vumbuzi kubwa zaidi za wanadamu zinazotupa rank kubwa among other species, ni uvumbuzi wa vifaa/zana.
In fact, kwa muda mrefu sana, scientist wanaamini kuwa hiki ndicho kanatufanya kuwa watu. Sisi ndio wanyama pekee amabo kwa kutumia zana, tumeweza kuexpand na kukua kwa haraka.
In fact, sio sisi pekee tunaotumia zana. Wanyama wengi especially primates hutumia zana kutafuta chakula mpaka hata kusafisha vinywa vyao na zaidi ya hayo.
Je nini kifanyike redefinition of human au redefinition of tools?
Je tuwakubali chimps kuwa ni human?.... of course not.
Kama Utumiaji Wa Vifaa Sicho Kinacgofanya Tuwe Watu Na Kujitofautisha Na Species Zingine, Je Ninini?
Katika research hiyohiyo ya utumiaji vifaa, imeoneka a pia sokwe wana personality na wana think rationally (via facts and reasoning)
Wana majuto na wana hisia. Wanabusu wanakumbatiana na wanabebana na kucheza.
Wana uwezo wa kudevelop bond na member wa familia na jamii yao. Na huweza kudumu kwenye mshikamano huo kwa zaidi ya miaka 50.
IF EMOTIONS, RATIONAL THOUGHTS, AND AFFECTIONATE ACTIONS DO NOT, THEN WHAT MAKES US HUMAN?
Kuna wakati ilisemekana kuwa sisi ni watu kwasababu tuna self-aware. Yani mtu anajijua vizuri kasoro na uimara wake na matatizo yake. Ukweli ni kuwa wanyama wengi wana consciousness pia.
2012 kundi la wana neuroscientist walieka declaration kwenye consciousness kuwa
" Humans are not unique in possessing neurological substrates that generate consciousness. Non human animals including all mammals and birds and many other creatures including octopus also posses these neural substrates"
#If consciousness, sentience, wakefulness and the ability to feel and experience do not, THEN WHAT MAKES US HUMAN???
We really don't know.
Tunavyojua tu ni kuwa siku moja hatukuwepo, saivi tupo, siku moja hatutakuwepo tena.
Hatujui kilichotokea wakati hatupo na hatujui kitatokea nini tukifa.
Mtu akifa halafu akarudi tena kuwa hai, hali hii huitwa NEAR DEATH EXPERIENCE. Hii ni kwa sababu tunaamini kuwa kifo ndio mwisho kwahiyo aliyefufuka tunaamini hakufa.
Lakini vipi kama ni kweli alikufa? Tatizo hatujui,

Vipi kama kuna imanj mojawapo ya dini ni ya kweli na kuna maisha baada ya kufa?
Dunia yenyewe haimake sense na ina mavitu ya ajabu. Kwa mfano nani alitengeneza Stonehenge na kwa ajili gani.
Pia zile Pyramids? Wapo wenye kuamini kuwa miungu wa Egypt walijenga wengine wakasema ni watu wakawaida tu waliojenga.
#LAKINI KIUHALISIA..... HATUJUI.

Akili ya mwanadamu ndiyo kila kitu.
Kila kilichotengenezwa kugunduliwa kusemwa kufikiriwa kuhisiwa n.k n.k yote huanzia kwenye bongo za wanadamu kisha kuwekwa kwenye utendaji.
#Ila bado KIUHALISIA hatujui how powerful a human mind can be.
#PLACEBO EFFECT.
Hapa daktari anafanya kumpa mgonjwa matibabu eidha kumpasua labda ili kutoa let say kidole tumbo au kumpa vidonge or whatever lakini in reality hafanyi hivyo. Anampasua ndio lakini kidole tumbo hakiondoi, au anampa vidonge vya vitamin c mgonjwa wa kifua kikuu au anamchoma sindano yenye maji tu kama tiba.
Ajabu ni kuwa ubongo unaregister matibabu na mtu anaanza kupona.
So basically ubongo unaponya mwili ila ukiwa tu unaamini kuwa mwili umepewa matibabu wakati hakuna matibabu.
Mtu akijiambia mambo mazuri hata ya kujidanganya ni kweli ubongo huamini na huadopt mood nzuri.
Kwahiyo bado ubongo nao ni utumbo tu. Fikiria ni mangapi hatuyajui.
Tunadhani tunajua mengi kuhusu wanyama, mbwa wana upendo kwa wamiliki wao, paka ni wazuri na simba ndiye mfalme wa mwituni, hatakama anaishi Savannah,

Kwenda kwenye outer space ni moja ya mafanikio makubwa ya mwanadamu ila mafanikio haya yametuonyesha sisi ni kitu kidogo kiasi gani.
Mpaka sasa zimegundulika solar systems 2500 na zinaweza kufikia makumi ya mabilioni.
# Hatuwezi KUJUA.
Na hayo yote ni kwenye galaxy yetu tu, THE MILKY WAY GALAXY, nayo ni moja kati mabilioni ya Galaxy zilizopo katika UNIVERSE.
Vipi kama kuna MULTIVERSE.
NI kubwa mno kiasi kwamba huwezi kujizuia kujiuliza, Je tuko peke yetu?
Na kama hapana, Je mbona hakuna aliyesema Hi!
Tuna ideas ndio, lakini kama kawaida Hatujui.
Hatuwezi kuprove vitu vingi mno. Kwa mfano moja ya maswali fundamental kuhusu ulimwengu ni
JE ULIMWENGU UMEUNDWA NA NINI?
Tutasema kila kitu huundwa na smallest indivisible atoms lakink hizo atoms hutoka wapi?
Je tunapokufa, atoms zilizotuunda huenda wapi na huwa nini? Kila kitu kingine?
Kusoma kufikia hapa umetumia dakika kadhaa za muda wako.
Muda uko persistent, kwa kila kitu chenye uzito muda hausimami. Tunachojua ni kuwa jana ni muda uliopita leo ni muda uliopo na kesho ni future.
#Lakini MUDA NININI? Na umetoka wapi?
Je wanadamu waliugundua muda au waliuvumbua?

Yapo mengi yakufikirisha, mfano tu ukiangalia mtu akipiga miayo na wewe dakika hiyohiyo unapiga mwayo.
Kwanini?
Kwanini tunapiga miayo?
Tukiwa na furaha tunacheka na tukiwa na huzuni tunalia.... lakini kwa nini?
Kwa kitambo tumekuwa tukiamini kuwa kicheko ni nyenzo moja nzuri ya kuonesha kuwa tuna enjoy kinachoendelea na hutuunga vyema na watu wengine.
Basi iaminike kuwa kicheko,
ndicho humpa binadamu upekee alionao, au àtleast tuseme primates. Lakini si kweli, wanyama wengi pia hucheka , papa wanacheka hata panya pia wanacheka.So Why Do we lough? Also why do we cry?
Kulia ni kama kuna nguvu ya tiba ndani yake. Kilio kina activate parasympathetic nervous system kuurudisha mwili kwenye hali nzuri. Sasa kama ni jambo zuri Kwanini tunalihusisha na mambo mabaya?
Tunalia kwa sababu jambo bala limetokea na sio wakati linatokea, Why? Ni kama ubongo unafanya interpretation ya bad events ndio tulie.
Halafu tena sometimes some peoples wanalia wakiwa na furaha. Kwahiyo yote nlosema hapo juu achana nayo maana sijui.
Kwanini wengine hutumia mkono wa kushoto wengine wa kulia.
Tuna theories kibao lakini ndo hivyo sasa, Theory ni theory tu...
Miaka ya nyuma iliaminika kuwa dunia ndicho kitovu , the center of the universe. Halafu ikagundulika kuwa sio.
Kisha kuna ambao mpaka leo wanaamini kuwa hiyo ndo ilikuwa sahihi.
Kuna chance kubwa mno kuwa kila kitu tunachojua kuhusu dunia ni wrong.
Hatujui kila kitu kuhusu kilakitu.