kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,931
- 7,828
Kila kitu sasa kiko ukutani kuhusu anguko la UKAWA. Kila chama mshirika kimesambaratika. Sio CHADEMA sio CUF wala NCCR mageuzi. Vyama vimevamiwa na mamluki waajiriwa wa tajiri anayedhani anaweza kununua urais wa Tanzania kwa hela yake. Baada ya usaliti wa viongozi wa CHADEMA wananchi wamegundua hila na mazingaombwe ya UKAWA wanangojea kutoa hukumu Oct 25 kwa kusema 'ndio' kwa Magufuli. Wasaliti sasa wanapigana vita gizani. Wanarusha ngumi bila kuona adui wanadundana ngumi wenyewe kwa menyewe. Kwenye mitandao ya kijamii wameishiwa hoja wanarusha magarasha tu.