Kila kitu sasa kiko ukutani

Kila kitu sasa kiko ukutani

Naomba nikukumbushe au nikuhabarishe kuwa watu wengi wamejiandikisha kwa nia ya kupiga kura bali ni kwa nia ya kutaka kupata vitambulisho vya uraia. Usijeshangaa pale ambapo watakaopiga kura watakuwa ni chini ya 50% ya wapiga kura wote. Rejea takwimu za chaguzi zilizopita.
Umewahi kuandamana na mgombea uraisi yeyote ukaona hali halisi ilivyo? Ni tofauti sana na chaguzi zilizopita!!
 
Mimi na nyumba yangu tutatumikia Ukawa to the last drop of our life.
 
Lowasa ndiye rais watake wasitake hawa mapimbii wa lumumba
 
Kila kitu sasa kiko ukutani kuhusu anguko la UKAWA. Kila chama mshirika kimesambaratika. Sio CHADEMA sio CUF wala NCCR mageuzi. Vyama vimevamiwa na mamluki waajiriwa wa tajiri anayedhani anaweza kununua urais wa Tanzania kwa hela yake. Baada ya usaliti wa viongozi wa CHADEMA wananchi wamegundua hila na mazingaombwe ya UKAWA wanangojea kutoa hukumu Oct 25 kwa kusema 'ndio' kwa Magufuli. Wasaliti sasa wanapigana vita gizani. Wanarusha ngumi bila kuona adui wanadundana ngumi wenyewe kwa menyewe. Kwenye mitandao ya kijamii wameishiwa hoja wanarusha magarasha tu.

Nilijipumzisha (kulala) chini ya mwembe kwa muda na ndiyo kwanza nimeamka. Mjukuu naye kanifanyia mzaha miwani kaificha hivyo najitahidi kusoma naona maluweluwe. Ebu nipigie uniambie umekusudia kuleta ujumbe gani?? Au unajaribu kupigana na kivuli chako???
 
Nilijipumzisha (kulala) chini ya mwembe kwa muda na ndiyo kwanza nimeamka. Mjukuu naye kanifanyia mzaha miwani kaificha hivyo najitahidi kusoma naona maluweluwe. Ebu nipigie uniambie umekusudia kuleta ujumbe gani?? Au unajaribu kupigana na kivuli chako???
ungelinawa uso kwanza halafu nitakupasha kuhusu hali tete ya ukawa.
 
Back
Top Bottom