Kila hoja moto bungeni, Kikao cha dharula wabunge wa CCM

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Kumekuwa na kawaida Katibu wa wabunge wa CCM kuitisha kikao cha dharula kila unapotokea mjadala mkali bungeni wa kuelekea kupinga hoja inayoletwa na serikali Bungeni. Matokeo ya kikao hicho ni aidha serikali kuiondoa hoja yake inapotokea wabunge wa CCM kuendelea kukataa kuiunga mkono katika kikao chao au wabunge wa CCM kukubali kuiunga mkono kwa msimamo mmoja. Hata leo baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu Mh Simbachawene alitangaza tangazo la Katibu wa wabunge wa CCM kutaka wakutane ni wazi ni juu wa sheria ya manunuzi vitu vilivyotumika. Hawawezi kukutana kabla ya kuupeleka Bungeni au wanakuwa wamekutana lakini wanabadilishwa na michango ya wapinzani na pili Utaratibu huu unawanufaisha kweli CCM kisiasa?
 
Bahati nzuri, bila wao kujua, utaratibu huo unawamaliza ccm, kwa kuwa hayo yanayajadiliwa gizani yanaondoa imani ya wanachi. Wananchi wanaona kama wanaburuzwa na serikali - nao wanakubali.
 
Bahati nzuri, bila wao kujua, utaratibu huo unawamaliza ccm, kwa kuwa hayo yanayajadiliwa gizani yanaondoa imani ya wanachi. Wananchi wanaona kama wanaburuzwa na serikali - nao wanakubali.

tena huko gizani wanachofanya ni kuambiana wakinusuru chama, chama kinachotutia hasara watanzania, sasa tutakizamisha chama na wote waliomo ndani watazama!
 
Hawana jipya hao 2mewachoka chama gan? Kabla sijazaliwa kilikuwa kinaongoza mpaka sasa kinaongoza bla mafanikio yoyote.Waiz 2 hao.
 
tena huko gizani wanachofanya ni kuambiana wakinusuru chama, chama kinachotutia hasara watanzania, sasa tutakizamisha chama na wote waliomo ndani watazama!

Hicho chama wala hakinusuriki tena! Wangekuwa na akili kidogo tu, wangekuwa wanazipima hoja zinazopinga jambo husika kama zina maslahi kitaifa au la na kufanya maamuzi sahihi badala ya kutaka kushinda katika kila jambo.
 
Hapo wananchi wanatakiwa kuwa makini sana na utaratibu huu unaofanywa na wabunge wa chama cha magamba-CCM,wamekuwa na tabia hiyo na wakirudi utasikia NDIYOOOOOOO,wendawazimu kabisa hawa watu.
 
Bahati mbaya kwao na nzuri kwetu kuwa wanazidi kupoteza mvuto kwa watanzania kwa mtindo huo wa kufanya maamuzi ya nchi nyuma ya pazia
 
Kila ninaposikia neno ccm naona chanzo cha ugumu wa ajira kwa vijana,kupanda kwa gharama za maisha,mauaji ya raia, mabomu ya machozi,ukandamizaji wa demokrasia n.k

Wewe unajisikiaje ukisikia neno ccm.
 
Back
Top Bottom