Kila hatua kwa CHADEMA ni hatua ya kusonga mbele

Kila hatua kwa CHADEMA ni hatua ya kusonga mbele

Ukisimama Nchale, Ukikaa Nchale .. chama dola kongwe kisicho chama halisi kinapitia wakati mgumu.

Hakika CHADEMA ndiyo chama kikuu cha siasa Tanzania.
Hakika... Na ndiyo maana wananchi wa kawaida wanaitegemea CHADEMA na kuiona kama Nuru kwenye maisha yao yaliyojaa giza, huku CCM wakiweweseka wakitafuta njia ya kupambana na nguvu ya ushawishi wa CHADEMA.
 
Ushindi Januari 2025, Mwezi Machi Mwenyekiti anaropoka maneno yanayoashiria uhaini na kisha akamatwa na kutupwa ndani
Uhaini ni vitendo sio maneno.

Ile ni kesi ya kubambikwa tu.
 
Hamtaki kuambiwa ukweli mnataka kusifiwa tu sasa mna utofauti gani na ccm
Kama huoni utofauti wa CHADEMA na CCM , basi Kwa CHADEMA hiyo ni hatua...

CHADEMA wanajua wapo watu wasiojitambua... Hivyo ukionesha kuwa wewe ni mmojawao, hiyo huwa ni hatua kwa CHADEMA.
 
CHADEMA wasiposema ni hatua na wakisema ni hatua.

Wakikamatwa ni hatua na wakiachiwa ni hatua pia.

Wakizuiwa kufanya siasa kimazabe ni hatua na wakiruhusiwa kufanya siasa ni hatua.

CHADEMA wakiizungumzia Tanganyika ni hatua na wakiizungumzia Zanzibar na hata wakiizungumzia Tanzania ni hatua zaidi.

CHADEMA wakishiriki uchaguzi ni hatua na wakisema No reforms No election kwao ni hatua pia.

CHADEMA wakiwa wengi ni hatua na wakiwa wachache ni ishara kwao kuwa hiyo ni hatua.

Ukijiunga CHADEMA ni hatua kwa CHADEMA na ukiamua kuhama CHADEMA nayo kwa CHADEMA ni hatua pia.
chama kikifa pia ni hatua
 
ccm unajua ni ya ngap duniani
Ona huyu sasa, hayo mambo yenu ya kusema CCM ni ya ngapi ni Propaganda ya kizamani Sana.

CCM ya ngapi kwenye nini na taasisi gani duniani huwa inapima vyama na kuvipanga?

Hii pia ni hatua kwa CHADEMA kuona wafuasi wa CCM huamini Kila wanachoambiwa na viongozi wao.
 
CHADEMA wasiposema ni hatua na wakisema ni hatua.

Wakikamatwa ni hatua na wakiachiwa ni hatua pia.

Wakizuiwa kufanya siasa kimazabe ni hatua na wakiruhusiwa kufanya siasa ni hatua.

CHADEMA wakiizungumzia Tanganyika ni hatua na wakiizungumzia Zanzibar na hata wakiizungumzia Tanzania ni hatua zaidi.

CHADEMA wakishiriki uchaguzi ni hatua na wakisema No reforms No election kwao ni hatua pia.

CHADEMA wakiwa wengi ni hatua na wakiwa wachache ni ishara kwao kuwa hiyo ni hatua.

Ukijiunga CHADEMA ni hatua kwa CHADEMA na ukiamua kuhama CHADEMA nayo kwa CHADEMA ni hatua pia.
Chadema ni kama maji usipoyanywa utayaoga.

Chadema haikushiriki uchaguzi lakini chama kinachoongelewa zaidi ni Chadema kuzidi vyote vilivyoshiriki kikiwemo CCM.
 
Back
Top Bottom