Kila biashara ina changamoto zake

Wasalaam jamii,

Binafsi nishafanya biashara kadhaa tofauti,

Kuna hii biashara ya kukopesha nguo,viatu nk, ni biashara yenye faida nzuri lakini inachangamoto sana,

Na inahitaji uwe kauzu haswa, pale wateja wakisha kuzoea kukulipa wanakulipa kwa mazoea,

Unakuta mwingine muda umefika wa kulipa deni,atakuambia nikipata nitakulipa,hiyo usihesabie kabisa,

Inafika kipindi bidhaa zimeisha na watu wanahitaji bidhaa na pesa zipo mikononi kwa watu,

Hivyo unaweza ukadai pesa yako na ukajiona msumbufu,

Kama hauwezi kudai hii kitu usifanye,bora uuze ata chakula kikibaki utakula mwenyewe.
Kuna biashara za wanaumme na wanawake, kama hiyo mtu mwenye focus siwezi kuifanya, ntakopeshaji mtu wakati hamna guarantee ya kulipwa hana bima hiyo biashara hapana.
 
Hii naona ni biashara ya kufanya kwa kiwango cha chini kabisa

Unampa mtu nguo anavaa hajakulipa, asipokulipa unamfanya nini?

Bora hata hiyo pesa ikopeshwe kwa riba kwa microfinance au hata uweke UTT utapata kagawio na usalama wa pesa yako unakuwepo
 
Back
Top Bottom