Kila aliyezaliwa anapenda sifa.

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Kuna tabia au hulka ambazo binadamu huzaliwa nazo na kuna zile ambazo mtu anazipata anapochangamana na watu mballimbali katika mazingira aliyopo.
Ukiachilia mbali tabia ya kutopenda kulaumiwa. Binadamu anapenda sana sifa. Ni asili yake kutafuta kuwa maarufu au mashuhuri.

Kila binadamu anapenda aonekane wa tofauti kiutendaji na hata kimienendo. Anaweza asijitape kuwa Yeye anapesa sana sifa ila utaona viashiria vingi tu ambayo vitaonesha uhitaji wa kutambulika. Na ndio maana kila mahali utakapokwenda, katika kila kikundi cha watu utakutana na mtu mashuhuli. Bila shaka hata kwenye familia yenu kuna mtu mashuhuli au nadanganya?


Nakumbuka kipindi nasoma sekondari alikuwepo jamaa mmoja alifahamika kwa jina la umaarufu kama Jembe. Huyu Yeye alikuwa anauwezo wa kumaliza ndoo ya rita ishirini yenye uji wa mtama akiwa pekee yake. Alitumia mbinu ya mdgo mdgo mpaka kinaeleweka. Hivyo, watu walimfahamu sana...na hata kama ameshiba itamubidi ajikakamue ili asipoteze sifa yake.

Kuna wale ambao wao hawasikii bakora. Mwalimu atachapa achapavyo, atainua juu fimbo kama vile anavuta ndoano majini kisha kuiangusha makalioni Mwa mwabafunzi kwa nguvu. Unakuta mwanafunzi hata ashituki. Unaweza dhania labda hajaumia lakini wapi ni sifa tu ndio anataka. Hapendi onekana dhaifu mbele ya wenzako, hasa hasa mbele ya jinsia ya kike.

Ni kawaida sana siku hizi ukienda kwenye nyumba za ibada utakuta kuna wale viongozi mashehe au wachungaji ambao ni mashuhuli. Wao wakisimama na kuongea watu wanafurahia na kuitikia kwa moyo mmoja. Unakuta kuna viongozi wengine nyuma yao wanatamani na wao wawe kama hawa wabaokubalika. Yote haya yanalenga sifa tu Hanna kingine.

Mfano nzuri utakaokufanya udhibitisho kuwa binadamu kutwa kucha wanaangaikia umaarufu ni kwa namna gani watu wanavyotumia mitandao ya kijamii. Utakuta kijana yuko radhi aazime mavazi kwa rafiki zake..na mikufu ya kuvaa shingoni ili apigie picha tu. Kisha baadae kuzipost kwenye kurasa mbali mbali za mitandao ya kijamii kama facebook, Instagram na hata snap chat.

Unamkuta mdada mwenye umbile dogo, anabinua makalio yake kisha anapiga selfie ili angalau kuwaonesha wapenzi watazamaji kuwa na yeye analo.

Utakuta vijana wengi hasa hasa wa miaka ya tisini na kupanda juu, wanaiga kila jambo ambalo watu mashuhuli kama wasanii wanyoyafanya. Msanii akivaa heleni, unakuta na kijana mkaanga viepe naye kavaa heleni. Hii yote sio kwa sababu anapenda sana msanii huyo Bali anataka na yeye awe na wafuasi (followers) wengi watakaokuwa wana like na ku-comment kila anachopost na ikitokea akikosa likes au komenti anafadhaika sana. Hii yote inadhihilisha jinsi gani kila mwanadamu anapenda sifa.

Sifa njema ni manukato lakini sifa mbaya ni uozo au matapishi ya mlevi. Usipende sana sifa kufikia hatua ya kupoteza akili. Penda sifa nzuri ambayo ni kwa manufaa yako na kwa jamii yako au familia. Mfano, wewe uliye shuleni soma kwa bidii ili ufaulu vizuri mathalani uwe wa kwanza kitaifa, ufurahishe ndugu, jamaa na hata jumuiya ya shule unayosoma.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom