Hotba yake nimeiangalia hadi mwisho japo alichelewa sana kufika uwanjani kwani ratiba ilionyesha kuwa shererhe zingeanza saa tano alifika saa saba kasoro robo.
Anajidai kusema kuwa vijana wasiwaunge mkono wanasiasa kwani wanataka kuwatumia kumwaga damu.
huu ni ushahidi kuwa amaanza kugundua kuwa vijana wameanza kuwatosa hao ccm ndio maana leo hotuba nzima iliwalenga vijana.
Pili aliposema kuwa kuna watu hawalitakii mema taifa hili,
1. hivi ni yupi halitakii mema taifa letu kati ya wale wanaosema ukweli na wale wanaoliibia taifa letu.
2. ni yupi anahatarisha amani kama sio yule anayekwenda kusaini mikataba kwa niaba yetu halafu anasaini vituko vya ajabu , buzwagi.
3.vijana , hawa ni kama wale wa wakati wa mwalimu Nyerere, kwani wakoloni nao walianza kutoa haotuba za aina hii kuwa wasiwaunge mkono wapigania haki ila kwa vile watu waliuona ukweli waliamua kumuunga mkono Mwalimu na wenzake.
4.ataweza tuu kuupata uungwaji mkono wa vijana kama ataweza kuwashughulikia wale wote wala rushwa .
Hotuba ya leo alijikita zaidi kwenye kuzungumzia ukimwi na kutoa siri kuwa wanaofadhili ujambazi ni wauzaji wa madawaq ya kulevya, aliuliza swali hili,
je, kwa mtu anayeishi maisha ya kawaida akipewa ama akipata milioni 100 si zinamtosha kuishi maisha yake yote,.
Swali langu kwake hivi wale first eleven walioiba zaidi ya 1.3 trilion wanaenda ama wamezifanyia kitu gani ,
Rais jua kwamba wananchi ndio wenye nchi na wana haki ya kumpa yeyote madaraka ya kuwaongoza, wanaweza kukipa chama chochote kwani wao ndio wenye mamlaka ya mwisho.
Wananchi wa leo wanaona jinsi uchumi unavyoliwa na vigogo huku kila siku wakiimarisha fence zao kwani hawataki hata maskini wasikie harafu ya kile wanachopika ,
Mwalimu ,nyerere angekuwepo leo sijui angeandika kitabu gani , kwani cha mwisho kilikuwa uongozi wetu na hatima ya Tanzania ,je , leo angeandika kuhusu nini.