Kikwete's most embarassing statements...

..........duuuuu, inatosha

Mbona ndio mwanzo tu game imeanza. Kina January Makamba na wenzake huko ikulu inabidi waeleze ni wapi walikuwa na nini walikuwa wanafanya wakati Kikwete akijionyesha utupu wake kwa watanzania.
 


Duh!
Ila jamaa anajitahidi sana kutoa kauli mkanganyiko.
Hivi huwa hana watu ambao wanamshauri cha kuongea mbeke ya kadamnasi?
 
Duh!
Ila jamaa anajitahidi sana kutoa kauli mkanganyiko.
Hivi huwa hana watu ambao wanamshauri cha kuongea mbeke ya kadamnasi?

aisee jamaa akicheza anaweza kuifikia record ya mzee Kenyatta hapo kwa watani zetu...
 
Ila kusema kweli, viongozi wetu wanahitaji kuwa 'serious' mara nyingine, hasa pale hotuba inapolenga wananchi (masikini), kwani kwao u 'seriousness' unaweza kuwafuta jasho...hata kama hawatarajii mabadiliko makubwa sana!
Franki
 
aisee jamaa akicheza anaweza kuifikia record ya mzee Kenyatta hapo kwa watani zetu...

Sure!
Mwingine mwenye kauli chafu sana ambaye alistahili kuwa katika kitabu cha Kumbukumbu ya Guinness ni mshitakiwa Basili Pesa2 Mramba!
Sijapata kusikia mtu mwenye kauli chafu kama mzee huyu, hasa katika utawala wa awamu ya tatu!
 
Mpaka sasa huwa najiuliza kwa nini huyu jamaa aliutaka sana urais. Ingawa pia nafahamu kuwa watu kama akina Rostam ambao walitaka huyu awe rais kuliko hata yeye mwenyewe alivyotaka. Tangu mwanzo niliwaonya watu washimshabikie huyu mtu kwa sababu nilijua hana uwezo, ni mswahili tu. Laiti Mwalimu angekuwa bado hai angalao mpaka 2005 bila shaka angetuepushia 'kikombe' hiki.
 
Huyu alishindwa kabla hajaanza hata huo urais! Ujasiri ni pale mtu unapoweza kujigundua kuwa kuna mambo mengine huwezi, inawezekana kuna mambo anayaweza kwa ufasaha kabisa, lakini hili la Urais angesema jamani inatosha, mnisamehe!


Huo ndio ukweli. Nitashangaa sana akiomba second term. Huyu anapaswa kukaa pembeni, imetosha! Miaka mingine mitano hapana, jamani. Tunataka mtu mwenye sifa zinazostahili, sio mswahili asiye na agenda yoyote katika kuipeleka nchi kwenye mafanikio.
 
Laiti Mwalimu angekuwa bado hai angalao mpaka 2005 bila shaka angetuepushia 'kikombe' hiki.

Braza Punch,
Ndo tushauvaa mkenge hivyo, kikombe tunakistahili kabisa, kwa miaka hii mitano! Ila mwakani nitapiga kura, ila simpi yeye, hata akishinda nitakuwa uhakika kuwa hakushinda kwa kura yangu!



Huo ndio ukweli. Nitashangaa sana akiomba second term.

Utashangaaje ilhali mwamuzi wa kugombea ama kutogombea si yeye?
Kuna watu wanamwamulia, iwapo agombee ama la, na huwa anawasikiliza sana!
Watanzania tunajutia sana kumpa kura mtu huyu, asiyejua kuwa kwa nini nchi anayoiongoza ni maskini hadi sasa!
 

wewe upo kama mimi.......sijui ni lini watanzania tutabadilika
 
Lakini hata Mwalimu aliwahi kuuambia mkutano wa akina mama kwamba "uchumi wanao, wameukalia"! Na mzee Mwinyi aliwahi kuuongelea "ukuni" mmoja hauvishi chakula.
 
Ni pale aliposema " Kelele za mpanagaji hazimnyimi mwenye nyumba kupata usingizi" pale wapinzani walipokuwa wanapiga kelele kuhusu ufisadi.
 
Hata hivyo, amesema tatizo hilo halikutokana na uzembe wa mtu yeyote, bali ni mitihani ya Mwenyezi Mungu.

Oct 2006 JK
 

nakubaliana na wewe mkuu Buchanan, huyu bwana mimi alinimaliza kabisa aliposema kuwa haelewi sababu kwanini nchi yake ni maskini tena anazungumza mambo haya akiwa ughaibuni kwenye nchi za watu!! Kila siku toka enzi za Mussa nchi hii tunaimba kuwa tuna maadui wakuu watatu na mmoja wao ni umaskini; kwahiyo mtu unatagemea yeyote atakayeusaka urais wa nchi yetu kazi yake kubwa ni kutafuta jinsi ya kupambana na maadui hawa na huwezi kumshinda adiu bila kumjua na kutafuta mbinu za kumshinda. Inaelekea Jakaya aliusaka urais bila ya kujua akiupata ataufanyia nini zaiadi ya uVASCO DAGAMA!
 
Ni pale aliposema " Kelele za mpanagaji hazimnyimi mwenye nyumba kupata usingizi" pale wapinzani walipokuwa wanapiga kelele kuhusu ufisadi.

Alikuwa anadanganya tu .... kelele zimemnyima usingizi hadi anakimbilia nchi za nje kila kukicha!
 
Kali nyingi ya mheshimiwa raisi hii hapa!


Mjadala uendelee
 
Na pale aliposema anawajua wala RUSHWA akawapa muda wajirekebishe je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…