Amesahau kuwa hao wanaodai mapinduzi yanawanufaisha wachache ni watoto wa juzi na jana ambao kwa msemo mwengine wazazi wao ndio walioshiriki katika Mapinduzi hivi huyu Kikwete haelewi kuwa Abeid Aman Karume hakushiriki katika mapinduzi ?
Endelea kusoma vitisho vya Raisi wa Tanganyika.
JK:Wanaobeza maendeleo ni walevi wa tende
Salma Said, Zanzibar
RAIS Jakaya Kikwete amewaita wale wote wenye kubeza maendeleo yalipatikana chini
ya serikali mbili ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
zinazoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) walevi wa tende.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika Uwanja wa Demokrasia uliopo Kibanda
Maiti katika Mkoa wa Mjini Magharibi, alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa
wananchi waliokwenda kusikiliza mkutano wa hadhara baada ya kumaliza ziara yake
ya kutembelea mikoa mitatu ya Unguja.
"Watu wengine sijui wanakunywa tende maana mtu mzima na akili yake anadiriki
kusema hakuna maendeleo wakati anapanda gari hatikisiki kwa sababu ya barabara
zilizojengwa na CCM, manawe haugui na hafi kwa kuwa hakuna malaria. Lakini mtu
huyo anasema mpaka mapovu ya mdomo yanamtoka kulia na kushoto, we sema mfereji
unatoka maji, wao watasema mfereji utatoka maziwa, na kila siku wanashangaa kwa
nini hawashindi, jibu ni kwamba hawasemi ukweli," alisema Rais Kikwete na
kushangiliwa.
Alisema anashangazwa na watu hao ambao wamekuwa wakitumia rasilimali za nchi
zilizoletwa na CCM, kuendelea kubeza maendeleo yaliyofikiwa na Visiwa vya Unguja
na Pemba.
Katika hatua nyingine aliwaonya wale wanaochezea mapinduzi na kwamba kama
hawajitaki au hawajipendi basi wachezee mapinduzi, waone kama hawatashughulikiwa.
"Tuliahidi kuyalinda mapinduzi jee tumeyalinda au hatukuyalinda, kuna mtu
aliothubutu kuyachezea, Kama kuna mtu hajipendi achezee, kama kuna mtu hajitaki
achezee nasema mtu acheze na yote lakini sio mapinduzi," alisema.
Rais Kikwete alisema kuchezea mapinduzi ni sawa na kurejesha utumwa katika
visiwa vya Zanzibar na kwamba wana CCM lazima wayalinde na kuyaenzi na kwamba
hakuna yeyote atakayethubutu kuyachezea bila ya kuchukuliwa hatua.
Akizungumzia maendeleo yaliofikiwa chini ya uongozi wa CCM, alisema kuna makubwa
na yanapaswa kuheshimiwa kwa kuwa yamekidhi ilani ya chama hicho, iliyiotolewa
wakati wa kunajidai kwa wananchi katika uchaguzi wa mwaka 2005.
"Shehia zote za Unguja zina maji na kwa upande wa vituo vya afya mtu hawezi
kufika kilomita tano kabla hajakutana na kituo cha afya,hata mikoa ya Tanzania
bara haijafikia maendeleo kama hayo. Sisi kule bara tunataka kuiga hapa Zanzibar
tunataka tuhakikishe kila kilomita tano kuna kituo cha afya..
Nasema mwaka 2010 tutatesa hatuna sababu ya kushindwa, maendeleo yaliofikiwa ni
makubwa ninafurahi kuwa tulioyaahidi tumeyatimiza na mengine tutayatekeleza bado
tunaendelea," alisema.
Rais Kikwete alisema katika ziara yake amepata kuona mambo mengi aliyokuwa
ameyaahidi wakati wa kampeni zikiwemo kero za muungano.
"Ahadi yetu kubwa ilikuwa kufufua mazungumzo kwa viongozi wetu waziri mkuu na
waziri kiongozi kukutana ili kuzungumzia kero za muungano na kwa hilo nadhani
viongozi hao wameshakutana zaidi ya mara sita sasa kama kuna jambo hawajamaliza
basi ni mimi na mheshimiwa Karume tutamaliza," alisema Rais Kikwete.
Akirejea kauli yake aliyoitoa Kisiwani Pemba alisema ni kweli waliwamabia
wananchi kwamba wakati umefika wa wapinzani kushirikiana na serikali kwa kuwa
wabunge na wawakilishi hawana serikali na serikali ipo chini ya Rais Kikwete na
Rais Karume.