Alisema tangi hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua lita za ujazo 200,000, wakati lile la awali lilikuwa na uwezo wa kuchukua lita 20,000. Alisema Serikali ya Japan imetoa Sh milioni 106.8 wakati SMZ imetoa Sh milioni 30 na nguvu za wananchi ni Sh milioni mbili. Alisema huo ni mojawapo ya miradi 10 iliyoanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2000.
Naam, habari ndio hiyoRais Jakaya Mrisho Kikwete amewaambia wapinzani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuwa inaweza kuwachukua muda mrefu mno kupata nafasi ya kuunda Serikali, ama pengine wasiipate kabisa, na hivyo ni muhimu kwao kushirikiana na Serikali ya CCM katika kuwaletea wananchi wa Tanzania Visiwani maendeleo.
Hizo milioni 106.8 ni kwa ajili ya mradi mmoja tu wa tanki la maji.kwa hesabu za haraka haraka wahisani wametoa 106.8mil kwa mradi na miradi iko 10 kwahiyo makadilio ya jumla yote ni kati ya (1-2)Bil tokea mwaka 2000. mi nafikili gharama za kuifuatilia hiyo misaada inazidi misaada yenyewe! na rais amesahau kauli ya Mwakyembe kua watanzania sio wajinga tena.
Tatizo nnaloliona hapo ni pale ambapo watawala huwa kuna wakati hawaonyeshi tofauti ya ziara za kichama au kiserikali.
Ni kweli kabisa ,Raisi anaona kwa vile yeye ni Raisi akitumia ziara za Kiserikali kukisafisha chama chake atafanikiwa kumbe ndio anazidi kukizamisha nafikiri bado ana hasira za Butiama kupelekwa kapa sasa anawazamisha wenziwe kwa kwenda kuhubiri utumbo.
Nadhni huwa anajisahau kwamba yeye ni raisi wa watu wote hata hao CUF
Kamanda taratibu, Prez yupo Pemba na lazima aongee Kipemba ili afahamike...