Kikwete ziarani Zanzibar: Ahadi, vijembe, na maagizo

JAMANI HUYU BWANA NI RAIS WA TANZANIA SASA HUO MRADI SERIKALI YAKE IMETOWA KIASI GANI?
Ajabu rasilimali za baharini zte ni mali ya muungano lakini nchi inajengwa na SMZ na wahisani au sio taswira tunayopewa hapa?
 
What do you mean by that? Una maana Wapemba ndio mbumbumbu? wanaohitaji kudharauliwa? au waliozoea kudanganywa? Hapa mzee hukuwatendea haki wenzetu na ipo haja ya kufuta usemi wako.
Hamna haja ya kufuta usemi., wao (Wapemba) ni watu wa ajabu ajabu tu. Na Waachane na ile simu- na Tumpe sefu-. Wanahitaji waangalie nini maendeleo yao -sasa -wawe macho ndugu zetu hawa (Wapemba)
.
 
JAMANI HUYU BWANA NI RAIS WA TANZANIA SASA HUO MRADI SERIKALI YAKE IMETOWA KIASI GANI?
Ajabu rasilimali za baharini zte ni mali ya muungano lakini nchi inajengwa na SMZ na wahisani au sio taswira tunayopewa hapa?
Ngerkewa SMZ ni sehemu ya Jamhuri ya Muunganoiwa Tanzania (SMT). Unaelewa hivyo?
 
Ajabu ameenda kuisifia misaada wakati alitakiwa atoe tathmini ya serikali imekifanyia nini kisiwa cha Pemba,hivi hashangai nchi ya Pemba haina hata kiwanda wakazi wake wanaokaribia milioni hajui wapi wanapata feza ya kuwaendeshea maisha,wakati matibabu kwa fedha,elimu kwa fedha na kila kitu kwa fedha umeme wa jenereta kama hakuna umeme hakuna maji.Barabara hizo za pemba ambazo hazizidi hata kilomita 40 zinajengwa na serikali za CCM tokea nchi zipate uhuru mpaka leo bado kila Raisi anakwenda kukagua barabara hizo,Waziri nae anakagua barabara hizo hizo.
Ujinga mliokuwa mnadhania wanao Wapemba jueni kwamba umeshawatoka sasa wanapigania utawala wao na Mkapa nae anapelekwa kwenye mahakama ya kimataifa taratibu zipo mbioni. Mpaka kieleweke.
What do u mean by utawala wao? Kwani hivi sasa hawajitawali? Si wana wabunge wamechagua wakina Hamad Rashid . Si wana wawakilishi wakina Abubakar. Au unataka lazima Sefu awe Rais ndio useme kuna utawala wao?
 
Kwa mtazamo wangu, tatizo sio Mheshimiwa Rais Kikwete au Amani Karume. Taizo sio Salmin Amour au Mkapa wala Ali Hassan Mwinyi. Tatizo la Tanzania kwa jumla ni CCM na sisi Watanzania wenyewe.

Tunapokwenda uchaguzini tunaambiwa na CCM yenyewe, tuchague Chama na sio mtu. Sisi tukienda tunachagua sura ya mtu. Ati, Kikwete anamvuto na kadhalika.

Tunajidanganya kwamba hii ni serikali ya Nyerere, na ile ni ya Mwinyi. Hii ni serikali ya Kikwete na ile ilikuwa ya Mkapa. Ukweli wenyewe ni kuwa serikali tangu tuache kutawaliwa na serikali ya Uingereza, tumetawaliwa mfululizo na TANU/CCM.

TANU/CCM imechukuwa nafasi iliyowachwa wazi na Mwingereza. Kusema kuwa tunajitawala wenyewe ni kujidanganya. Tunatawaliwa na TANU/CCM.
Mbunge unayemchagua amewekwa na chama na akienda Bungeni anakwenda
kukiwakilisha chama. Sio wewe uliyemchagua.

Akienda Bungeni kuwasilisha ya waliomchagua ambayo yanapingana na maslahi ya chama chake, anawekewa vizingiti vya kufukuzwa katika chama hicho. Akifukuzwa na Ubunge wake unakwisha. KATIBA inalinda chama, wala
haikulindi wewe mpiga kura. KATIBA imesukwa kwa maslahi ya chama. Na chama hicho ni kile cha CCM wala si kingine.

Katika nchi iliyo HURU, mwananchi yeyote anayetaka kugombea uongozi, tangu ule wa kata mpaka ngazi ya Rais, anakuwa huru kufanya hivyo awe na chama au asiwe nacho. Na haitokei mtu huyu akazuiliwa na chama chake. Atakataliwa au atakubaliwa na wananchi wenyewe. Chama hakina haki ya
kumwekea mwanachama wake vizingiti.

Katika nchi iliyo HURU mwanachama halazimiki kumpigia kura mgombea wa chama chake. Anakuwa na uhuru wa kumpigia mgombea anayemwona anafaa kuwakilisha anayoyataka yeye yawakilishwe Bungeni. Atamchagua anayemtaka awe wa chama chake, chama kingine au mgombea binafsi.

Matatizo nchini Tanzania hawayapati watu wa Pemba tu peke yao. Wananchi wengi katika sehemu nyingi wamechoshwa na mizengwe ya CCM. Lakini, wenzao wa Pemba wamekuwa wajasiri zaidi.

Mpaka tutakapoamka na kumaizi kuwa tatizo ni TANU/CCM na mfumo wake na sera zake na KATIBA za kujipendelea , tukajijumuisha na sisi wenyewe, ndipo tutapoacha kuwalaumu au kuwasifia watu binafsi kama akina Nyerere, Mwinyi,
Mkapa na Kikwete.

Ipo haja ya Watanzania kujikomboa. Bado hatujajitawala wenyewe, mpaka pale tutaposhika HATAMU za nchi badala ya kushikiwa na vyama vya siasa.
 
...nilitaka kusema kwanini basi chama cha CUF kwa kusaidiana na wafadhili kisiwahamasishe wananchi wa Pemba kujiletea maendeleo yao, mara nikakutana na hili;

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya lami kati ya Mkoani na Makombeni katika mkoa huo wa Kusini Pemba, Rais Kikwete aliendeleza somo lake kwa wapinzani akisema:

"Ndugu wananchi, msije kudanganywa. Kazi ya maendeleo haiko mikononi mwa mbunge ama mwakilishi. Hii ni kazi na dhamana ya serikali zote mbili ya SMZ na Muungano. Mbunge hawezi kujenga barabara ya lami. Sisi ndio wenye dhamana kwa waliotuchagua na hata wale ambao hawakutuchagua.


"Tutofautishe kipindi cha uchaguzi na kipindi cha maendeleo. Tutambue kuwa siasa za uchaguzi ni siasa za uchaguzi, baada ya hapo mleta maendeleo ni serikali. Na hata baadhi ya watu wakinuna wakati tukipita, lakini ukweli ni kwamba serikali tunayo sisi. Anayewaongopea vinginevyo, mwambie hivyo sivyo.

...ina sound kama Political black-mailed, ama?
 
Hamna haja ya kufuta usemi., wao (Wapemba) ni watu wa ajabu ajabu tu. Na Waachane na ile simu- na Tumpe sefu-. Wanahitaji waangalie nini maendeleo yao -sasa -wawe macho ndugu zetu hawa (Wapemba)
.

Sasa hata wakimpa CCM itawasaidia nini iwapo hiyo CCM ndiyo inayowakandamiza kwa muda wote?
Jina lako tayari limeshanipa taswira ya wewe ni nani na sitegemei kuwa tunaweza kupata uadilifu wa suala la Wapemba kutoka kwako.
Liwalo na liwe lakini demokrasia ndio inawapa Wapemba haki ya kuchaguwa yupi wa kuwaongoza na pengine wanazo sababu za kumpenda Sefu. Kwani kiongozi wa pili kwa Tanzania si Mpemba lakini mbona hawana habari nae pengine naye hana habari nao.
 
Ngerkewa SMZ ni sehemu ya Jamhuri ya Muunganoiwa Tanzania (SMT). Unaelewa hivyo?

Si elewi na ninachoelewa ni kuwa SMZ ni serikali ya Zanzibar na hivi karibuni viongozi wake walishasema kuwa wao ni nchi kamili, sasa bado utabaki kuamini kuwa SMZ ni SMT?
Aidha nini maana ya sehemu kama kila kimoja kinajitegemea? Naomba ufafanuzi zaidi.
 
b Wafuasi wa CUF ndio wanaojisahau- Inabidi waelewe kuwa Kikwete ni Rais wao.

Kama ni mfatiliaji wa mambo ungekwisha sikia kauli za CUF wakimtaka kama Rais alete suluhu ya Zanzibar. Ushahidi gani unataka mwenzetu?
 
hopeless.gif
kuna uwezekano mkubwa wewe ndie Hopeless
 
Kikwete awasuta wanaomshutumu kusafiri nje
Mgaya Kingoba, Pemba
Daily News; Wednesday,January 21, 2009 @20:21​


“Wapo watu wanaosema kwenda nje tunapoteza muda, kwamba huko kwingine hakutuhusu…kunatuhusu sana. Maendeleo yana sura mbili, moja ni nguvu za wananchi na nyingine ni misaada ya kuchangia maendeleo yetu,” alisema Rais.

“Sasa ili kupata misaada hiyo ya maendeleo ni lazima utoke na ukutane na wahisani hao sehemu mbalimbali,” alisema Rais Kikwete jana wakati akizindua tangi la maji katika Shehia ya Kengeja katika Wilaya ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba, ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

“Japan hapa hajileti mwenyewe…Japan anawajua ninyi? Anawahusu nini? Japan anakuja hapa mpaka awepo mtu wa kuwatambulisha, ndio maana tumepata msaada huu. Ndiyo maana mwaka jana nilikwenda katika mkutano wa ushirikiano wa Japan na Afrika unaoitwa TICAD.



What do you mean by that? Una maana Wapemba ndio mbumbumbu? wanaohitaji kudharauliwa? au waliozoea kudanganywa? Hapa mzee hukuwatendea haki wenzetu na ipo haja ya kufuta usemi wako.
Hebu soma tena kabla ya kumaka maka
 
Amesahau kuwa hao wanaodai mapinduzi yanawanufaisha wachache ni watoto wa juzi na jana ambao kwa msemo mwengine wazazi wao ndio walioshiriki katika Mapinduzi hivi huyu Kikwete haelewi kuwa Abeid Aman Karume hakushiriki katika mapinduzi ?

Endelea kusoma vitisho vya Raisi wa Tanganyika.

JK:Wanaobeza maendeleo ni walevi wa tende
Salma Said, Zanzibar
RAIS Jakaya Kikwete amewaita wale wote wenye kubeza maendeleo yalipatikana chini
ya serikali mbili ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
zinazoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) walevi wa tende.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika Uwanja wa Demokrasia uliopo Kibanda
Maiti katika Mkoa wa Mjini Magharibi, alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa
wananchi waliokwenda kusikiliza mkutano wa hadhara baada ya kumaliza ziara yake
ya kutembelea mikoa mitatu ya Unguja.

"Watu wengine sijui wanakunywa tende maana mtu mzima na akili yake anadiriki
kusema hakuna maendeleo wakati anapanda gari hatikisiki kwa sababu ya barabara
zilizojengwa na CCM, manawe haugui na hafi kwa kuwa hakuna malaria. Lakini mtu
huyo anasema mpaka mapovu ya mdomo yanamtoka kulia na kushoto, we sema mfereji
unatoka maji, wao watasema mfereji utatoka maziwa, na kila siku wanashangaa kwa
nini hawashindi, jibu ni kwamba hawasemi ukweli," alisema Rais Kikwete na
kushangiliwa.

Alisema anashangazwa na watu hao ambao wamekuwa wakitumia rasilimali za nchi
zilizoletwa na CCM, kuendelea kubeza maendeleo yaliyofikiwa na Visiwa vya Unguja
na Pemba.
Katika hatua nyingine aliwaonya wale wanaochezea mapinduzi na kwamba kama
hawajitaki au hawajipendi basi wachezee mapinduzi, waone kama hawatashughulikiwa.
"Tuliahidi kuyalinda mapinduzi jee tumeyalinda au hatukuyalinda, kuna mtu
aliothubutu kuyachezea, Kama kuna mtu hajipendi achezee, kama kuna mtu hajitaki
achezee nasema mtu acheze na yote lakini sio mapinduzi,
" alisema.
Rais Kikwete alisema kuchezea mapinduzi ni sawa na kurejesha utumwa katika
visiwa vya Zanzibar na kwamba wana CCM lazima wayalinde na kuyaenzi na kwamba
hakuna yeyote atakayethubutu kuyachezea bila ya kuchukuliwa hatua.
Akizungumzia maendeleo yaliofikiwa chini ya uongozi wa CCM, alisema kuna makubwa
na yanapaswa kuheshimiwa kwa kuwa yamekidhi ilani ya chama hicho, iliyiotolewa
wakati wa kunajidai kwa wananchi katika uchaguzi wa mwaka 2005.
"Shehia zote za Unguja zina maji na kwa upande wa vituo vya afya mtu hawezi
kufika kilomita tano kabla hajakutana na kituo cha afya,hata mikoa ya Tanzania
bara haijafikia maendeleo kama hayo. Sisi kule bara tunataka kuiga hapa Zanzibar
tunataka tuhakikishe kila kilomita tano kuna kituo cha afya..
Nasema mwaka 2010 tutatesa hatuna sababu ya kushindwa, maendeleo yaliofikiwa ni
makubwa ninafurahi kuwa tulioyaahidi tumeyatimiza na mengine tutayatekeleza bado
tunaendelea," alisema.
Rais Kikwete alisema katika ziara yake amepata kuona mambo mengi aliyokuwa
ameyaahidi wakati wa kampeni zikiwemo kero za muungano.
"Ahadi yetu kubwa ilikuwa kufufua mazungumzo kwa viongozi wetu waziri mkuu na
waziri kiongozi kukutana ili kuzungumzia kero za muungano na kwa hilo nadhani
viongozi hao wameshakutana zaidi ya mara sita sasa kama kuna jambo hawajamaliza
basi ni mimi na mheshimiwa Karume tutamaliza," alisema Rais Kikwete.
Akirejea kauli yake aliyoitoa Kisiwani Pemba alisema ni kweli waliwamabia
wananchi kwamba wakati umefika wa wapinzani kushirikiana na serikali kwa kuwa
wabunge na wawakilishi hawana serikali na serikali ipo chini ya Rais Kikwete na
Rais Karume.
 
Hatari inakuja kwa kauli ya huyu Kikwete nchi iko hatarini kiongozi mkuu kama huyu lazima awe na lugha za hekima na busara lakini hii ndio hatari ya viongozi kama huyu Kikwete wanadhani kupata madaraka basi wamekuwa au kujifanya miungu watu.Nyerere alimtabiri zamani Kikwete kuwa bado hawezi kuwa Rais wa Tanzania leo tunayashuhudia.Vilevile Kikwete amesahau kuwaletea maendeleo wananchi iwe ni maji au barabara ndani ya nchi au sehemu ya nchi ni haki ya Rais wa nchi kufanya hivyo kiongozi kufanya jambo fulani kwa anaowaongoza si fadhila bali ni wajibu
ni haki na wajibu wa kiongozi kuwatumikia wala hakuna haja ya kiongozi kujigamba au kuwasumbulia wananchi............ Na kuijilabu kwa misaada majuu wanajua kama Afrika wanashida hivyo safari zake zisizokuwa na mpango asizitafutie sababu ,ila akae akijua akiondoka yeye basi watakaoshika madaraka watamweka kiti moto kama alivyomuweka Lowasa.Na ndivyo mfumo tulionao unavyoelekea.
 
Wapinzani waliposema kikwete ni msanii, hawakukosea. Anajua wapi aseme lipi ili kukidhi mahitajio yake ya kisiasa.

".......anadiriki kusema hakuna maendeleo wakati anapanda gari hatikisiki kwa sababu ya barabara zilizojengwa na CCM,........."

Hivi ni kweli hajui kwamba hizo barabara zote alizopitishwa yeye ktk ziara yake zilikuwa zinazibwa viraka usiku na mchana? I wish leo angetembelea maeneo ya mjini tu siseme apite barabara ya bububu kuelekea nugwi/kiwengwa n.k na barabara nyengine nyingi tu; maana mvua ya leo vile viraka vyote chaliii ukipata bahati mbaya ukaingia ktk shimo basi ukanunue spring mpya ili gari liende sawasawa la sivyo litatembea hali limelalia upande mmoja.

".........mwanawe haugui na hafi kwa kuwa hakuna malaria.........." Ni kiongozi gani wa nchi ameshindwa japo kwenda kuwatembelea wagonjwa hospitali? Angepita japo kwa dakika chache tu pale MMNAZIMMOJA Hospital aone wagonjwa walivyojazana ktk foleni ya kusubiria huduma.

"..........Lakini mtu huyo anasema mpaka mapovu ya mdomo yanamtoka kulia na kushoto, we sema mfereji unatoka maji, ......."
Asiekujua hakuthamini; binafsi ni mtu wa huko tz bara na hapa znz naishi pale ktk majumba ya Kilimani, hakuna jambo linalonikera kama issue ya kutopata maji kwa uhakika hata km unatumia water -pump. Sasa mheshimiwa mtawala anapowadanganya hadhira yake kwamba serikali imepiga hauta kubwa ya kusambaza maji wakati maji yenyewe hayapatikani sijui tusemeje kwakweli maana mtu mzima akiongopa kumwambia hapa umeongopa panakazi!!!! Kuna mradi ulifadhiliwa na Japan ukaendeshwa na KONOIKE wa kusambaza maji but huo mradi umepigwa KATAFUA nadhani wadau wa bara mmenielewa hapo. Mradu umeisha, wajapan wamesharudi kwao, fedha zishaliwa lakini adha ya majipo bado ipo.

Hivi ni kweli huku znz kuna-maendeleo ya kuigwa na watu wa bara????? Ingekuwa ni hivyo basi watu wa visiwani hasa Wapemba wasingepigana vikumbo kwenda kuwekeza tz bara; maan hali ni ngumu mno hasa kwa wafanya bishara wakubwa. Hivi mahala penye maendeleo ya kuigwa anaweza akaondoka mtu kwenda kuwekeza kiwanda cha saruji bara wakati saruiji inagomabiniwa kama njuu hapa znz?

Ni kweli mapinduzi daima maana kama mtu ameshindwa kutoa japo maji kwa raia wake; atatoa nchi kwa hao raia wake ili waongoze kwa usawa waaoutaka wao wananchi????

Mheshimiwa amewatangazi ahli ya hatari kama alivyotangaza Mr. Clean (Ben); then tujianaae kwa makubwa zaidi, maana vikosi vishaanza kuingia kwa gea ya sherehe za mapinduzi lakini hatujawaona kuondoka kwa wingi kama walivyokuja maana hizo sherehe zishaisha siku nyingi!!!!!!!

Aluta kontinua
 
Katika hatua nyingine aliwaonya wale wanaochezea mapinduzi na kwamba kama
hawajitaki au hawajipendi basi wachezee mapinduzi, waone kama hawatashughulikiwa.
"Tuliahidi kuyalinda mapinduzi jee tumeyalinda au hatukuyalinda, kuna mtu
aliothubutu kuyachezea, Kama kuna mtu hajipendi achezee, kama kuna mtu hajitaki
achezee nasema mtu acheze na yote lakini sio mapinduzi,
" alisema.
Rais Kikwete alisema kuchezea mapinduzi ni sawa na kurejesha utumwa katika
visiwa vya Zanzibar na kwamba wana CCM lazima wayalinde na kuyaenzi na kwamba
hakuna yeyote atakayethubutu kuyachezea bila ya kuchukuliwa hatua.
Naam, habari ndio hiyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom