Kikwete warudishie fedha maskini waliokuchangia.. please! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete warudishie fedha maskini waliokuchangia.. please!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 12, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Nimesikitishwa na kitendo cha Rais Kikwete ambaye kwa maneno yake alidai kuwa ana uwezo wa kulipia fomu za kugombea lakini alikubali kuchukua tufedha tudogo kwa maskini wa Tanzania ambayo yeye aliamini wamefanya hivyo kwa sababu ya mapenzi yao kwake. Maskini hawa ambao kwa mifano yake Rais kwenye mkutano mkuu walimchangia kuanzia shilingi 200 na fedha nyingine.

  - Vijana waliouza maandazi kumchangia shilingi elfu thelathini
  - Mama aliyetoa shilingi 200
  - Mtoto wa shule aliyetoa fedha za shule kumpa JK
  - na wengine wengi..

  Mimi ninaombi kabisa.. kama kuna fedha zozote alizochukua kutoka kwa maskini wa Tanzania kuchangia kuchukua fomu na kama ana mpango wa kuchukua tena fedha kwa maskini kama alivyoahidi (kwenye fomu za serikali) naomba chonde.. tafadhali warudishie.

  Jilipie mwenyewe kwani tayari una fedha za kutosha. Huna sababu ya kuchangiwa hata senti moja na maskini wa Tanzania.

  Ni ombi tu na ni ushauri lenye kufanana na lazima ya aina fulani; usiwafanye maskini wakamlilia Mungu mbinguni.
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  No Mwanakijiji maskini asiye jitambua si maskini hawa nia matajiri, hawa wametoa kwa malengo si unajua tena ni kama wamepanda mbegu na wanatarjia kuwa iko siku itaota.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Shalom hawa wengine wanafanya hivyo kwa sababu ya woga.
   
 4. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wamefuata maandiko. Sasa wanasubiri karama za Mkulu. Usije shangaa wale vijana 3 yatima wa pale Chamwino wakipata skolashipu na yule mama wa Shinyanga akijengewa nyumba na kupewa trekta kama sera ya kilimo kwanza. Na wale vijana wa UDOM has kale kajamaa kalikoongea kiswanglishi kakikilimiwa kutoka na elimu yake ya siasa ya jamii teh teh teh
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Woga na kutojua haki zao ndiyo maana tumeshuhudia mibaba ikicheza taarabu na hata yule mlokole mwezangu akikata viuno jukwaani, wengine wameanza kuiabudu CCM.
   
 6. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Umaskini na Ujinga wa mtanzania ndio mtaji wa CCM, eti JK anathubutu kutoa ushuhuda wa mwanafunzi aliyemcangia fedha ambazo kapewa na wazazi wake kwa ajili ya shule!!!! kama ni mwanangu angejuta, then ukute ni karo ya shule kheeee !! mifano mingine haifai kabisa, utafikiri anahadithia watoto wa chekechea bana !!
   
 7. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Naweza kugawa wana CCM katika magrupu haya.
  1. WanaCCM safi kabisa ila wamechoka na SIASA na hawaoni kama wanaweza - wameamua kupumzika ila wanalia kimoyomoyo, umri umewatupa na inawezekana hawana taarifa sahihi. Hawa ndo kweli wanasiasa ndani ya CCM bado wana itikadi yao. Na huenda wanahisi CCM ya sas inakwenda na wakati.
  2. Wengine ni wasafi ila hawana uhakika nje ya CCM kama watakula na kulala kama wafanyavyo.
  3. Hapa wapo wengi, baada ya kuja kundi la vijana kujiunga na kuamsha upinzani wengi wameenza kujau hasara wanazozipata kutokana na kuikumbatia au kuwa na CCM ila background zao ni chafu ila hawana mshiko ndani ya CCM. Wengi ni wafanyabiashara, wafanyakazi wa serikali. Wao na TRA au mabosi wao wanajuana na wakitoka kijani tu mambo hadharani na aibu itawashika. wote wanajuana na huenda kama SLAA akigombea hili kundi litapiga kampeni maana ulaji wao kwisha. Kuishi kwa kundi hili pia linategemea sana viongozi wa wilayani hasa DC OCD. Kwa sasa hili kundi ndo linaipata fresh kwani linachangia kampeni na CCM kwa kulazimishwa kiaina. Hawapati tija maana mambo yanabadilika na hawana impact yeyote kwenye sera. Hili kundi utasikia halimtaki huyu wala huyu ila wakijua tu na wakajipanga watachomoka pia huenda usiku huku mchana kule.
  4. Wazee wa busara sina maana kuwa niwachawi ila hawajaona namna gani ya kuisaidia maana wana imani kuwa labda upinzani uungane au hawajatosha..... Kinachonitia moyo ni kuwa akisimama SLAA wanasema lazima mapinduzi iyatokee. Hili grupu ni lile ambalo hawana nafasi ndani ya ccm ila walijikuta humu baada ya vyama vingi. hawa wameathirika na rushwa kubwa au ndogo au madaraka kutumiwa vibaya. Kuna wengine wana hata nguvu kibiashara lakini woga wa asili umewapumbaza.
  5. Vijana safi kabisa ila baba zao na mama zao au walezi wao wapo na nafasi za juu pamoja na marafiki wao au walikuwa exposed kwao. Hawa wazazi huo ni wezi na kwame hawawezi kuwaambia jinsi walivotajirika. Huwa nao wanajitahidi kufikia mafanikio na wanaamini ndani ya CCM ndo itakuwa. Wapo waliona nia safi e.g. Nape na wengine hawajui. Kinachonishangaza ni kwanini wanang'angania. Hili grupu pamoja na sisi ndo wapo au wako hatarini kutekwa na kundi ndani ya ccm (bado nalifanyia kazi). Huenda CCM wameamua kuliteka hili na pia wale wapinzani waliokulia huko kama mimi, Zitto hawa ndo wanatumia kutujua strength husika.
  6. Wezi na walarushwa either ya moja kwa moja au kupitia. Wana makampuni yao yanafaidi tenda na wengine wanakula straight money. Hawa maisha yao, kula kwa ni kusimama kwa CCM. Ni ngumu sana hili group kuhama na wanatuaminisha kuwa hata haya maneno ni wivu tu wakike ila rohoni wanajua ukweli.
  7. Mwisho kuna grupu la wale walioingizwa choo cha jinsia tofauti na wanajutia kuingia kwao. Wanatamani sana kuomba radhi ila muda haujafika ila angekuwa JKN wangeshafanya na kama watafanya sasa watapata credit ila watakuwa hatarini.
  8. Wengi hapa hawajuni nini wala nini CCM ni kama vile matangazo ya bia, sigara, habari za vita. Just for leisure. maisha yao yote wamemwachie Mungu awalinde, wapo tayari kusukumwa na kibaya zaidi vimeingia mpaka chuo kikuuu. hii inanipashinda kuamini lakini huenda wapo pia grupu la 6.
  Kundi wa vijana wasomi na wafanyabiasha safi wa wenye kujua haki zao ni tishio kwa CCM na wanahijua hilo na lile kundi la 6 ndo ajenda yao na kichwa kinapasuka kwa ajili hio.

  asante kwa leo ruksa kujadili
   
 8. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tatizo kubwa lililopo Tanzania ni elimu ya raia ambayo inatufanya wengi tusijue tuyatendayo. Lakini unaweza kuangalia katika upande mwingine yawezekana pesa hizo walipewa ili wakazitoe ili kwa jamii ionekana kwa JK kachangiwa.
   
 9. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sidhani kama aliwalazimisha ila sio fresh kwa jamaa kupokea ni dhambi.
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  MKJJ bana!!!
  Mkuu arudishe ili iweje? CCM wanajua dawa ni kutafuta sympathy kutoka kwa wananchi; wanajaribu kuonyesha CCM bado ni ya jembe na nyundo!!!

  Wana uhakika nyuma ya pazia hakuna mwenye uwezo wa kufika ajue yaliyopo, ndo maana uteuzi wa candidates ndani ya CCM ni kwa kupanga na kupeana!!! Si umeona walikotoka... toka prezidaa ZNZ hadi makamo wa rais.
   
 11. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,503
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji
  Hapa unakuwa a bit extra-ordinary radical. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Hiyo ilikuwa ni mibaraka kwake. Mibaraka si kwamba inapatikana kwenye nyumba takatifu tu km vile misikiti na makanisa, inapatikana kutoka kwa watu pia, especially ukiwasikiliza matakwa yao mema, wanapokuwa wako chini wakati wewe ukiwa juu. Kukataa michango ya watu hawa kungewasononesha sana na possibly wangeweza hata kujenga some sort of a hatrage kwake, ambayo si nzuri sana, ukilinganisha na kuikubali michngo ya hao maskini wenzetu!
   
Loading...