Kikwete: Waliochochea ukabila ndio wanachochea udini leo...

Status
Not open for further replies.

"Kuna watu hawana raha na utulivu na amani ya nchi yetu. Walijaribu kutufarakanisha kwa kutumia ukabila lakini hili lilishindikana na sasa wamegeukia dini. Lakini ndugu zangu moto wa dini hautakuwa na wa kuuzima na hautakuwa na mshindi,"

Kama walianzisha hoja la ukabila kwa lengo la kuwagawa Watanzania ikashindkana, ana maana gani ama tumuelewe je yeye kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu kusema hayo maneno ya rangi nyekundu niliyopigia mstari. Kwa maana nyingine mambo yanayotokea sasa yana baraka kutoka kwake na hakuna mwenye mamlaka ya kukemea mambo hayo ili apatikane mshindi.
 
Message sent and delivered,
WALIOCHOCHEA UKABILA/UKANDA NDIO WANAOENDEKEZA UDINI. BIG UP JK, atleast umeliona tatizo

Mkuu basi tanua zaidi hiyo busara na kumshauri rais awachukulie hatua kali hao wanaotaka kuangamiza nchi. Yeye hatakiwi kuishia kuwa shabiki kama wengi tulivyo humu JF. Yeye ni rais wa nchi mwenye nyenzo zote za dola. Rais kuishia kutoa taarifa kwenye majukwaa ya kisiasa kama vile hao watu hatari wanaoeneza ukabila na udini "hawagusiki" wala "hawatamkiki" haitupi faraja hata kidogo!
 
Mwana Mpotevu Hii mbona iko wazi inawalenga CDM moja kwa moja, kwani wao ndio 90% ya viongozi wao wanatoka kaskazini, na sasa wameleta udini chini ya mwamvuli wa kanisa

Sasa rais anashindwa nini kuwachukulia hatua kali za kisheria ili atuondolee balaa hilo nchini? CDM ni nani hadi rais aishie kuwaimba kwa mafumbo kwenye majukwaa bila "kuwafanyia kazi" inavyostahili? Kiongozi wa nchi anawachekea watu wa aina hii?
 
mkuu wetu ameongea kana kwamba wananchi wanajua ukweli .kule zanzibar nani alimteka sheikh farid ni askari wetu .sio hawkusoma intelegensia kuwa vurugu zitatokea ?sheikh ponda nani kamtuma akavamie viwanja vya watu intelegensia ya kova haikuona .hapa ni kosa kubwa kufungamanisha vurugu hizi na vyama vya siasa ,sheikh farid ni cdm? ponda ni cdm pia ?tulinde maslahi ya taifa kwanza
 
Haya maandishi yameonesha kinyume cha jina lako!

Mwana Mpotevu Hii mbona iko wazi inawalenga CDM moja kwa moja, kwani wao ndio 90% ya viongozi wao wanatoka kaskazini, na sasa wameleta udini chini ya mwamvuli wa kanisa
 
Last edited by a moderator:
Ninachompendea rais wangu ni hiki, nae huwa anayaona matatizo kama tunavyo yaona wananchi wake, tofauti tu ni hii, sisi hatuna uwezo wa kuyatatua ila yeye hua anaouwezo lakini hautumii.

Natoa mifano:-
Nape Nnauye ameishawahi kusikika sio mara moja akiwaasa watu wasijuiunge na CDM kwa vile eti CDM ni ya wachagga, mwenyekiti wake alikaa kimyaaaa kabisa akijua ni upepo tu utapita, Radio Imani, vikundi kadhaa vya kiislamu vilifanya mikutano mingi tena hadharani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010, vilisema kwa uwazi kabisa, CDM ni chama cha kidini na Dr. Slaa ni Padre, rais wa wakati huo pamoja na msajiri wa vyama vya siasa walikaa kimyaaaa kabisa.

Twende Igunga, bakwata ikatia timu huko na kuwaasa waislam kutokumchagua mbunge wa CDM (wagombea wote wenye mvuto kumbuka walikua Wakristo pale Igunga) na kuawaelekeza Waislamu wamchague yule mgombea wa CCM, yote hayo serikali ilikaa kimya, mbegu ilipandwa na nyie wenyewe wacha sasa iote na hakika tutavuna hata ambao hatukushiriki kuipanda, ninacho sikitika, wengi mliopanda mbegu hii, wakati wa mavuno wenzetu mnaweza kukimbilia popote, sisi je?

Kwa kweli inasikitisha sana kuona kuwa swala la udini lilitumika sana kukandamiza demokrasia na kuacha kuchagua viongozi makini.
 
Kweli we ni wa kuonea huruma kabisa!

Haitaji phd kujua jk ana tapa tapa kutafuta huruma ya wananchi ili kujitoa kwenye dhambi waliyo ipanda!
Ni wewe peke yako usiye jua kuwa tumefika hapa kwa jili ya ujinga wa ccmweli na leo wana lia wenyewe majukwaani.

Walidhani kuzushia cdm ndio kunge iuwa kumbe walipanda mbegu ambayo mavuno yake tuna yaona!

Leo wanajifanya wanafiki kushangaa!

Mwana Mpotevu Hii mbona iko wazi inawalenga CDM moja kwa moja, kwani wao ndio 90% ya viongozi wao wanatoka kaskazini, na sasa wameleta udini chini ya mwamvuli wa kanisa
 
Last edited by a moderator:



“Kuna watu hawana raha na utulivu na amani ya nchi yetu. Walijaribu kutufarakanisha kwa kutumia ukabila lakini hili lilishindikana na sasa wamegeukia dini. Lakinindugu zangu moto wa dini hautakuwa na wa kuuzima na hautakuwa na mshindi,”
\
Hapa nadhani alikuwa anatania, mi sijawahi kuona mtu aliyefarakanisha watu kwa misingi ya dini zaidi ya kundi lake mwaka 2010





 
Jakaya kikwete na chama chake ni wahusika wakuu wa kusambaza chuki za dini na ukabila tanzania. Mungu anazidi kuwaumbua wanajitaja wenyewe.
 
Yeye ndie MWANZILISHI & this reflects he supports what his fellow muslim did & continue to do....

Badala akasemee Zanzibar hayo anasemea Kilimanjaro....??

Mbona anakosea sana....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom