GE2025 Kikwete: Wabunge wote wa Pwani bunge lijalo watatoka CCM, hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele

GE2025 Kikwete: Wabunge wote wa Pwani bunge lijalo watatoka CCM, hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho kikwete amesema kuwa anaamini Bunge lijalo wabunge wa Pwani wote watakuwa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na pia anaamini hiyo itakuwa Kwa Nchi nzima.

Dkt. Jakaya ameyasema hayo Leo Sept 28,2025 Kiwanja Cha Sabasaba Kibaha Mkoani Pwani Kwenye Mwendelezo wa Mikutano ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025 ya Dkt. Samia Suluhu Hassan

Aidha Dkt. Jakaya amesema kuwa watu wa Pwani hawapo tayari kuchanganya Pumba na Mchele kwani wanayajua madhara yake na hawatathubutu kufanya hivyo.
Huyu babu kageuza politics Simba na Yanga. Ushabiki tu.

One thing for sure, this is precedent

Msije mkatulaumu baadaye. Tuliwaonya
 
Sahihi kabisa,

Kama Upinzani hauwezi kupata mbunge hata mmoja kwenye mkoa mzima kama wa Pwani; unategemea nini...

Ukifanya analysis CCM wamekuwa na uhakika wa ku-sweep mikoa karibu 15 kila uchaguzi (hata ule uchaguzi mgumu wenye nguvu ya Lowassa + upinzania wa 2015).

Hauoni upinzani wote kwa ujumla mfano ukipata jimbo hata 1 kwenye mikoa ya Dodoma, Lindi, Mtwara, Tabora, Simiyu, Shinyanga, Pwani, Katavi, Ruvuma, Njombe, Tanga, Bila
Kusahau Singida (huwa wanapata jimbo 1 tu, Mwanza huwa wanapata jimbo 1 tu la Nyamagana, Mbeya huwa wanapata jimbo moja tu la Mbeya Mjini, Iringa huwa wanapata jimbo moja tu la Iringa Mjini (yaani hata Lukuvi hawamwezi), Rukwa wanaweza kupata jimbo 1 tu, Songwe wana jimbo moja tu la Tunduma.

Sasa imagine CCM wanaingia kwenye uchaguzi wana mikoa zaidi ya 18 wakiwa na comanding lead (solid green) inayotosha ku control Bunge..??? Na kumbuka Nchi yetu watu wanavote kwa tiketi - maana yake Uraisi pia automatically mgombea wao anapata.

Upinzani unatakiwa kupmbana sana aisee kujenga imani hasa kule chini, kule vijijini, kujenga wagimbea wanaoaminika,
Mzee unachekesha Yani wizi wote huo kumbe Huwa hamu uoni Sasa kilichowafanya mublock cdm na no reform no election Nini? Mpaka Sasa hivi mgekuwa tayari chali
 
Sijajua kama mambo yapo sawa, kauli hizi ni kama kuna tatizo zaidi ya lile twaona
 
Bado mikoa niliyoitaja CDM hawawezi kutoa ushindani wowote; (mfano mikoa yote ya Pwani na kusini - Ukitoa Dar, CDM hawawezi kupata chochote), mikoa ya kanda ya kati, mikoa ya Usukumani, Zanzibar yote na hata mikoa ya nyanda za juu kusini. Wana mikoa michache, majimbo machache sana ya Mara, Arusha, kilimanjaro, Manyara, Songwe, Mbeya, labda Geita kidogo sana, hata Kigoma - hawana nguvu. unajua shida kubwa watu wengi wana mhemko hawafanyi analysis bila kuegemea kwenye upande.

Ukisikiliza interview ya Fr. Kitima na jambo TV alisema bado CCM wana comanding lead ya over 70% ukifanya analysis. Tatizo CCM wanataka kushinda asilimia 90+ huo ndio mgogoro wanaojitengenezea.
Kanda ya kati? Hiihii?
Kabka kina heche hawajafungiwa pis uliona dodoma kilichowaogopesha wahusika ni nn?
Unafikiri mpk ss wangekua wsliendelea na ile mikutano ingekuwaje mpk ss?
AMini ht huko sio kwamba wanawapenda wanalszimishwa tu kukiwepo uhuru tutashangaa
 
Sasa Mkuu, unaongelea Dodoma Mjini? Vipi mikutano yake Kongwa? Kondoa? Chamwino nk ilikuwaje? - kama kwenye mkoa mzima ukishinda jimbo la Dodoma mjini tu then CCM inabeba majimbo
Mengine 9 kunakuwa na uwiano gani hapo?

Changamoto ni kiwa CCM wanataka kushinda asilimia 90+ lakini wamgewcha tu nature ichukue mkondo bado wanauhakika wa kushinda over 70+ kucontrol Bunge na Halmashauri over 70+ . Waache tamaa tu
 
Huyu mzee mbona alikuwa poa tu akiwa Rais,maana upinzani ulishamiri kipindi chake cha uongozi.. vip amepatwa na nini? Au anataka ku mslead maza?
 
Mzee unachekesha Yani wizi wote huo kumbe Huwa hamu uoni Sasa kilichowafanya mublock cdm na no reform no election Nini? Mpaka Sasa hivi mgekuwa tayari chali
Mkuu,

Ukifanya analysis kimhemko utaishia kufedhehesha watu. Nenda tena sikiliza knterview nzima ya Fr. kitima na Jambo TV kwa makini.. (tatizo tunasikiliza vipnde tu vinavyotupa furaha).

Ni kwei kwenye majimbo yenye ushindani CCM huwa wanapata tabu sana, lakini ni machache sana hayafiki hata 40 (ndiyo maana huwa hawana presha kubwa hata wakiwa na mgombea dhaifu)

Mfano, U haguzi ukianza tu CCM kwa Urais wa JMT wnakuwa wana kura karibu laki nne za Zanzibar, CDM chini ya elfu 10. Hzio kura jnaweza kudhani ni significant.. lakini CDM itahitaji majimbo takribani 20 waongoze kwa margin ya 20,000 votes kwa kila jimbo..

Kumbuka majimbo ambayo ni ngome ya CDM - bado CCM anaweza kupta kura nyingi. Wakati majimbo ambayo ni ngome ya CCM - CDM huwa hapati kura za kutosha (gap huwa kubwa mno). Unategemea nini????

Jiulize wewe, uko mkoa gani? Halafu fanya analysis kwenye mkoa wako Perfomance ya CDM ikoje? Kama kuna majimbo 10 kiuhalisia wanaweza kupta majimbo mangapi??? dar es Salaam yenyewe, hawawezi kupata majimbo yote; sasa unategemea nini?
 
Huyu mzee kwa sasa, siyo tu hana faida, bali ni hasara kwa taifa. Ajumuishwe kwenye ile orodha ya watakaopelekwa ICC.
 
Pwani yenyewe sasa baada ya miaka 60+ ya uhuru iko duni, na watu wake ni duni zaidi. Kwenye jimbo ambalo yeye amkuwa Mbunge mpaka Rais, na kijana wake bado ni mbunge pakoje?
 
Unavyofikiri na dhamira yako ya ndani kabisa kwa uwazi serikali hii na dola yake ina nia ya kweli kuhusu vyama vya upinzani.. kwa wanayofanyiwa unadhani watakuwa lini ?
 
Mwaka 1975 bunge na Serikali ilikuwa chini ya Tanu, vipi kulikuwa na chochote kilichobadirika

Mwaka 2020 asilimia 99 ya Wabunge walikuwa ni wa Chama kimoja, vipi kulikuwa na mabadiriko yeyote ya kimaendeleo?

Wakiona hawahitaji Vyama mbadala, wavifute tu tuishi Mwaka 2025 kama 1985 🙌
 
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho kikwete amesema kuwa anaamini Bunge lijalo wabunge wa Pwani wote watakuwa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na pia anaamini hiyo itakuwa Kwa Nchi nzima.

Dkt. Jakaya ameyasema hayo Leo Sept 28,2025 Kiwanja Cha Sabasaba Kibaha Mkoani Pwani Kwenye Mwendelezo wa Mikutano ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025 ya Dkt. Samia Suluhu Hassan

Aidha Dkt. Jakaya amesema kuwa watu wa Pwani hawapo tayari kuchanganya Pumba na Mchele kwani wanayajua madhara yake na hawatathubutu kufanya hivyo.

Inaelekea huyu Mzee ndiye Mchawi pekee aliyebaki huko CCM.
 
Siasa zina nyakati JK wa 2009 akikutana na huyu watuana Sema JK hapa anaongea kama CCM sometimes namuelea
 
Back
Top Bottom