Kikwete: Vyama vya upinzani ni vya msimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Vyama vya upinzani ni vya msimu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TandaleOne, Sep 9, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Thursday, 09 September 2010

  Waandishi Wetu

  MGOMBEA urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete ameviponda vyama vya upinzani akisema kuwa huibuka wakati wa uchaguzi tu, ukimalizika vinayeyuka. Kauli hiyo aliitoa jana katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika majira ya jioni katika uwanja wa Azimio mjini Handeni, Tanga na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu waliokuja kumsikiliza.

  "Chagueni kwa mafiga matatu, rais, mbunge na diwani wote wa CCM. Sisi ndiyo wenye uwezo mkubwa wa kuwaletea maendeleo ukilinganisha na wa vyama vya upinzani ambao huibuka wakati wa uchaguzi mkuu pekee, wakishindwa wanapotea," alisema Kikwete na kuongeza.

  "Wao wanategemea kupata nguvu kutoka kwa wanachama wa CCM ambao walikigombea katika kura za maoni wakishindwa wanachukia na hukimbilia kwao," alisema. Kikwete aliwaomba wananchi nchini kote kuwachagua wagombea wa CCM katika ngazi zote kwa kuwapigia kura ili waweze kipindi kuingine cha miaka mitano ijayo. Akizungumzia mafanikio ya serikali yake wilayani Handeni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Kikwete alisema ni kuongezeka kwa shule za sekondari.

  Kikwete alisema wakati anaingia madarakani mwaka 2005, wilaya hiyo ilikuwa na sekondari 11 sasa zimefikia 30 na kwamba idadi ya wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza kwa sasa wamevuka lengo na kwa zaidi ya asilimia mia moja.

  "Awali ilikuwa wakati wa matokeo ya mtihani wa darasa la saba ilikuwa ni kilio kwa kila kaya kutokana na wanafunzi wengi kufanya vibaya, lakini sasa wakati wa matokeo hayo kila nyumba sasa ni kicheko kutokana na watoto wengi kufaulu mitihani yao," alisema Kikwete.

  Rais Kikwete alisimama na msafara wake kwenye vijiji vya Kimbe, Viadigwa, Masagala na kufanya mkutano mkubwa Songe katika jimbo la Kilindi, mkoani Tanga ambapo aliahidi kuwaboreshea zaidi sekta za afya, elimu, kilimo, maji na mawasiliano. Akiwa Songe alizungumza na maafisa wafugaji na kuwaambia kuwa ataboresha pia malisho ya mifugo ili kupunguza wafugaji kuhama hama hovyo kwasababu ya kusaka malisho hatua ambayo wakati mwingine husababisha mapigano kati yao na wakulima.

  SAU, DP waungana kufungua kesi

  Wakati huo huo, vyama hivyo vya Sauti ya Umma (Sau) na Democratic ( DP), vinatarajia kufungua kesi hiyo ya kikatiba Mahakama Kuu leo kuiomba mahakama isimamishe uchaguzi huo Chama cha SAU kinachoongozwa na Paul Kyara na DP, Mchungaji Christopher Mtikila, vimeungana kesi hiyo baada ya kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuwania nafasi ya urais.

  Kesi inayopangwa kusimamiwa na wakili Israel Mgusi, ilitarajiwa kufunguliwa jana mchana, lakini ilishindikana kutokana na taratibu kadhaa kutokamilika. Katibu Mwenezi wa Sau, Johnson Mwangosi aliliambia Mwananchi kuwa watafungua kesi hiyo leo asubuhi chini ya kiapo cha dharura.

  Alisema katika kesi hiyo inayopinga hatua za Nec kuwaondoa katika kinyang'anyiro cha urais na kwamba wameandaa hoja 19 kutetea ombi lao la kuitaka Nec isitishe mchakato huo. SAU na DP vimeondolewa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kudaiwa kushindwa kutimiza sharti la kuwa na wanachama 200 kutoka kila mkoa kwa mikoa kumi nchini.

  Alisema moja ya maombi yao ni kuitaka mahakama hiyo isitishe kwanza kampeni za urais zinazoendelea hadi kesi hiyo itakapomalizika na wao kuruhusiwa kushiriki. "Sisi ni washiriki halali katika uchaguzi huu, lakini kwa kuwa Makame (Lewis Mwenyekiti wa Nec ) ametuengua bila sababu za msingi, sasa tutaiomba mahakama itamke kuwa sisi ni wagombea halali katika uchaguzi huu; "Tutafungua kesi hii chini ya hati ya dharura na baada ya kuwasilisha hati ya madai yetu tutaiomba mahaka isimamishe kwanza uchaguzi hadi tutakapotendewa haki," alisisitiza Mwangosi.

  Mgombea wa urais wa Sau, Kyara alienguliwa na Nec katika kinyang'anyiro hicho Agosti 19 mwaka huu kwa madai ya kushindwa kutimiza sharti la kuwa na wadhamini 200 kwa kila mkoa katika mikoa 10 nchini. Kwa upande wake Mchungaji Mtikila ambaye pia alikuwa ni mgombea wa urais kupitia chama chake cha DP, alienguliwa na Nec katika mchakato huo kwa madai kushindwa kutimiza sharti hilo la wadhamini kutoka mikoa 10.

  CUF wamkataa msimamizi wa uchaguzi

  Wakati huo huo, CUF kimemkataa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Sengerema na Buchosa, Erika Msika na wakidai kuwa hawama imani naye kwa sababu ameshindwa kutimiza wajibu amekuwa akitumiwa na wagombea wa CCM.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Mwanza kuelezea ziara yake ya kampeni katika mikoa ya Kanda ya ziwa, Mgombea mwenza wa CUF, Juma Haji Duni alisema chama chake kimeamua kumwandikia Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kutokana na kutoridhika na jinsi alivyolishughulikia pingamizi alilowekewa mgombea wao wa ubunge, Mbaraka Saidi Chiru na mgombea udiwani wa kata ya Katunguru, Pelece Essau Balalukuliliza.

  Duni alieleza kuwa makosa ambayo yametumika kuwaengua wagombea wa CUF hayana nguvu, lakini pia msimamizi huyo amekuwa akiwashauri wagombea kujitoa (wa CUF) na kuwaacha wa CCM kuendelea na uchaguzi. "Kwa niaba ya chama change ninatoa tamko rasmi kuwa hatuna imani naye msimamizi huyo wa uchaguzi, kwa vile ametumika na CCM bila ya kuzingatia wajibu wake na kuwaengua wagombea watu" alieleza.

  Awali akitoa ufafanuzi wa rufaa hizo jinsi zilivyoshughulikiwa na maimamizi huyo, mkurugenzi wa siasa taifa wa CUF, Mbaraka Maharagande alidai kuwa katika pingamizi la mgombea ubunge, aliyetumika kumuwekea ni Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi, Roida Makopora.

  Lipumba amtibulia Mkuchika

  Naye mgombea wa urais kupitia Chama cha Wananchi, CUF Profesa Ibrahim Lipumba jana aliingia kwa kishindo wilayani Newala na kumponda Waziri wa Habari na Utamaduni, George Mkuchika akidai kuwa ameshindwa kutekeleza ahadi zake hasa kumaliza kero ya maji kwa wapiga kura wake.

  "Mkuchika ameshindwa kumaliza tatizo la maji, akidai kuwa eti Newala imeinuka kama meza hivyo maji hayawezi kupanda. Mbona mkoa wa Kilimanjaro una milima, lakini maji yanapanda? Bonde la Mto Niger linafafanana kabisa na Bonde la Mto Ruvuma, lakini wenzetu Niger hawana shida ya maji," alisema Lipumba.

  Aliongeza: "Ukitazama Dar es Salaam kuna chuo kikuu, Morogoro kuna chuo kikuu, Dodoma kuna chuo kikuu, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza kote kuna nvyuo vikuu, lakini mikoa ya kusini, anzia Pwani, Lindi na Mtwara hakuna vyuo vikuu. Mikoa ya kusini imetengwa. Mkiichagua CUF nitaweka mtu maalumu wa kushughulikia kero za mikoa ya kusini".


  Imeandaliwa na James Magai,Dar; Edwin Mjwahuzi, Kilindi; Frederick Katulanda, Mwanza; Hussein Semdoe-Handeni na Elias Msuya, Newala.

  Source: Mwananchi
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu mjamaa anashangaza kweli kweli? Ati anasema Chadema nacho ni chama cha msimu? Anasahau kwamba tangu Day One JK aliposhika nchi, serikali yake imekuwa inatolewa kamasi na Chadema Bungeni na majukwaani?

  Hataki kuamini kwamba Chadema imekuwa kama vile imewasha moto ndani chupi za viongozi wa CCM na serikali yake? JK anasahau Mwembeyanga, Richmonmd, Buzwahi, EPA, Tangold etc – zote hizi ni hujuma dhidi ya Watz masikini ambapo Chadema katika miaka mitano iliyopita imefanya kazi kubwa ya kuwafungua macho wananchi?

  Na kinara wa haya yote katika Chadema ni huyu mpambanaji anayeminyana na JK katika majukwaa ya kampeni na kuonekana tishio kubwa hadi kuwafanya CCM waanze kampeni za maji taka baada ya kuishiwa hoja?

  JK anasahau uchaguzi mdogo wa Tarime ambao baada ya kutumia mapesa na nguvu kubwa za dola waliishia kulamba mchanga? Au ule wa Busanda na Biharamulo ambazo CCM ilitolewa kamasi nyingi hadi wakatumia wizi kuiba kura?


  Hivi wananchi wanaamini kabisa Chadema ni chama cha msimu? Labda JK alikuwa na maana ya vyama vingine vya upinzani, na siyo Chadema! Nadhani wanaomuamini JK kwamba Chadema ni chama cha msimu ni makondoo tuuuuu!!!!!!!
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Rais anaahidi kuboresha malisho ya mifugo, how?

  ha ha ha ha ha ha ha ha ... JK ameishiwa ahadi, sasa nimekubali. Kuna mtu alitoa kichekesho cha ahadi kwamba JK atawanunulia meli watu wa Dodoma ilihali Dodoma haina ziwa wala mto. Sasa hapa anaahidi kuboresha malisho ya mifugo.
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jk anafikiri CCM haitokuja kuwa chama cha upinzani.
  Aulize KANU cha Kenya ndio ajifunze kuwa hata kwa CCM inawezekana.
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Hivi sheria inasema kuwa vyama vya siasa vingine mbali na CCM ni vya msimu? Tendwa daftari lako linasemaje kuhusu ili? Hivi CCM moja kwa moja inawasaidiaje wananchi? Nijuavyo mimi chama kinatumia serikali kuwatumikia wananchi na sio chama moja kwa moja!

  Nionavyo mimi usemi sahihi ni kuwa serikali ni ya msimu, ndiyo maana na CCM wanatafuta msimu mwingine wa serikali, vyama vya siasa ni vya kudumu! Na kama CCM ni ya kudumu na wengine sio, mabango ya nini? Kampeni za nini? Kuchafua wagombea wa vyama vingine kwa nini?
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana naye huyo mfamaji aendelee kutapatapa. Bado kidogo ccm kitakuwa chama cha upinzani!
   
 7. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  CCm ni chama pinzani kwa CHADEMA and Vice versa.
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Pia uwakilishi bungeni na kwenye udiwani in wa msimu. Mbona msimu uliopita katika uwakilishi kulikuwa na madiwani na wabunge wa upinzani? Huko sio kuonyesha uhai wa vyama vya upinzani?
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilimaanisha kutokuwa madarakani against walioko madarakani!
   
 10. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Illogical:becky:
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nonsensical!
   
 12. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Vipi.Hivi amesema hivyo?
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Tuma ujumbe huu kwa watu 50 thanks

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehe hehehe
  rais wangu anakoma mwaka huu
  Rais wetu (slaa) anasubiri kuapishwa baada ya ushindi wa kishindo oktoba
   
 15. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  kyabo nasikia nae kakimbia
   
 16. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Dreamers:violin:
   
 17. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Angezungumzia Mbulu hayo angekoma.

  ____________________________
  "TOBIKO DR. SLAA"
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kikwete, viko wapi vyama vya msimu?

  Na Hilal K. Sued

  AKIHUTUBIA mkutano wa kampeni mkoani Tanga wiki iliyopita, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete alisema vyama vya upinzani ni vya "msimu."

  Siamini kama Kikwete alilenga vyama kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) au Chama cha Wananchi (CUF), ingawa bila shaka alikuwa anataka wasikilizaji wake waamini hivyo.

  Aidha, Kikwete hawezi akasema, bila ya kutafuna maneno kwamba chama chake, hakipati tija yoyote kwa kuwepo wingi wa vyama vya upinzani.

  Duniani kote, hasa katika nchi hizi za Afrika, wingi wa vyama hunufaisha chama kilichopo madarakani.

  Kwa mfano, katika uchaguzi wa urais nchini Kenya mwaka 1992, Daniel arap Moi alishinda kwa asilimia 35 ya kura, huku wapinzani wake wakuu, Kenneth Matiba wa FORD na Mwai Kibaki wa DP, na vyama vingine vidogo, walipata asilimia 65 ya kura zilizosalia.

  Baada ya uchaguzi, Kenya ilibadili mfumo huo na kuweka sharti la mshindi kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

  Pamoja na kwamba mshindi wa uchaguzi anapatikana kwa wingi wa kura, lakini kuna kila dalili kuwa iwapo Kikwete atabahatika kushinda, ataweza kupata chini ya asilimia 50.

  Tukiacha hilo la wapinzani kugawana kura, kuna hili jingine la kuvifanya baadhi ya vyama kama mradi wa chama tawala.

  Wengi wa viongozi wa vyama hivyo huwa na uswahiba au "hununuliwa" na viongozi wa CCM ili kutoa kauli zenye lengo la kuvidhoofisha vyama makini vya mageuzi. Mifano ipo mingi na vinafahamika hata kwa majina.

  Kwa jumla, kauli ya Kikwete, kwamba vyama vya upinzani ni vya msimu haina mashiko. Kikwete na CCM yake, kwa mfano, hawawezi kusema kuwa CHADEMA ni chama cha msimu.

  Hawezi kusema, CUF ni chama cha msimu. Hawezi! Hii ni kwa sababu, mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Jamhuri, 21 Desemba 2005, Kikwete amekuwa katika wakati mgumu kujibu hoja za upinzani.

  Ndani na nje ya Bunge, serikali ya CCM na Kikwete mwenyewe, wamekuwa wakihaha kujinasua kutoka katika lundo la kashifa za ufisadi zinazoikabili serikali yake.

  Hakuna sehemu ambako CCM imejikuta katika hali ngumu kama suala la ufisadi; suala ambalo CHADEMA ilikuwa imelivalia njuga na kukitoa chama hicho kamasi kwa kipindi chote cha miaka mitano ya utawala wa Kikwete.

  Je, katika mazingira haya, Kikwete anaweza kusema CHADEMA au CUF ni chama cha msimu?

  Kama CUF ni chama cha msimu, nini kilichosababisha yeye na serikali yake kusalimu amri kule Zanzibar na kuicha CUF leo ikipepea kwa kujihakikishia nafasi ya kuingia serikali, iwe jua au mvua?

  Wala hakuna mashaka, kwamba ni CHADEMA na mgombea wake wa urais, wakati huo akiwa mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa iliyoibua na kuweka hadharani rasilimali za umma zinavyokwapuliwa na kikundi kidogo cha watu.

  Katika hatua moja, Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta aliwahi kunukuliwa akimtaka Dk. Slaa kutoa ‘vielelezo' alivyokuwa navyo. Alipowasilisha alidai kuwa ni feki na hivyo angemchukulia hatua za kisheria.

  Isitoshe, upinzani na hasa CHADEMA wameonyesha, na kwa ushahidi kwamba baadhi ya fedha zilizokwapuliwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zilitumika katika kampeni zilizomwingiza yeye madarakani.

  Hatimaye serikali ikakubali kusalimu amri na kuruhusu ukaguzi wa hesabu kufanyika katika akaunti ya EPA. Yaliyofumuka kuanzia hapo yanajulikana kwa wengi, kama siyo kwa kila mmoja, akiwamo Kikwete.

  Haya ufisadi katika Richmond ulipigiwa kelele na upinzani ukiongozwa na CHADEMA. Ni baada ya kushinikiza Bunge kuunda Kamati Teule kuchunguza tuhuma hizo.

  Yaliyotokea yanafahamika. Kwamba Edward Lowassa alilazimika kujiuzulu, tena kwa aibu.

  Hata pale ambapo Kikwete alipora majukumu ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP), mahakama na bunge, kwa kutoa msamaha wa jumla kwa watuhumiwa wa EPA, ni wapinzani waliomjia juu Kikwete.

  Je, kweli Kikwete anaweza kusema CHADEMA ni chama cha msimu?

  Ni upinzani uliokaba koo serikali katika ufisadi uliohusu uchimbaji dhahabu Buzwagi, ununuzi wa rada chovu na kwa bei ya kuruka, ukwapuaji mabilioni ya shilingi uliofanywa na makampuni ya Meremeta, Deep Green Finance Limited na ujenzi wa Minara Miwili BoT.

  Katika chaguzi ndogo za ubunge zilizofanyika katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, vyama ambavyo Kikwete ameita vya msimu, ndivyo ambavyo vilikitoa kamasi chama chake.

  Kwa mfano, matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Tarime, Biharamulo na Busanda, yameonyesha kuwa CHADEMA siyo chama cha kuchezewa.

  Kimsingi vyama vya upinzani haviwezi kubezwa kwa kauli za rejareja za viongozi wa CCM. Kuna mengi ambayo vyama hivi vimeyafanya na ambayo yameleta tija kwa wananchi.

  Bali tukijenga hoja kuhusu CCM, hicho ndicho chama kinachojisahau zaidi. Huwa kinachukua kila kitu na kukabidhi serikali na chenyewe kwenda likizo hadi uchaguzi mwingine.

  Wakati huo, vyama vya upinzani huwa vinaibuka na kuzama vikitafuta jinsi ya kukabiliana na "zimwi" mwishoni mwa miaka mitano. Tuseme kweli, nani wa msimu katika hali hii: CCM au vyama vya upinzani?

  CHADEMA au CUF vingekuwa vyama vya msimu, CCM ingekuwa imelala ikisubiri ushindi. Sivyo ilivyo.

  Angalia. CCM imejifunza kutumia helikopta kufika ambako ni vigumu kufika kwa magari au ambako ingetumia muda zaidi. Imepunguza siku za mapumziko za mgombea wake. Imekataa kukutana na wagombea wa vyama vingine katika mdahalo wa wazi.

  Wananchi wapigakura hawawezi kuamini kile anachosema Kikwete. Wanaona anasema uongo na mwisho wa waongo huandaliwa na wananchi waliochoka kudanganywa.


  Makala hii imetoka katika Mwanahalisi.
   
 19. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Vijiwe vya ruzuku.
   
Loading...