Twalb zubeir
Senior Member
- Feb 23, 2015
- 143
- 51
Rais Kikwete anapaswa kutenganisha uenyekiti wake wa Chama Cha Mapinduzi na Urais wa Jamhuri ya muungano alio nao kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti wa CCM taifa anaingiza Ushabiki kwenye suala linalohusu haki za kiraia za wananchi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mfano kauli yake ya kuwataka watu wanaohamasisha watu kulinda kura wazomewe ni kauli ya kichochezi isiyopaswa kutolewa na Mhe.Jakaya Kikwete. Kauli hiyo sio makini kutokana na kuwa ameadi kuwa kukusanyika ili kulinda kura ni kuvunja Sheria.
Je, Ni Sheria ipi itakayokuwa imevunjwa kwani uchaguzi huu si unaongozwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010? Sheria hiyo Kifungu cha 104(1) cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 kinasema hairuhusiwi kwa mtu yeyote kutumia picha,nembo au mavazi yenye rangi za chama fulani ndani ya eneo la mzio(Radius) wa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura.
Kwa hiyo watu kukusanyika eneo linaloanzia mita 201 haivunji sheria.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Jakaya Kikwete,Jaji Lubuva na IGP Mangu wanapaswa kusoma sheria vizuri.Tena Jaji Lubuva anasikitisha sana katika hili. Asome Sheria vizuri..
Baadhi ya maeneo mwaka 2010,pamoja na kuwa na mawakala wetu ndani bado baadhi ya wagombea wa chama tawala walitoroka na masunduku.Safari hii hilo halitawezekana.
Hilo la kukusanyika baada ya mita 200 halivunji sheria isipokuwa IGP na Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Jakaya Kikwete ndio wanaotaka si kuvunja sheria bali kuivunja kabisa katiba ya nchi hasa ibara ya 20 . Pamoja na ubovu wake ilionao, Katiba ya Nchi, katika Ibara ya 20 (1), imetoa haki kwa mtu au watu kuwa huru kukutana, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine kutoa mawazo hadharani.
Huku kuzuia watu kukutana siku ya uchaguzi inashabihiana na amri za tawala za kiimla zinazoweka curfew(Amri ya kutotembea) hasa pale nchi inapokuwa katika shinikizo kali la kisiasa ambalo maimla wengi ili kujiimarisha madarakani huweka Curfew.
Tangu lini kupiga kura katika nchi ya kidemokrasia kukaendana na jaribio la kukiuka katiba ya nchi hasa ibara hiyo inayotoa uhuru wa kukusanyika au kwenda popote ilimradi havunji sheria hasa hiyo sheria ya uchaguzi ibara ya 104(1) na (2)?
Vilevile, Natoa Raia kwa Tume ya Uchaguzi sasa itoe kauli dhidi ya Matamshi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano aliyotoa kuwa kuna wapiga kura Milioni 28 wakati Tume ilitangaza kuna wapiga kura Milioni 22.7 tu.
Inapotokea watu wenye dhamana wakafanya mambo yanayoashiria uvunjaji wa sheria hasa sheria ya Takwimu inayokataza kutoa Takwimu za uongo hadharani tunashindwa kuwaelewa malengo na dhamira zao katika kujenga taifa lenye haki, linalofuata misingi ya Utawala bora wa sheria..