Kikwete unamuogopa Mwakyembe

Kwa mawazo yangu hapa Presdaa kunuondoa Dr. Mwakembe hakuwa sahihi bora angeendelea.
 
Hapa kambi moja imeua ndege wawili kwa jiwe moja! Mwakyembe nyota yake kisiasa itafifia manake kuacha ishu ya Richmond bandari ni sehemu iliyompaisha na kumuongezea mvuto wa kisiasa kwa jamii! Labda alitaka kutangaza nia au kuna kambi alishachagua wakampeleka huko kummaliza nguvu!

Sitta tayari amejijenga vya kutosha kwenye medani ya siasa, na uzuri wizara yake ya awali haikuwa na mikiki mikiki sana ya kukagua miradi so alikuwa na muda mzuri tu wa kujijenga kisiasa jimboni kwake na kupima mvuto wake kwa wananchi. Sasa huko alikohamishiwa itambidi afanye kazi kweli kweli ili aonekane, najua hatakubali kugeuka uchochoro wa ufisadi na rushwa, japo mwanzoni hapa watampiga sana(hata Mwakyembe) mwanzoni alipigwa sana.

Tatizo kwa Sitta ni kwamba hadi akomae na ofisi azibe mianya yote ya rushwa atashindwa kukimbizana na muda wa kampeni zijazo sababu ya kubanwa na hii wizara mpya yenye changamoto lukuki. Kwahiyo mwisho wa mchezo Sitta atakuwa ashachoka na bandari na nguvu ya ku-concentrate kwenye uchaguzi ujao itakuwa ndogo(miezi nane tu imebaki kuelekea uchaguzi)

Hapa kashawamaliza hawa wote wawili kwa pamoja! Ni kazi kwao kuangalia wakomae na nafasi walizopewa au waendeleze ndoto zao za kutaka madaraka au kuwa upande wa fulani kumuingiza kwenye madaraka! Athari za makundi ndani ya chama ndio kama hivi sasa!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Tatizo la mwakyembe ni papara halafu ana ndoto za kufanya biashara. Ni hatari sana kupewa wizara zenye miradi..ni mpigaji kama wengine wala msijidanganye. Huyo hatakiwi hata kuwa waziri abaki kuwa mbunge tu aendelee kupiga kelele

Wewe unaongelea ndoto sie tunaangalia kitu harisi,kama unasema ana ndoto sa kuwa mfanya biashara bado zitabaki kuwa ndoto tu,sio kitu harisi,lakini sie tunaongelea kuwa kati ya watu ambao ndani ya ccm angalau wanajishughurisha basi ni pamoja na hyu jamaa!!!!!
Sasa wewe unaongelea ndoto bana hivyo ni vitu vya kufkrika na hatuwez kukaa hapa tunajadili kitu ambacho wew mwenyewe tukikuambia thibitisha utabaki kung'aa tu macho!?!:-(
Tunajadili kuwa pamoja na kuwa ccm imechafka but atleast the man was abit reacting negatively for wrong doers!!!
 
Jamani tumwache rais afanye kazi yeye ndo mwenye dhamana

Yeye pia ni binadam kuna mda anaweza kwenda tofauti,yeye sio mungu!!!! Mbona hatusemi wizara zingine?!,ujue hadi tunaongea inamaana kuna kitu hakijaenda sawa!!!!
 
Nia ilikuwa kumfifisha ila kuanzia sasa hii miezi chache iliyobaki tutasikia chochote kwenye wizara yake mpya maana ana maamuzi ya ukweli
 
Mimi sijafuhishwa mwakembe kutolewa wizara ya uchukuzi,na mheshimu JK yeye ndiye anajua nini achokifanya tumpe muda
 
alikuwa wazir wa tanzania sio kyela unapoona anafanya kaz ni kwa niaba ya watanzania milion 46 upo mku, acha ubinafsi ww na ukabila
 
 
Mkuu malafyale hiyo bandari ya Kyela inaunganisha vitongoji gani
 
Last edited by a moderator:
Teh teh teh Bandari ya Bagamoyo....
Maghembe na Miradi ya Maji jimboni kwake
.....Kyela nayo ni Tz hivyo kuitaftia Fund haikuwa Kesi kwa Waziri...... Kisiasa Jimbo kwanza.... Hv Hamjiulizi....Kawambwa pamoja na kuwa flop lkn Mkuu kakazanae? Ni Mipango tu
 
hv kuwa waziri wa serikali Hii maana yake ni umekuwa waziri wa jimbo lako?
 
Mwakyembe ha-allocate bajeti,halafu bandari ya kyela huwezi ifananisha na mwanza
 

100% hujawahi fika Kyela!
100% hujawahi iona Kyela ya Mbunge Mwakipesile na Mbunge Mwakyembe
100% hujui kama Kyela nayo ina bandari na ina meli mbovu na Mwakyembe kama Mbunge wetu hajawahi hata fika bandarini kuona tatizo wanalopata wapiga kura bandarini hapo
100% wala hujui Mbunge kwanza ahudumie matatizo ya wapiga kura wake kingine ndiyo kinafuatia

Kama mmnampenda Mwakyembe mshaurini agombee kwenye majimbo yenu,huku anajua hapiti hajafanya lolote kwa miaka yake hii 10

Then unapoleta hoja ACHA KUTUMIA LUGHA ZA KUKERA,tumia lugha nyoofu utaeleweka zaidi!Neno una akili wewe sidhani kama hapa ni mahali pale
 
Mwakyembe ha-allocate bajeti,halafu bandari ya kyela huwezi ifananisha na mwanza

Mwakyembe ktk miaka 10 Kyela hajafanya lolote zaidi ya usanii na porojo
Kyela tunamtoa hata yy anajua!Mbunge lzm uhudumie Jimbo lako kwanza mengine yanafuatia na hata kama bandari ya Kyela si kama ya Mwanza ndiyO USIFANYE lolote sababu sio kama ya Mwanza>
 
usijali sana atawaletea jumuia ya afrika mashariki huko huko kyela.
hahahahaha mkuu umeua!!!!
Kwahio sisi tusio na mawaziri maendeleo hakuna? Acheni hizo bana uwaziri sio wa jimbo bali taifa zima. Huu ubaguzi unaolazimishwa utatufikisha pabaya
 
Mkuu malafyale hiyo bandari ya Kyela inaunganisha vitongoji gani

Mkuu bandari ya Kyela maarufu kama Itungi Port ipo ktk kata ya Kajunjumele nyumbani kwa mama yake Mwakyembe!Ni Bandari ya asili ambayo haijachimbwa kina chake na ina mchanga mweupe unao anzia Mwaya kutambaa hadi Ikombe kwa upande wa pili!Ni bandari inayohudumia nchi za Msumbiji na Malawi lkn biashara imedorara sababu ya uchakavu wa meli zake MV Iringa na MV Songea!

Mwakyembe hapatani na wapiga kura wa kata hiyo sana kwa sababukuu 2: Kwanza ilikuwa ngome kuu ya Mwakipesile na walimnyima kura Mwakyembe uchaguzi wa 2005 na sababu ya pili ni uchafuzi wa mazingira wa meli za Malawi zinazoleta makaa ya mawe toka Mchuchuma na malori ya Mbeya Cement yana pakua makaa hayo toka pale kijijini yanaharibu sana mazingira!Wananchi wamemuomba Mwakyembe aingilie kati bila majibu

Wakati wa Mwakipesile bandari hii ilikuwa chanzo kikubwa sana cha ajira kwa wazawa
 
Hii nchi bwana, ukiwa waziri ni wa taifa. Ila Ukiwa mkuu wa nchi siyo wa taifa. Kwa mfano rais akipelekewa bandari kwao wakati nyingine ipo km 20 kutoka kwake ni sawa tu, kujengewa barabara kubwa kama iendayo mikoani ni sawa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…