Kikwete unamuogopa Mwakyembe


sidhani kama analysis yako iko sawa kwasababu inajulikana wazi kwamba taifa hili ni la limeshajifia
 

Pia yale mabehewa ya treni mapya ni mabovu....
 
Ali ahidi kuboresha TAZARA lakini mpaka anaondoka wafanyakazi wanadai mishahara ya miezi mitano na wizara inakwepa kuongea na wafanyakazi ...ngoja wamjaribu EAC
 

MKUU!
Analysis yako ni ya nguvu na inaonyesha undani wa mambo ambayo kweli tunapaswa kuyazingatia katika hili.

Hata hivyo, yapo mengine pia ambayo ni vema tukayaweka hapa na kujadili "objectively" pia kama unavyosema. Na haya ni kama yafuatayo:
1. Suala la Uchukuzi na usafirshaji linagusa maslahi ya watu wenye nguvu kubwa sana ya kiuchumi. Ukiacha viwanda vinavyotengeneza vifaa vya kijeshi, yaani silaha nzito nzito, (hasa kwa nchi zilizoendelea) hakuna sekta yenye nguvu ya kiuchumi kwa nchi kama ya kwetu kama usafirshaji. Hata nchi iwe na rasilimali nyingine za nguvu kama madini nk, suala la uchukuzi na usafirishaji ni uti wa mgongo wa miundo mbinu yote mingine.

Mwakyembe ameingia wizara ile na kukutana na mambo mazito kwelikweli kama uvujaji mkubwa wa makusanyo au makusanyo hafifu kwa uzembe, pamoja na rushwa za aibu kama zile za kupitisha unga kwenye viwanja vya ndege.

Data za kuonyesha udhibiti wa mapato aliouanzisha katika entry points zipo na zinaonyesha mafanikio makubwa tu.

Willingness ya uongozi wa juu serikalini kukubali kutenga rasilimali za ziada ili kuinua sekta ya usafirishaji pia imekuwa questionable. Mwakyembe alishapeleka Action Plan yenye strategies za uhakika za kuinua sekta ya usafirishaji, lakini hadi sasa hakuna aliyeisemea kwa nguvu na kuonyesha commitment ya kutaka iwe na mafanikio zaidi yake mwenyewe! Kwa nini?

Bandari, Viwanja vya ndege, mashirika ya uchukuzi, vyote vinahitaji umakini na msukumo wa dhati wa uongozi uliopo, sio mtu mmoja lakini viongozi wa juu wa chama wanaishia kutuimbia tu "Ilani ya Chama Ilani ya Chama," huku hakuna hatua tunazoona za kumuunga mkono mwenzao.

Mimi sioni tatizo la Mwakyembe kutoa taarifa za uhalifu wa aibu kwenye vyombo vya habari. Manake tusipo fanya hivyo, ni wapi tunapojulishwa kwamba serikali imechukua hatua za kukabiliana na wavusha unga na wezi wengine? Yanabaki kuwa siri na ndio maana wakubwa ndio wanaonyooshewa vidole kuwa wao ndio Ma Drug Lords.

Ukweli utabaki kwamba Watanzania tumekuwa tukifaidika zaidi na uwepo wa Mwakyembe pale uchukuzi hata kama anao uwezo mzuri wa kusimamia mambo ya ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Na wengi tunashawishika kuamini kuwa kuondolewa kwake pale kuna msukumo wa kimaslahi ambao hauna heri kabisa kwa nchi hii. Tusaidiane kupambana nao kwa kushinikiza watu kama Harrison Mwakyembe hata kama sio yeye binafsi, WAWEPO KATIKA MAENEO KAMA LILE ALIPOKUWA!
 
Wauza sembe wameiweka siri kali mfukoni pale air port sasa wanapita bila hofu yeyote.

Usijidanganye Serikali haijalala kiasi hicho. Wenzio wamejaribu kusafirisha kupitia JNIA jana mchana. tena walikuwa wamemeza unga kilo moja moja waulize wapo wapi muda huu.
 

Dawa ya Mwakyembe sio kumtetea na kulalama kila kona! Kama yeye jasiri na mchapakazi anayekataa wezi na waovu, anajua majina yote ya vigogo anaosema wamemwondoa ili kufanikisha biashara zao kupitia 'kuliangamiza' shirika la reli (TRL), au kupitia njia haramu za usafirishaji kama magengo, na 'unga' aiport, na kupitisha nyara au bidhaa mipakani, kwa manufaa yao binafsi, AWATAJE MMOJA BAADA YA MWINGINE, aache woga! la sivyo kama anapiga porojo na woga, atakuwa anawahadaa watanzania, kuwadanganya na kuomba huruma 'ambayo hataipata kwa porojo' bali na kuwasema kiukweli-kweli! "Mwaga mboga nami nimwage ugali!" hatasahaulika akisema ukweli! Kama yeye mzalendo AWATAJE ili vyombo husika, PAC na taasisi nyingine zenye uzalendo zifuatilie na kuwawajibisha viongozi hao na familia zao!
 
Hebu mpigie simu mwakiembe tusikie yeye binafsi anasemaje?
Kupiga kazi vile (kwenye media) mpaka kuwaaminisha watanzania halafu mkuu anakuweka benchi mwaka wa uchaguzi aisee unaweza kuwa kichaa jamani!! Kumbe
Utabiri wa shehe Yahya junior kuwa kuna waziri wa jk atakuwa kichaa mwaka huu una weza kuwa kweli!! Mbona ngafu nkamugwangu!
 

Subutu hajitaki? Nao wana yake kibao.
Cc lara
 

Mbatata nakubaliana na hoja yako ya sekta ya uchukuzi kuwa uti wa mgongo. Vile vile, nakubaliana nawe kwamba Mwakyembe alipoingia alikutana na mambo mazito na alifanya jitihada kubwa kuyashughulikia.....lakini tatizo ni kwamba alizama kushughulikia hayo akaacha kushughulikia mambo makubwa strategic katika sekta. Performance ya bandari inapimwa kwa ongezeko la idadi ya mizigo inayopitia hapo, idadi ya meli zinazotia nanga hapo...na sio idadi ya wezi ulioakamata....(sio kuseme kwamba kukamata wezi sio muhimu).

Hoja yako kuhusu action plan, aliipeleka wapi? Kwa nani? Yeye ndiye mwenye dhamana ya utekelezaji wa mikakati yoyte ya wizara, wala haihitaji kupitishwa popote. Ukiangalia mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano, ukiangalia BRN zoote zinatilia mkazo umuhimu wa kundeleza Central corridor kama priority-yaani reli ya Kati na bandari ya Dar es salaam......hivyo kilichobaki ni utekelezaj tu.

Kwa bahati nzuri ipo mifano ya mawaziri waliopata mafanikio ambao waliingia kwenye wizara zao wakiwa na mazingira kama ya Mwakyembe.......Prof muhongo ni mmmoja wao.....aliingia wizara ya nishati kukiwa na mchwa, wezi, wahujumu uchumi wa kila aina......lakini alichukua hatua ya kusafisha uozo na kujikita kwenye kufanya mambo makubwa strategic kama vile kuanzisha miradi mipya ya uzalishaji umeme Kinyerezi 3,4, Usambazaji wa umeme(transmission lines), usambazaji wa umeme vijijini, kupitisha sera na sheria zinazotaka uchimbaji wa madini ya vito nchini ufanywe na watanzania peke yake au wakiingia ubia lazima wawe majority shareholders, na processing ya vito ifanyikie nchini, sekta za gesi nayo inatake off. Je Muhongo aliungwa mkono na nani? Magufuli ambaye amejenga kilomita kibao za barabara kuunganisha nchi nzima anaungwa mkono na nani?


Kuhusu kutoa taarifa za uhalifu hakuna ubaya wowote....... sioni shida Mwakyembe kutangaza waalifu japo sina uhakika kama ilikuwa kwenye instrument (masharti ya kazi) ya waziri wa Uchukuzi...au majukumu ya wizara kwa ujumla


Ni kweli Watanzania tumekuwa tukifaidika na uwepo wa Mwakyembe pale uchukuzi, lakini tungefaidika zaidi maradufu kama angetekeleza majukumu makubwa zaidi (strategic).....miradi ya reli, bandari, ndege inge takeoff.....uti wa mgongo uliousema ungekuwa haswa umetimia....kwa sasa wacha tufaidike naye anapokwenda Afrika ya Mashariki.....kuna mambo muhmu na nyeti ya kusimamia kule kwa maslahi ya taifa,sina shaka kanisa na uwezo wake huko.
 

Hivi mzee huyu anatumia kiungo gani kufikiria lakini...!!?? Jambo la maana analifanyia mzaha kweli..??? It is too much now..!!??
 
Kwani uchukuzi ni kwa ajili ya watu wa Kyela???? ubunge ndio unawahusu na vile mlimfanyia kwenye kampeni wakati EL alipojipenyeza kichini chini kumwangusha, ndoa kabisaaa, hana habari na nyie.

poleni lakini.

Swala la kuwaaid meli kyela ni utapeli wao ilikuwa ktk kutafuta kura ila ilikuwa ahadi walioitoa wao bila kushinikizwa na wana kyela hivyo a hadi ni deni lazima watimize na wasipo timiza lazima wapewe hukumu yao, wanakyela co lazima mwakyembe awe m bunge tuna wasomi wengi sana mwakyembe ni sehemu ndogo ya wasomi na wamiliki wa mali wa kyela asipo jirekebisha tutamuadhibu kyela co wavivu tambua hili uvivu kwetu tunatafsili kuwa ni dhambi, kama kijana wetu Harisoni jiangalie poti
 
Mwakyembe kapelekwa huko ili apate uzoefu wa mambo ya kimataifa,kumbukeni ndo mteuliwa wa uraisi kupitia ccm
 
Wewe uanashindwa kuona kwamba alihangaika sana na TAZARA sio ndio inakwenda huko kwenu? na Songwe airport havitoshi tu hivi?

Kaka ninakuambia hivi pr Mark Mwandosya ndie mwekuheshimika mkoa mzima wa mbeya,co mwakyembe .mwandosya jembe ww
 
Hayo mtajuana wenyewe watu wa ccm bhana , mmeshindwa miaka karibu 60 ndio mtaweza miezi 6 ? Hivi humu JF kuna mtu anaamini hawa magamba watafanya zaidi ya haya waliyofanya ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…