Kikwete: Sihusiki Zanzibar

Mkuu wasipoelewa na hapa basi yaani umeeleza kinagaubaga hilo lipo wazi na ndio maana walikua wanasema ataongozwa na "remote from msoga" Nashangaa leo hii wanatubadilikia kwamba JPM sio chaguo la JK. Wakati Magufuli mwenyewe hakuwa hata na wazo la kuchukua fomu JK ndio kamwaambia tena kwa masharti afanye "kimya kimya" na SHOW kaisimamia mwanzo mwisho JPM mwenyewe hakuna alichokua anajua siri za ushindi alikua nazo JK,Kinana na akina Mangula ivi wanafikiri JK angeamua Membe awe rais ingeshindikana nini?
Sema CCM wanacheza ngoma wanzopigiwa kwa wakati huu ilibidi wampate Magufuli ili kurudisha matumaini kwa wananchi yalikaanza kupotea. Na Magufuli anamuhitaji sana JK sababu ndio Mfumo uliomuweka pale kama ilivyokawa kwa JK miaka yake ya mwanzo akina Rostam na Lowasa ndio walikua wanamcontrol lakini baadae alijua mfumo akawatumbua na kuwa na mfumo wake hata JPM baada ya miaka 5 ndio anaweza kumtumbua JK.
 
Naona unatapatapa Mchaga rais tulishamjua kitambo kama JPM.
 
Ni ukweli ambao hamtaki kuusikia JK ndio aliyemuambia JPM akachukue fomu Pombe mwenyewe akufikiria au na hii unaitaji tochi mkuu? Kwa nini asimuambie Membe? Kama CCM wakimtaka lowasa alipohama chama mbona hawakenda nae Ukawa?
Ulikuwepo?
 

Hahahaha haahaaaaaaaaaaa...
Hahahaha haaaaaaaaaa.....
Hahahahahahaaaaaaaaaa....
Umenifulahisha sana leo dah!


Lakini hata nyerere alikana katakata kwamba kamsaidia karume kwenye kufanya mapinduzi!
 
DO U KNOW THE MEANING OF FACT?
 

Hapo na mm nakukatalia Mkuu. Magu amepigiwa kura na watanzania na wala hakupenya kimungumungu. Inawezekana wote hawakumpigia kura, lakini wengi walimpigia.
 
Je mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi bila Rais wa nchi kujua/kushirikishwa? kweli?
 
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete amesema hajahusika kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kwa kumpigia simu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Aliyasema hayo juzi mjini Kibaha wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Chama ya Kibaha Mjini mkoani Pwani na kusema maneno hayo ni ya uongo, hayana ukweli wowote na watu hawapaswi kutoa shutuma hizo juu yake.

Rais huyo wa Awamu ya Nne alisema maneno hayo hayana kichwa wala miguu wala hajawahi kumpigia simu Jecha kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwani tume hiyo inajitegemea.

“Wasitoe lawama zisizohusika, wapuuzeni sikuwahi kufanya hivyo hata kwa Damian Lubuva wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania hivyo nashangaa watu wanavyosema kuwa nimehusika kufutwa uchaguzi huo,” alisema Kikwete.

“Tume ya Zanzibar ni tume huru na inajitegemea kwani ina mambo yake hata Dk Ali Mohamed Shein (Rais wa Zanzibar) hana uwezo wa kuingilia na kuahirisha uchaguzi huo, watu hao wasipake watu matope wasio husika kwani kila mtu ana nafasi yake,” alifafanua Kikwete.

Alisema kikubwa kinachotakiwa ni kuwaombea Wazanzibari wafanye uchaguzi wao mkuu wa marudio kwa amani na utulivu ili wapate viongozi wao wa kuiongoza Zanzibar na wawaombee wagombea wa CCM washinde.

Chanzo: Mpekuzi
 
Ndio huhusiki ? Lakini kutuma jeshi la JWTZ keenye kituo cha matangazo ya uchaguzi Bwawani na kumchukua Mwenyekiti wa Zec Na makamo wake huhusiki vile vile na walio kuweko kuwaweka under military?

Uchaguzi wa Zanzibar chanzo cha kuvuruga ni wewe kwa kutumia nguvu za kijeshi lakini usione dunia tamu leo kwa vile una nguvu za kibinadamu kufanya zulma .

Ujuwe hizo punzi ni rehma za M/mungu na yeye yupo na huna gerentii naye umebakia muda gani wa maisha yako kuonana na yeye.

Ujuwe tu Allah anasema dua ya mzulumiwa haiendi kwake na akaikataa na mwenye kuzulumu hafaidiki chochote zaidi ya hasara.

Kwahio wazanzibar wameshatuma dua zao na kwahali walio sasa na inayo endelea wamezidi kujiunganisha na kua pamoja na kuwajuwa nyiyi ni watu wa aina gani.

Ccm haito endelea maisha kutawala zanzibsr kwa nguvu zakijeshi iko siku itangoka tu Zanzibar madamu wananchi hawaitaki tena Zanzibar ccm basi hamuweze kuwa force .
 
KWANI Tokea Lini Mchawi Akakiri Kuwa Ni Kweli Yeye Mchawi Na Ndiye Anayehusika KUWAFANYA WATU Wa Kijiji Fulani MISUKULE!!! JAPOKUWA Yeye Amekanusha, Ila Watanzania Wajua Kilichojiri, Kilichopo Na Kinachokuja ZANZIBAR Na MHUSIKA Mkuu Wa Kutoa MAELEKEZO Yale Anajulikana!!! ZANZIBAR Kama Ni Sehemu JMT, Haiwezi Kufikia Maamuzi MAKUBWA Vile, Pasipo KUSHIRIKISHA Tanganyika!!! NA CCM Visiwani Hawafanyi Maamuzi Mkubwa Pasipo Kupata Miiongozo Ya Upande Wa Bara!!! HIVYO Maneno Yake Ni Sawa Na MWIZI Anayekanusha Kuiba Simu, Wkt Alikuwepo Tukio Lilitokea Na Kukutwa Na Ushaidi!!!
 
Haya maneno yangeingia kwenye alili za waelewa
kama tume za uchaguzi zingekuwa huru..... kama watendaji wa NEC walikuwa wanabadilishwa na JK hata ndani ya mwez mmoja anatwambia nini hapa...... ni punguani pekee anaweza elewa hili..... tengenezeni tume huru za uchaguzi plz....
 
Mkuu chaguo la JK lilikuwa ni membe baada ya kuona asinge pita kwenye chujio akaona amshauri magufuli na kumuahidi kimyakimya kuwa atamuunga mkono, hivyo baada ya kuona membe amekwama akaacha maji yafuate mkondo wake huku akijua magufuli anakubalika zaidi
 
Mkuu ulikuwepo?
Kwani mkuu unafikiria Kongo lilizungumkwa jengo LA bwawani na vifaru hamna kuingia MTU wala kutoka mwisho makamo mwenyekiti akachukuliwa mzoba mzoba sehem isiojuilikana kikwete anahusika kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…